Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, December 20, 2014

NEWS ALERT: Mgombea CHADEMA atoweka kwenye mazingira ya kutatanisha

Mgombea uenyekiti, Ndg. Erick Ngiliama, kijiji cha Mahango kata ya Madibila wilayani Mbarali amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha tokea December 18, 2014 usiku. Mke wa Ndg. Ngiliama alipo hojiwa amesema kuna watu walikuja kumkamata usiku wa December 18 wakijitambulisha kama polis. 

Baadhi ya maeneo Wilayani Mbarali kama kijiji cha Kapunga hali sio nzuri; vijana wengi wamekimbia majumbani kwao na kujificha maporini.  Hali hii ya ukimbizi imetokea wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo vijana pamoja na wakina mama wenye mlengo wa upinzania wamekuwa wakikamatwa usiku wa manane na kuwekwa ndani bila sababu za msingi. Hadi juzi kulikuwa na watu zaidi ya 40 jela.  Jana Ijumaa watu 20 waliachiwa huru akiwemo Diwani wa Mapogolo Ndg. Ramadhan Garahenga; huku wengine wakiendelea kusota jela.

Kwa bahati mbaya, sintofahamu lipo kwa katibu kata wa Madibila/CHADEMA Ndg. Erick Ngiliama ambaye haieleweki amepelekwa wapi baada ya kukamatwa.  Ndg. Ngiliama alikuwa anagombea uenyekiti wa kijiji cha Mahango kwa tiketi ya CHADEMA

No comments: