Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, December 17, 2014

CCM ‘yapoteza’ viti 2,600 Serikali za Mitaa

Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imetangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa Serikali za mitaa nchi nzima yanayoonyesha kuimarika kwa upinzani. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Tamisemi), Khalist Luanda alisema jana kwamba wakati CCM ikifanikiwa kupata ushindi wa jumla mitaa na vijiji 9,406, kwa pamoja vyama vingine vya upinzani, vimegawana nafasi 3,211. Kwa ushindi huo upinzani umeongeza viti 1,981 ikilinganishwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita mwaka 2009 ambao kwa ujumla, ulipata nafasi 1,230 za wenyeviti wa mitaa na vijiji.
Kwa upande wake, CCM imepoteza nafasi 2,636 za uenyekiti wa vijiji na mitaa ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2009 ilipopata jumla ya viti 12,042. Hata hivyo, uchaguzi mwa mwaka huu, umefanyika huku kukiwa na nyongeza ya mikoa, wilaya, mitaa na vijiji katika baadhi ya maeneo nchini. Luanda alisema CCM kimepata vijiji 7,290 kikifuatiwa na Chadema yenye vijiji 1,248. CUF imeshika nafasi ya tatu kwa kuwa na vijiji 946, ikifuatiwa na UDP yenye vinne na TLP na NLD vyenye viwili kila kimoja. Katika nafasi za wenyeviti wa mtaa, CCM kimechukua jumla ya mitaa 2,116. Vyama vingine na nafasi zao kwenye mabano ni Chadema (753), CUF (235), ACT (9), NCCR - Mageuzi (8) wakati vyama vya TLP, UMD, UDP na NRA vimepata mtaa mmoja kila kimoja.
Matokeo hayo yamejumuisha maeneo mengi ambayo CCM ilipita bila ya kupingwa. Katika matokeo hayo, CCM imeendelea kufanya vizuri katika mikoa ambayo imekuwa ikitajwa kuwa ni ngome yake lakini kuna maeneo ambayo yalionekana kuyumba kwa kuzolewa na upinzani. Mfano wa ngome ambazo CCM kimetikiswa zaidi ni Mkoa wa Dodoma katika wilaya za Kondoa na Chemba ambako vyama vya CUF na Chadema vimefanya vizuri tofauti na uchaguzi uliopita. Kuhusu nafasi ya mwenyekiti ambaye alisimikwa na wananchi kibabe katika Mkoa wa Arusha, Luanda alisema Tamisemi haitamtambua, bali atakuwa ni mwenyekiti wa kimila tu.
Mwananchi

No comments: