Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, December 20, 2014

News Alert: Uchaguzi S/Mitaa marudio kesho; hujuma Kinyerezi; wananchi kuchukua sheria mkononi


Kinyerezi: Katika mitaa ya Kichangani na Kibaga ni kati ya maeneo ambayo uchaguzi unarudiwa kesho Jumapili Dec 20, 2014. Wakazi wa Kinyerezi wamekuwa wakilalamika leo hii kuona hujuma za waziwazi zikifanywa kwa kuandikisha watu ambao sio wakazi wa huko. Wamekuwa wakihoji mbona muda wa kuandikisha umekwisha ili hali kuna vijana ambao hawafahamiki wamekuwa wakiandikisha? Pia ina semekana watu wanao andikishwa ni kutoka Ilala, Vingunguti na Buguruni

Zaidi, wakazi wa Kichangani (ambako kuna wagombea wa CUF na CCM) na Kibaga (ambako kuna wagombea wa CHADEMA na CCM) wameweka mikakati mikali ya kuwafukulizia mbali watu ambao watajidai kupiga kura na sio wakazi wa maeneo hayo. Wakazi hawa ambao wanalilia demokrasia ya kweli wamekuwa na mikakati mikali ya kuhakikisha mamluki hayapigi kura. 

Hadi hii habari inaandikwa kumekuwa na mawasiliano ya hapa na pale kwa wakazi wa Kinyerezi wakijadili namna ya kuona uchaguzi huru na haki. Kibaya ni kuwa kuna baadhi ya wakazi hawa ambao wamesema watachukua sheria mkononi zidi ya hujuma hizi

2 comments:

Unknown said...

Jaman haki itendeke wakubali kuxhindwa, kipind cha mabadiliko hik

Unknown said...

Haki itendeke jaman