Na Bryceson Mathias, Mvomero
MCHUNGAJI Salvatory Vicenti wa Kanisa la Uponyajila Lusanga Mji Mdodo wa Madizini, amewaonya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba akidai, wasipompiga Adui wa Katiba hiyo kwa pamoja ili kufanikisha matakwa ya wananchi na badala yake wakaweka mambo yao binafsi, Historia itawahukumu.
Mchungaji huyo amesema, anashangazwa kuona pamoja na Heshima kubwa ambayo Rais Jakaya Kikwete amewapa kuwateua miongoni mwa watanzania Milioni 45 ili kushughulikia Maboresho ya Katiba hiyo, wamejisahau na kuona wao ni muhimu kuliko wananchi na Rais.
Akizungumza na Tanzania Daima katika Maombi ya kuombea Mustakabali wa Katiba hiyo yanayoendelea kanisani kwake, Mchungaji Vicenti alisema, Biblia inaonya kwamba Uroho ni dhambi! Hivyo anapoona wajumbe waliobarikiwa na Mungu kuwa na kipato cha kutosha, na kupewa kibari cha kujadili rasimu hiyo halafu bado Posho zaidi ni Hatari kwa Taifa.
Mchungaji Vicent ambaye alionesha ni Muumini wa Serikali Tatu alisema, “Uroho ni hamu isiyoratibiwa ya kujipatia mali kuliko mtu anavyohitaji, hata kuwakosesha wengine.Ni chanzo cha maovu mengi katika maisha ya jamii, kama vile unyonyaji, wizi, na vita.“Kwa sababu hiyomaadili ya Kanisa yanauhesabu hivyo ni kama kati yavilema vikuu ambavyo vinasababisha dhambinyingine”.alionya.
Vicenti alikwenda mbali akiufananisha uroho na Mtu Mvivu ambaye anataka apate vitu bila kufanya kazi halali ambapo alinukuu maandiko ya Mithali 6:6-9 yanayosema,
“Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?”.alisema Vicenti akiwataka wajumbe waache usingizi wakidai Posho!
No comments:
Post a Comment