Na Bryceson Mathias, Kilombero Morogoro
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Azimina Mbilinyi, ametupiwa Lawama na wananchi wa Kata ya Kibaoni, wakimtuhumu kutoiorodhesha Kata yao kwenye Uchaguzi Mdogo wa Madiwani wa Kata 27 uliofanyika hivi karibuni, hali akijua hawana Diwani. Kwa Miezi 9.
Aidha Wananchi hao pia wameilalamikia Serikali Kuu kwa kutoihusisha Kata hiyo katika Uchaguzi huo, hali ikijua Wananchi wa Kata hiyo, wanakosa Mtu wa kusimamia Maendeleo na kuwaondolea Kero zinazowasibu tangu alipofarika Diwani wao, Salum Msika, Mei 29, 2013.
Kiti cha Diwani wa Kata ya Kibaoni kipo wazi kwa miezi tisa sasa tangu kifo cha Msika, huku wachumi na wadau wa mambo ya maendeleo wakilalamikia kwamba, Shughuli za Maendeleo ndani ya Kata hiyo zitadorola kwa kukosa Diwani wa kuzisukuma kwa ukaribu zaidi.
Tanzania Daima ilimpigia Mkurugenzi Mbilinyi Simu 0786 091342 ili aelezee kwa nini Kata hiyo haikuorodheshwa katika Kata 27 zilizofanya Uchaguzi 16.2.2014, wakati ilikuwa na sifa za kuwemo, kutokana na aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo Msika kufariki tangu Mei 29, 2013.
Alipotafutwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA) Kata ya Kibaoni, Odrick Matimbwi, alisema, Ofisi yake na ya Wilaya, imemuulizia Mkurugenzi Mbilinyi dhidi ya kucheleweshwa kwa Uchaguzi huo, lakini hakuna majibu ya maana ambayo amekuwa akitoa, zaidi ya wananchi kuendelea kukosa mwakilishi wa kuwatumikia
Aidha katika hali isiyo ya kawaida CHADEMA Kibaoni, kimedai kubaini Tuhuma na Njama zinazofanywa na Vijana wa ‘Green Guard’ wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Kata hiyo, wanaoandaa Mafunzo kwa nia ya kukusudia kukihujumu Chadema Kata ya Kibaoni katika Uchaguzi ujao wa Diwani wao utakapotangazwa.
“Tunazo Habari zinazovuja toka kwenye Vikao vyao vya siri wanavyofanya wilayani na hapa kwenye Kata, zinavuja na tunazipata, lakini Chadema hatuwezi kukaa kimya na kupuuzia hatua hiyo, ila tutaifanyia kazi kwa karibu na tutauarifu uongozi wa chadema Taifa”.alisema Matimbwi.
Hata hivyo kwa upande wa wadau wa siasa wilayani Kilombero na wananchi wa Kata hiyo, wamelitonya Tanzania Daima wakidai, Viongozi wa Serikali na wale wa Wilaya, huenda wanahofia hali tete ya upepo wa kisiasa, ambapo upinzani upo juu zaidi katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment