Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, March 16, 2014

Karata ya Sita Urais 2015 CCM, Njia Nyeupee…..!

Na Bryceson Mathias

KARATA ya Urais 2015, Njia ni Nyeupe kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta, iwapo ataendeleza kufanya kazi kwa Viwango vipya vya kujali maslahi ya watanzania katika kuongoza Bunge Maalum la Katiba.

Ushindi alioupata Sita katika kinyang’anyiro cha kumpata Mwenyekiti wa Kudumu wa kuongoza Bunge hilo, ni Ishara tosha ya kuwawashia taa (Indicator) Mahasimu wenzake katika Chama chake cha Mapinduzi (CCM) waliodaiwa kuanza Kampeni mapema wakapigwa Stop!.

Makada wa CCM ambao pia wanadaiwa kuwania Karata hiyo pamoja na, William Ngeleja, Edward Lowassa, Stephen Wassira, Bernard Membe, Januari Makamba, akiwemo na Sita ambapo wadau wa duru za kisiasa wanasema, Nyota ya Sita, sasa inaonekana kuwaka zaidi.

Turufu ya Sita kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, imemuonesha kuwa kana kwamba amelamba Dume la kisiasa, ambapo akifanikiwa kukonga nyoyo za watanzania katika uboreshaji wa Katiba nzuri itakayokidhi matakwa ya watanzania, hana kipangamizi kuiwakilisha CCM Urais 2015.

Upepo na Sifa zitakazompelekea Sita kwenye mafanikio ya nchi ya Ahadi [Promise Land] kisiasa, zinatokana na jinsi alivyoongoza Bunge la Tisa, lililoibua Ufisadi mkubwa kiasi cha kuwagusa, kuwahusisha na kuwatia doa hata baadhi ya wanaharakati wenzake wa Urais 2015.

Mizoga Mingi ikiwemo ya Richmond, EPA, Meremeta na mingi mingine iliyokuwa ikiiharufisha Tanzania kikiwemo Chama Tawala, Serikali na Wananchi wake ilibainika, lakini kutokana na Sintofahamu iliyotokea, Sita alienguliwa kimizengwe katika Bunge la 10, Ufisadi ukawa hai kiainia.

Wananchi na watu wenye mapenzi mema na Tanzania, waliumizwa sana na tukio la kumshika Sita shati aslielekeze Bunge kuwa lenye kiwango cha Wabunge wanaowajibika na kuwatumikia wananchi wao bila woga, hivyo wakabakizwa katika uoga wakihofia vyeo vyao kuguswa.

Kuchaguliwa kwa Sita, kunaondoa upya Mawingu yaliyoifunika Nyota na Mwenzi wa Ndoto zake, kuona kwamba watanzania wanaiendea Tanzania yenye mustakabali wa kufaidi rasilimali ilizonazo, pasina kuwaachia Mafisadi watambe, huku walalahoi wakishindia Mlo mmoja kwa siku.

Pamoja na kwamba waswahili wanasema, yaliyopita si ndwele tugange yajayo, nina uhakika Sita hatafanya Mzaha wa kushusha Kiwango chake cha utendaji uliotukuka katika Bunge la Tisa, na badala yake atafanya vizuri zaidi huku akijua ana Mtaji kwa mustakabali wa watanzania na kitu Fulani 2015.

Sita Ni Muumini Mzuri wa Haki na Uchaji mbele za Mungu wake ambaye kila mara amekuwa akimtaja katika hotuba zake, hivyo sitegemei kama ataamua kumsaliti kama Yuda Isikariote alivyomsaliti Yesu. Ni rai yangu asiwasaliti watanzania kuwapa Katiba Safi inayokidhi Demokrasia ya kweli.

Ni rai yangu kwa Sita atambue kuwa wajibu wake katika Bunge Maalum la Katiba si kwa Chama chake cha CCM bali upo kwa Watanzania wengi walalahoi ambao hawana EPA au, Richmond, na wengine ndio hao ambao sasa wanashindwa hata kununua Umeme wa LUKU.

Sita Mungu anasema hivi, “ Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima. Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu; Bali yeye aiogopaye amri atapewa thawabu. Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti

 “Ufahamu mwema huleta upendeleo; Bali njia ya haini huparuza.  Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa; Bali mpumbavu hueneza upumbavu”. Mithali 13:12-16.

Siata; Watanzania walikutarajia sana uongoze Bunge Maalum la Katiba, hata walipoona watu wanaomba Posho, Wanapigana Vijembe, na kufanya Vituko bungeni Kodi yao ikiliwa, walikuwa wanaugua sana, hivyo naomba usikubali vijembe ila mustakabali wa Tanzania na Si Mafisadi.

No comments: