Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, November 25, 2014

Muhongo ahusishwa wizi nyaraka za Escrow bungeni


Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, ametajwa kuwa na uhusiano wa karibu na mmoja kati ya vijana wawili wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi  mkoani hapa kwa tuhuma za kuiba kutoka Ofisi ya Katibu wa Bunge ripoti ya ukaguzi wa hesabu za zaidi ya Sh. bilioni 300 zilizochotwa kifisadi kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Ukaguzi huo ulifanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).Wakati Waziri Muhongo akitajwa kuwa na uhusiano wa karibu na mtuhumiwa huyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, ambaye jana ilikuwa ni siku yake ya kwanza kuongoza Bunge tangu lianze Novemba 4, mwaka huu, anadaiwa kutajwa kuwamo katika orodha ya vigogo waliovuna fedha hizo, huku yeye akipata mgawo wa Dola za Marekani milioni moja.

Aliyemtaja Waziri Muhongo kuwa na uhusiano wa karibu na kijana huyo, ni Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika. Mnyika alimtaja Waziri Muhongo, wakati akichangia mjadala kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2014, bungeni jana. Muswada huo uliwasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, bungeni, Ijumaa wiki iliyopita. ”Mheshimiwa Spika, ni muhimu ofisi yako ifuatilie. Kwa sababu mtuhumiwa yule ana uhusiano wa karibu sana na Prof. Sospeter Muhongo, ambaye ni mmoja wa watuhumiwa kwenye kashfa tunazozijadili,” alisema Mnyika. Aliongeza: “Sasa nasema haya mapema ili isifikie hatua tukatumiwa kisingizio cha mambo kuwa mahakamani kushindwa kuwataja kwa majina wahusika. Polisi wafanye uchunguzi, wachukue hatua.”

Tucta yamtaka JK kuwatimua waliohusika kuchota Escrow


Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limemtaka Rais Jakaya Kikwete atumie rungu lake kuwawajibisha vigogo  wote waliohusika na uchotaji wa fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, liyoko katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).   Rais wa Tucta, Gratian Mukoba, (pichani) aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Alisema Tucta inaamini kuwa wizi kama huo wa fedha za umma unakwamisha jitihada za  kupatikana kwa mishahara bora kwa wafanyakazi pia unakwamisha ulipaji wa madeni ya walimu kwa muda mrefu.

“Tunajua kuwa zipo juhudi za kufunika suala hilo kupitia baadhi ya wabunge wanaojali maslahi yao, kamwe Tucta hatutakubali pamoja na Watanzania wanyonge kushuhudia fedha na rasilimali zikiibwa na kunufaisha wachache,” alisema. Alisema wizi huo ni ishara kuwa nchi inaelekea kubaya kwani Watanzania wanyonge wamechoka kushuhudia rasilimali na fedha zikiendelea kuwanufaisha watu wachache huku kundi kubwa likiendelea kutaabika.

Tanzania Daima

Mkono: Nimelishwa sumu

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM), amesema licha ya kulishwa sumu na watu asiowajua hatohama Tanzania kama anavyoshauriwa. Mkono, pia amegoma kuzungumzia sakata la IPTL na akaunti ya Escrow hadi apate kibali cha Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema. Kauli hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari juu ya tukio la kulishwa sumu na kulazwa hospitalini nchini Uingereza. Mkono, alisema Novemba 11 mwaka huu akiwa na wabunge wenzake wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, walikwenda nchini Uingereza kwa ziara ya kikazi, ambako alipofika huko aliugua ghafla na kukimbizwa hospitali. Alisema akiwa hospitali, wabunge wenzake wakiongozwa na Mwenyekiti William Ngeleja, waliwasiliana na ndugu zake juu ya tukio hilo na waliwapa maelekezo ya kuwasiliana na daktari wake (Mkono), Dk. Kapteni

Mkono, alisema Dk. Kapteni anayefanya kazi hospitali ya TMJ, aliwaelekeza wenzake dawa za kumpa kwa kuwa alihisi amelishwa sumu. “Ukweli nimelishwa sumu, madaktari wameshathibitisha jambo hilo…sijui kina nani walionifanyia hivi, uchunguzi wa aina ya sumu na mtu aliyenipa bado vinaendelea…, waliotenda hivi wanajidanganya,” alisema. Mkono, alisema akiwa jijini Dar es Salaam alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms), ikimtahadharisha juu ya safari yake na madhara atakayoyapata. Alisema baada ya kutumiwa ujumbe huo, aliwaonyesha wenzake ambao walimtia moyo na kumtaka awe muangalifu na nyendo zake. Mkono, alisema ujumbe huo utakuwa ni sehemu ya uchunguzi wa tukio lake aliloliita ni la kihuni, lilifanywa na wahuni wasiomtisha.

“Nimeshauriwa nihame Tanzania kwa kuwa tumefikia hatua mbaya, lakini mimi nimesema sihami kwa sababu ya wahuni wachache,” alisema. Alibainisha kulishwa sumu kwa wabunge si jambo geni hapa nchini, kwa kuwa hata Waziri wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe, alifanyiwa hivyo na kukimbizwa nje ya nchi kwa matibabu.
Kuhusu IPTL

Zitto: Maisha yetu hatarini

        Siku moja kabla ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwasilisha bungeni, ripoti ya uchunguzi wa IPTL kuhusu ufisadi katika akaunti ya Escrow, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe amesema amekuwa akipata vitisho ili kuzuia ripoti hiyo. Akizungumza jana, Zitto alisema pamoja na vitisho hivyo haogopi kwa kuwa maisha yake ameshayaweka nadhiri siku nyingi. “Kuna kundi la wahuni kutoka Musoma limeletwa Dodoma likiongozwa na mtu (jina tunalihifadhi) mwenye rekodi ya ujambazi. Hivi sasa anashikiliwa na polisi kwa kukutwa na nyaraka zilizoibwa Ofisi ya Bunge. Usalama wa wajumbe wote wa PAC upo shakani,” alisema Zitto. Aliongeza kuwa kuna vipeperushi vimesambazwa mjini Dodoma kumkashifu lakini havitamsumbua kwa kuwa yeye anataka ukweli ujulikane.
Baadhi ya wabunge jana walionekana na kitabu kilichoandikwa ‘mjue Zitto Kabwe kama mtetezi wa wanyonge,’ lakini ndani yake kikiwa na mambo ya kumchafua mbunge huyo. Vitabu hivyo vinaelezwa kusambazwa kwa wabunge katika nyumba zao vikilenga kuonyesha kwamba Zitto hafai kusimamia PAC ambayo hivi sasa inashughulikia escrow. Wakati Zitto akisema hayo, suala hilo la vitisho jana pia liliibuka bungeni baada ya Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed kueleza kuwa hali ni tete kuhusu usalama wa wabunge kutokana na escrow. Akiuliza swali la nyongeza, Mohamed alisema usalama wa wabunge uko shakani kuanzia maeneo wanayofanyia kazi na makazi yao na hasa kipindi hiki tangu kuanza kwa sakata la escrow.

Sunday, November 23, 2014

SEHEMU YA TAARIFA YA CAG JUU YA ESCROW


Hapatoshi:Wabunge wa upinzani wadai ripoti imechakachuliwa

             Hali ni tete. Ndiyo neno ambalo unaweza kulizungumza kuhusu kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow. Mji wa Dodoma tangu juzi umejaa pilikapilika zikiambatana na mikutano iliyokuwa ikijadili kashfa hiyo. Kamati ya Uongozi wa Bunge, Kamati ya Uongozi wa Wabunge wa CCM, Baraza la Mawaziri, kwa nyakati tofauti walikaa kujadili ripoti ya escrow ambayo inatarajiwa kujadiliwa na Bunge Jumatano na Alhamisi. Leo kikao cha wabunge wa CCM kinatarajiwa kufanyika kujadili suala hilo. Wabunge walionekana kila kona ya Viwanja vya Bunge jana wakijadiliana katika vikundi kuhusu sakata la escrow, huku wengine wakitaka hata miswada yote iliyobaki isijadiliwe ili kutoa nafasi kuichambua kwa kina kashfa hiyo.
Wabunge wa kila vyama wamekuwa wakikutana kuweka misimamo yao kuhusu namna watakavyoshiriki kujadili ripoti hiyo. Wabunge wa CCM wamegawanyika katika makundi matatu; linaloshinikiza waliohusika na wizi huo wajiuzulu, kundi la watu wasiokuwa na msimamo na kundi linalotaka ripoti isijadiliwe bungeni. Kikao cha Kamati ya Uongozi kilichofanyika jana asubuhi kilikubaliana suala hilo la escrow lijadiliwe kwa siku mbili badala ya moja iliyokuwa imepangwa awali.
Kamati ya Uongozi CCM

Friday, November 21, 2014

Mahakama yakana barua kuzuia mjadala


      Wakati Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakichachamaa wakisema hawatakubali Bunge hilo kuingiliwa na mhimili wa Mahakama, Mahakama hiyo imejiweka kando na tuhuma hizo. Sakata hilo lililotawala kikao cha Bunge hilo jana lilitokana na madai yaliyoibuliwa juzi na wabunge wa kupinzani unaoundwa na vyama vya CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi. Wabunge hao Tundu Lissu (Chadema), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Habib Mnyaa (CUF) waliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma juzi kuwa wamepata taarifa za uhakika kuwa Mahakama imeandika barua ikiritaarifu Bunge lisijadili kashfa ya uchotaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania. Wabunge hao,  walisema kuwa hatua hiyo ni kuingilia uhuru wa mhimili wa Bunge na kwamba lengo lake ni kutaka kukwamisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili wahusika wasichukuliwe hatua.

Msajili wa Mahakama Kuu, Amir Msumi, alipotakiwa  jana na NIPASHE kuthibitisha kama Mahakama imeandika barua hiyo kwenda Ofisi ya Spika wa Bunge kuzuia suala hilo lisijadiliwe kwa kuwa kiko mahakamani, alisema yeye na wasajili wenzake hawana taarifa kuhusu kuandikwa kwa barua hiyo.  “Labda unieleze hiyo barua imeandikwa na nani na lini, kama ni Jaji au Msajili nitajie jina lake ili iwe rahisi kufuatilia, lakini hadi sasa nimepekua kwenye kumbukumbu zetu sijaona barua hiyo,” alisema Msumi. Aliahidi kwamba jana angewasiliana na wenzake wa Mahakma ya Rufani kama kuna barua imeandikwa kutoka mahakama hiyo kwenda bungeni.

Hadi sasa hakuna mamlaka yoyote ya serikali iliyothibitisha rasmi kama kuna barua iliyoandikwa na Mahakama kwenda Ofisi ya Spika wa Bunge. Juzi Naibu Spika,Job Ndugai, alisema kuwa ofisi ya Spika haijapokea barua hiyo. Hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akizungumza bungeni jana kuhusiana na madai hayo, hakuthibitisha wala kukanusha kama kuna barua iliyoandikwa na Mahakama kwenda bungeni kuzuia mjadala huo, zaidi ya kusisitiza itumike busara ili kuepusha mihimili hiyo kuingiliana katika majukumu yao kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Nipashe

NIMROD MKONO ALISHWA SUMU, ILIKUWA AFE NDANI YA MASAA 72


Mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono amelishwa sumu ambayo ilibidi imuue ndani ya masaa 72. Siku mbili baada ya kufika London, Uingereza kwa shughuri za kibunge na wenzake Mh. Mkono alidondoka na kuwahishwa hospitali. kabla ya kudondoka Mh. mkono alikuwa akitoka jasho jingi sana. Baada ya kufika kwa dactari; dactari amesema sumu hiyo ilikuwa ina teketeza figo zake.

Awali ya hapo Mkono alipewa tahadhari na watu wake wa karibu kuwa muuangarifu na safari yake na hoteli ambazo ameandaliwa kwenye safari hiyo. 

Mkono alikuwa mshauri mkuu kwenye kesi ya Tanesco na Serikali dhidi ya IPTL. inaaminika kwa wengi kuwa Mh. Mkono ndio aliye vujisha kashfa ya ESCROW

The Citizen

Kitimtim bungeni

            Kitimtim bungeni. Hicho ndicho kilichotokea bungeni jana baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuwaomba wabunge kukishauri kiti chake juu ya hatua ya kuwasilishwa na kujadiliwa kwa ripoti ya uchunguzi wa IPTL kwa madai ya kuwapo kesi mahakamani. Wabunge wa pande zote – chama tawala na upinzani  waliopata fursa ya kuzungumza, walitoa kauli zinazofanana za kutaka suala hilo lijadiliwe na chombo hicho cha kutunga sheria, huku wakipinga njama za kutaka kuzima hoja. Hata pale Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipojaribu kueleza umuhimu wa kumaliza suala hilo bila mihimili ya Bunge na Mahakama kuingiliana, zilisikika sauti wabunge wakimzomea, ikimaanisha kuwa suala hilo lazima lijadiliwe kwa uwazi bungeni.
Kwa jinsi mjadala huo wa wabunge ulivyokwenda, ni dhahiri kwamba ripoti hiyo iliyochunguza kuchotwa kwa Sh306 bilioni katika akaunti ya Tegeta Escrow italeta mtikisiko mkubwa serikalini na bungeni kama ambavyo gazeti hili liliripoti Jumanne iliyopita. Wabunge wanane waliochangia mjadala huo walionekana wazi kutaka kiti cha Spika kitumie mamlaka yake vizuri kuhakikisha ripoti hiyo inawasilishwa bungeni haraka na kujadiliwa ili waliochota fedha hizo “wabebe msalaba wao”. Mjadala huo mkali uliibuka baada ya kuibuka taarifa kwamba kuna barua kutoka mahakamani iliyowasilishwa kwa Bunge kutaka kuzuiwa kwa mjadala huo, barua ambayo hata hivyo, Ndugai alisema hajaiona.
Naibu Spika alitoa fursa hiyo baada ya kuombwa mwongozo na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila aliyetaka kujua iwapo ripoti hiyo itawasilishwa bungeni au la, kutokana na kuwapo kwa madai ya barua kutoka mahakamani. “Tunataka tujue ripoti italetwa au la, tunasikia kuna mkakati wa kimahakama kuzuia isije, sasa tunataka utuhakikishie kama itaingia bungeni kwa kuwa Mahakama haipaswi kuingilia Bunge,” alisema Kafulila. Kabla ya kujibu mwongozo huo, Ndugai alisema: “Kama mlivyozungumza hili ni jambo la haki za Bunge, sasa naomba mkisaidie kiti tujadili mwelekeo.”
Kafulila
Aliyepewa nafasi ya kufungua mjadala huo ni Kafulila aliyeanza kwa kutoa ushauri kwa kiti cha Spika kuwa Bunge ndilo lenye mamlaka ya mwisho na wabunge ndiyo wawakilishi wa wananchi, hivyo kuna mtihani kuhusu jambo hilo na Bunge ndilo litaamua. “Ni lazima tujue kama Bunge tunatosha au hatutoshi, kama Bunge linaweza au haliwezi. Kama taarifa zinasema kuna majaji na viongozi wamekula fedha hizo halafu kuna hoja ya kuzuia eti jambo liko mahakamani. Hilo jambo halina msingi kama kweli kuna hoja ya Mahakama mbona CAG alipochunguza kwa niaba ya Bunge haikuzuia?” Alisema ni lazima Bunge lifanye uamuzi kama ilivyoamuliwa tangu mwanzo.
Bulaya
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya alisema lazima Bunge liheshimiwe kwa kuwa haiwezekani mhimili mmoja ukaingilia mwingine na kujifanya uko juu. “Sisi tunachojadili hapa ni ripoti ya CAG na hii ni ripoti ya Bunge na si ya Serikali. Hatujadili kesi hizo alizosema Waziri Mkuu, hatuwezi kukubali Mahakama moja ikatoa uamuzi tofauti katika jambo moja,” alisema Bulaya. Alisema ni muhimu Bunge likaendelea na ratiba yake kuhusu ripoti hiyo na kila mtu achukuliwe hatua kwa kile alichokitenda.
Lekule Laizer
Mbunge wa Longido (CCM), Michael Lekule Laizer alisema wabunge wengine hawalielewi suala la escrow lakini kama kweli kuna wezi ndani ya Bunge wachukuliwe hatua na ripoti hiyo iwasilishwe bungeni. “Hili jambo ni kubwa na tumegawanyika kwa kuwa wengine hatulijui vizuri. Kama kuna wezi humu ndani au nje ya Bunge naomba Naibu Spika tusifiche maovu, tusifuge wezi, hivyo ripoti ije haraka na liwe ni jambo la dharura, waliokula wabainike na washughulikiwe. “Hili jambo lijadiliwe na Kamati ya Uongozi ikae leo (jana) ili jambo hili lije kwenye ratiba ya kesho (leo),” alisema Laizer na kushangiliwa na wabunge wengi.
Msigwa