Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, March 16, 2014

CHADEMA: Polisi sio Chanzo cha Mapato!

Na Bryceson Mathias

WAKATI Polisi na Vyama vya CCM na Chadema kinawaka Kalenga, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa Kambi ya Upinzani bungeni, Vicent Nyerere, amelikoromea Jeshi la Polisi nchini aksema, ‘Wao sio Chanzo cha kukusanya Mapato’.

Kauli ya Nyerere inafuatia kuwepo kwa madai ya Malalamiko ya chini kwa chini ya Askari wa Usalama barabarani Dodoma, kuwa wanaagizwa kila Askari anatakiwa kukamata Makosa 90 tofauti na 15 yaliyoainishwa awali katika ufanisi na utendaji wao.

Katika hali isiyo ya kawaida, kumedaiwa kuwepo Malalamiko hayo kwa baadhi ya Askari ya Askari (Traffic) hao wa Dodoma, wakidai wanashikizwa na Viongozi wao kukamata Makosa 90 na wahusika kupigwa faini, huku Nyerere akipinga Polisi si chanzo cha Mapato.
Kwa Njia ya SMS ya simu yake Nyerere alisema kuwa, “Polisi sio chanzo cha mapato  cha nchi, wanakosea kuwa hivyo kikubwa ni ni Elimu”.alisema Nyerere.

Awali ilidaiwa, Miongoni mwa Viongozi wa Vitengo wa Usalama Barabarani mkoani humo, walilalamika wakidai, kwa sasa wananchi wanateseka kwa kukamuliwa kipato chao kiduchu kutokana na kukamatwa na kupigwa faini ovyo, Baiskeli SH. 20,000/- na Magari 30,000/-.

Kama Askari wa usalama barabarani Dodoma wakiwa 89, kwa Makosa 90 ambayo kimsingi ni vigumu labda uwabambikize na kuwakamata wasio na makosa, kwa faini ya SH.30,000/- zitakusanywa SH. 240,300,000/- na SH.20,000/- zitakusanywa SH.160,200,000/-.
“Hatuwezi kuwakamu wananchi namna hiyo wakati maisha yao ni magumu, na kidogo walicho nacho kinawasaidia kusomesha na kuwalisha watoto”. alisema Askari wa Kike aliyesema yupo tayari kuacha kitengo, kutokana na kauli za kuambiwa wasipotimiza malengo hayo wajitoe.

Uchunguzi uliofanywa, kuna Baiskeli Nyingii, Pikipiki na Magari katika eneo la Polisi Dodoma, ambapo viongozi wakihojiwa mara nyingi wanaombwa wasitajwe, ila wanadai hiyo ni Amri toka Ngazi za Juu, hata hivyo inasemekana inawatesa wananchi, huku wao wakiilalamikia Serikali kuu.

1 comment:

Anonymous said...

Inaumiza sana hasa mkoa wa pwani ni lazma makosa yafike 60