Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, March 8, 2014

CCM walivyomchoma kisu mtoto wa Kiongozi wa serikali aliyejiunga na CHADEMA Kalenga

Ni Green Guard  vijana wa CCM waliomchoma kisu mtoto wa Kiongozi wa serikali aliyejiunga na CHADEMA Kalenga

This is very serious, na kama ccm wamefikia hatua ya kufanya unyama wa namna hii basi ni dhahiri wameshindwa kufanya ushawishi kwa wapiga kura jukwaani, badala yake wamebaki na mbinu hii mbaya isiyokubalika mbele ya jamii, mbinu za kuteka, kutesa na kuua raia.

Kama mtakumbuka kulikuwa na taarifa za kiongozi wa baraza la vijana wa CHADEMA kuchomwa kisu usiku wa kuamkia leo na green guards wa ccm baada ya kile wanachokidai kuwa wamekosa uungwaji mkono wa wanaKalenga baada ya CHADEMA kuvuta hisia za watu, na kwamba yule kijana ambaye mama yake mzazi ni kiongozi wa serikali ya kijiji ameweza kuwashawishi wapiga kura wa kata yake kuiunga mkono chadema.

Haikuishia hapo tu, Mama mzazi wa kiongozi wa bavicha aliyechomwa kisu alikuwa amejiunga chadema jana, ambapo baada ya masaa machache kujiunga na timu ya ukombozi ya chadema, mtoto wake alitekwa na green guards sita na kuchomwa kisu karibu kabisa na kwenye moyo.

Nisiwachoshe msinichoshe, someni habari kutoka kwa kamanda wetu aliye uwanja wa ukombozi Kalenga, na picha ya mama aliyejiunga na chadema pamoja na mtoto wake ambaye ni kiongozi wa bavicha aliyechomwa kisu na makada wa ccm.


 Juu na chini ni kijana Richard Mawata aliyechomwa kisu na green guards wa CCM akiendelea na matibabu

Kiongozi wa serikali ya kijiji akipokea kadi ya chadema, ni mama ambaye ni mama mzazi wa kijana aliyechomwa kisu na green guards wa ccm Kalenga.

Kijana yaani Katibu wa Bavicha aliyechomwa jana Richard Mawata ni Mtoto wa sita wa kuzaa kbs wa huyo Mama Mwenda aliyejiunga na CHADEMA jana hiyo hiyo mchana. Yaani mama (of course kawaumiza sana CCM kwa sbb ni influencial maeneo hayo) kajiunga na CHADEMA mchana, usiku mwanae akachomwa kisu na watu wa CCM. Baada ya kufanya nae interview militia maelekezo kwa uongozi wa hospitali na kamanda mwenyewe, asifanye interview na mtu mwingine yeyote bali apumzike maana intelijensia ilitonywa mapema kuwa CCM wanapeleka waandishi wao kwenda kubadili story.

Cha kutia moyo ni kwamba kamanda yuko imara sana. Wamedhuru mwili lakini moyo u imara. Mapambano haya ni imani, moyo kabla ya silaha.

Mama naye yuko imara mbaya. Anasema mwanae atapona tu na mapambano yanasonga mbele. Harudi nyuma...maana anajua wakati ni huu.

Kwa mujibu wa RPC hadi sasa wamekamatwa watu wanne wale wale ambao Kamanda aliwaona kwa sura na anawafahamu kwa majina.

Walimvizia mahali akitoka kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba kuhamasisha watu kumchagua mbunge mtarajiwa na kuhudhuria mkutano wa chopa leo Luhota.

Wakamvizia wakati anakwenda home mahali ambapo hakuna watu wala nyumba hivi akiwa na baiskeli yake wakasimama mbele yake kuziba njia watu kama sita hivi, alipofika tu wakamshambulia na kumchoma kisu. Alilazimika kupata msaada wa wasamaria wema pamoja na viongozi wa Chadema waliowahi kufika eneo la tukio kwenda hospitali.

Kwa mujibu wa muuguzi Kamanda atapona ingawa ukweli ni kwamba kisu kilikosa kdg tu kufika moyoni. Sasa hivi tungekuwa tunasema habari zingine.

Source: Recipient/JF

No comments: