CHADEMA JIMBO LA CHALINZE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
6 MACHI, 2014
Chama cha
Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Chalinze kimeanza mchakato wa ndani
wa kupata mgombea ubunge kwa ajili ya uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika
mapema mwezi Aprili, mwaka huu, ambapo fomu za uteuzi zimeanza kutolewa kwenye
Ofisi Jimbo, kuanzia tarehe 4 Machi na mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu
hizo itakuwa tarehe 7 Machi 2014, saa 10.00, jioni.
Kura za maoni
ndani ya chama, zitafanyika tarehe 8 Machi katika Mji wa Chalinze na kufuatiwa
na kikao cha kamati ya utendaji ya jimbo ili kufanya uteuzi wa awali kwa mujibu
wa Katiba ya chama na hatimaye kikao cha Kamati Kuu kufanya uteuzi wa mwisho
ili kupata mgombea atakayeshindana na wagombea wa vyama vingine.
Mpaka sasa
wagombea waliochukua fomu kwenye ofisi ya jimbo ni watatu (3) na wagombea
wengine watatu (3) wamechukulia fomu Ofisi za Makao Makuu ya Chama, Dar es
Salaam, hivyo hadi sasa idadi ya wagombea waliotambuliwa rasmi ni sita.
Tunatumia
nafasi hii kuujulisha umma wa Watanzania, hususan wanachama wa CHADEMA, kuwa
fomu za kuwania uteuzi wa ndani zinaendelea kupatikana sehemu tatu, Makao Makuu
ya Chama, Ofisi ya Jimbo la Chalinze na kwenye tovuti ya chama
www.chadema.or.tz
Imetolewa
Machi 5, 2014
Iddi Omary
Ucheche
Katibu wa
CHADEMA, Jimbo la Chalinze
0756 639014
No comments:
Post a Comment