Mwandi, Kichangani, Morogoro kumetokea taharuki baada ya mgombea wa CHADEMA kushinda kwa kura 276 na CCM kupata 275. Aliye kuwa anasimamia, ni binti ambaye yupo kwenye 20's yrs old akalopoka kuwsa CHADEMA wameshinda. Kulikuwepo na mtendaji ambaye baada ya kusikia kauli ya kuwa CHADEMA imeshinda, akapiga simu ambapo hiyo simu ilikuja na maelezo kuwa matokeo lazima yageuzwe. CHADEMA walikuwa macho waki hakikisha kura haiibiwi hata moja.
Baada ya ile simu, mtendaji akambonyeza yule msichana msimamizi. Yule dada wakati wa kusoma matokeo alianza kwa kusema; CCM wamepata kura 275, na CHADEMA wamepata kura 276. yule binti akasema kwa sauti kuwa "MSHINDI NI CCM". Baada ya hapo ilitokea taharuki kubwa sana. Kulikuwa na mgambo ambaye alipiga simu polis. Polis walifika na mabomu yao.
Wananchi walionekana wana hasira na kuwaambia askari mtupige tu mabomu. Askari wakasema jamani sisi hatujaja kuwapiga mabomu na tunaomba mtulie tumekuja kusimama katika haki. Hapo wananchi na mawaka wakaanza kueleza kwa mapolis kilicho sibu. Yule dada (msimamizi) akaulizwa tena; "nani aliyeshinda hapa?. Akasema CCM.
Wakati huo, mabox ya kula yalikuwa yameingizwa ndani na ikatoka amri yaletwe nje na kura zihesabiwe tena. Mabox yakaletwa nje na CHADEMA wakagoma kuhesabia tena wakisema CCM hatuwaamini kwani kwa kupeleka mabox ndani lolote laweza kuwa limesha fanyika.
Wakati taharuki na mzozo huo ukiendelea, watu wa CCM walikuwa waki piga kelele "ZIHESABIWE TENA, ZIHESABIWE TENA". Kulikuwa na kijana mmoja wa CHADEMA ambaye alikuja mbio na kupita katikati ya polis kisha kubeba sanduku moja la kura na kutokomea nalo. Polis wakashikwa na butwaa; hawakumkimbiza wakawa wanamuangalia tu. Hadi sasa haijulikani hilo box limeenda wapi.
Baada ya hapo Mgurugenzi alipigiwa simu na akafika na viongozi wengine. Viongozi hawa wakauliza kilicho jili na kila mtu akawa anaeleza la kwake. Hawa wanasema imeshinda CCM na hawa CHADEMA. Baada ya kuona pressure ni kubwa sana mkurugenzi akasema uchaguzi ni BATILI na urudiwe tena siku ya Jumapili. Mawakala na wahusika wote wakaandikishana hapo hapo na Mkurugenzi akaishia. Hii ilikuwa ina tokea saa kumi za usiku.
Baadhi ya Polis wamehojiwa kwa nini hamkumkimbiza jamaa wa CHADEMA amekimbia na kura? Polis wanasema hata sisi tupo huko huko na tumnaona wazi wananchi wamechoka.
habari zaidi kutoka Morogoro zinasema kuwa viongozi wa CCM Morogoro na kitaifa wamechanganyikiwa kwa sababu mkoa wa Morogoro ni kati ha mikoa ambayo CCM imeishika vizuri na CHADEMA imekuwa haina nguvu; lakini kwa sasa ni story tofauti kabisa.
No comments:
Post a Comment