USHAURI
alioutoa Mhe Mizengo Kayanza Pinda katika semina ya kujadili na kupitisha
kanuni zitakazotumika kujadili na kupitisha ibara na vifungu vyake vya rasmu ya
katiba. Ushauri ambao ulijaa busara
ndani yake, kama kamati ya kanuni na wajumbe wa bunge hili watazingatia
utamwingiza Rais Kikwete kwenye historia.
Nasema
hivi kwa sababu mambo yanye mabishano/mvutano mkubwa kama hayataamuliwa kwa
busara ha hekima watanzania hatutapata katiba tuitakayo na baadaye hatutapata
Tanzania tuitakayo na kumfanya si tu Rais Kikwete asiingie kwenye historia bali
pia hata bunge lenyewe litaingia katika historia mbaya.
Mhe
Mizengo Kayanza Pinda ametoa ushauri kuwa mambo ambayo yatakuwa na mabishano/mvutano
mkubwa yasiamuliwe na kura ya 2/3 ya wajumbe wa bunge
maalumu la katiba, badala yake yaundiwe jopo (roundtable) la watu wenye mapenzi
mema na uzalendo kwa nchi si tu kuamua
bali pia kupitisha mambo yenye manufaa kwa watanzania wote bila kujali itikadi
zao, makundi yao, jumuiya zao wanazowakilisha.
Waziri
mkuu Mizengo Pinda si tu ameachukua ushauri wangu kwa wajumbe wa bunge maalumu
la katiba nilioutoa katika makala zangu mbili katika Gazeti hili makini tole
Na. 3372 la 26/02/2014 yenye kichwa cha habari “Bunge maalumu la katiba kipimo
cha kuchaguliwa tena 2015” na makala nyingine katika Gazeti hili hili lenye
kichwa cha habari “Bunge halina mamlaka
ya kupigia kura rasimu ya wananchi” bali Mhe Mizengo Pinda ametoa ushauri
huo baada ya kusoma alama za nyakati kwamba kuamua ibara na vifungu vya rasimu
iliyotokana na maoni ya wananchi k wa kupigia kura ni kuwashushia hadhi hasa
wabunge wa CCM kwa kuwa wao ndiyo wengi na kuwafanya wasichaguliwe tena kama
chama katika chaguzi za Serikali ya mtaa na ule wa mwakani 2015.
Ushauri
wangu katika makala hizo mbili, ushauri ambao umeungwa mkono na Mh Mizengo
Pinda utalinusuru bunge kama kupitisha kanuni kumeleta vurugu je wakati wa
kupitisha ibara na vifungu vyenye ubishani kama watatumia kupiga kura
itakuwaje? Jibu la swali hili ndilo litapelekea ushauri wangu na wa Mhe Pinda
uzingatiwe.
Katika
ushauri wangu pamoja na maombi mengine niliwashauri, wajumbe wa bunge hili la
katiba kuwa si tu watakuwa wamefanya
makosa makubwa kupigia kura maoni yaliyopo kwenye rasimu ya katiba iliyotokana
na wananchi bali pia hawana mamlaka ya kufanya hivyo. Nawakilazimisha kufanya hivyo si tu
watakuwa wamewapuuza watanzania bali pia
kuwasaliti watanzania kwa kukataa maoni yao kwa kupiga kura ya hapana.
Kitendo
cha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwaomba wajumbe wenzake wabunge la katiba
kujadili na kupitisha ibara vifungu vyenye mabishano/mvutano mkubwa kwa kutumia
jopo (roundtable) la watu wenye busara na uzalendo na nchi yao ndani ya bunge
lenyewe si tu atalifanya bunge hili kuingia katika historia nzuri ya kuwaletea katiba
yao iliyotokana na maoni yao.
Ili
nisiwe mwizi wa fadhila, aina hiyo ya pongezi niwamiminie, kiongozi wa kambi
rasmi ya upinzani Mh Freeman Mbowe na Prof. Ibrahim Lipumba kwa kuunga mkono kauli ya Waziri mkuu Mizengo
Pinda kuwa mambo yenye mvutano/ubishani yajadiliwe kwa busara na kuamuliwa kwa
pamoja na jopo (roundtable) la watu wenye si tu na busara bali pia wenye
mapenzi na uzalendo na nchi yao ndani ya Bunge hilo la Katiba.
Kauli
hiyo ya Mhe Mizengo Pinda kama Mwenyekiti wa Bunge wa CCM ni dalili tosha kuwa
inachukuliwa kama kauli ya wabunge wote wa CCM, kwa hiyo ninawapongeza wabunge
wote wa CCM kuliona hilo, ambalo mimi nililiona mapema zaidi na nikalitolea
ushauri mapema katika makala nilizozitaja hapo juu ingawa mimi nilipendekeza
mambo hayo yaamuliwe na Majaji 11 kutoka nje ya bunge badala ya kupigiwa kura
ya 2/3 ya wabunge hilo la katiba.
Kuamua
mambo yatakayokuwa na ubishani/mvutano mkubwa kwa ushauri wa Waziri mkuu
Mizengo Pinda ni kuonyesha wao wenyewe wanauwezo wa kufanya jambo hilo
nililokuwa nimewashauri bila kupata watu nje ya bunge hilo kwa kuunda jopo
ndani ya bunge.
Aidha
dalili za hicho alichokishauri Waziri mkuu Mizengo Pinda kitapata uhai baada ya
Bunge hilo kupata mtu makini na mwenye uwezo mkubwa kuliongoza bunge hilo kama
Mhe Samweli Sita.
Kwa
lugha nzuri unaweza kusema “kazi ya Mwenyekiti wa bunge inatakiwa
kupata mtu siyo mtu amepata kazi ya kuwa Mwenyekiti wa bunge”
(Mwl. Anthony Gella).
“Mimi
bado napigia kelele utaratibu wa kufanyia maamuzi ibara na vifungu
vilivyotokana na maoni ya wananchi baada ya wabunge kutofautiana kwa kupigia
kura ya ndiyo na hapana badala ya kufanya marekebisho ibara hiyo ikaaje kwa manufaa
ya watanzania na baadaye kutuletea sisi tupigie kura tena ya ndiyo au hapana,
huku ni kuwasaliti watanzania” kanuni mlizipitisha za kupiga kura
badala ya maridhiano hazijawatendea haki watanzania.
Baada
ya kauli hiyo ya Mhe Pinda ninawasihi wabunge wote wanatokana na Chama cha Mapinduzi
(CCM) kuungana na Mwenyekiti wenu Mhe Pinda kwa busara kubwa alizozitoa kwa
wajumbe wote wa bunge hilo maalumu la katiba, kufanya hivyo si tu kujiongezea heshima mbele ya watanzania bali
pia ni kumwingiza Rais wetu Jakaya Kikwete kwenye historia nzuri ya
kuwaletea watanzania katiba waitakayo na makundi yote ya watanzania. Na kufanya kinyume na hilo ni kujinyima
wenyewe historia nzuri na kumyima pia Rais Wetu aliyelianzisha suala hili kwa
nia ya kuwaletea watanzania katiba yao waitakayo na baadaye waipate Tanzania
waitakayo.
“Mimi
binafsi nafurahi ujumbe wangu si tu
umefika bali pia umefanyiwa kazi na Mhe Mizengo Pinda na naomba wajumbe
wa bunge maalumu la katiba mfanyie kazi pia”.
Nawatakia
kila la kheri kuingia katika historia kama lilivyo bunge la kihistoria na
kumwingiza pia Rais wetu katika historia.
Na Mwl. Anthony Thomas Gella
0656 907751
agella72@yahoo.com
No comments:
Post a Comment