Na Bryceson Mathias
HIVI aribu karibuni wajumbe 629 wa Bunge Maalumu la Katiba. Wamejiweka kitanzi na kuagana na Mungu kutenda haki watakapopitia na kuiboresha Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba.
Nasema wamejifunga Kitanzi kwa sababu wamefanya Agano naye Agano la Utii kwake na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama lilivyokuwa Agano la Mwanaye Yesu Kristo kuwa, la kumpendeza Mungu na Watu. Je Wabunge wa Katiba watalitimiza agizo hilo?
Lakini Yesu alilitimiza Agizo! Biblia inasema, “Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake. Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu Luka 2:40, 50.
Mwishoni mwa wiki; Niliwasikia Wabunge wa Bunge Maalum mjengoni kwa majina yao, wakimwomba Mungu kwa majigambo wakitaka awasaidie kupitia vitabu vyake vitakatifu vya Biblia na Kurani, na hiki ndicho kiapo chao;-
“MIMI… [Jina la Mjumbe]…niliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge Maalumu, naapa/ nathibitisha kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kadiri ya uwezo na ufahamu wangu, nitatimiza wajibu wangu na kufanya kazi zinazonihusu bila ya upendeleo, na bila kukiuka sheria za nchi. Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.”
Sasa ninavyomfahamu Mungu na jinsi ambavyo wengi wetu husema sauti Wengi ni ya Mungu, hata kama humo ndani ya uteuzi kulikuwa na Mkono wa Mtu kupendelea Chama au Asasi na Taasisi yake, mradi Mungu ameombwa asaidie, uharifu ule unatakaswa na anakuita yeye kufaya kazi yake kwa ajili ya watu si Jakaya Kikwete.
Baada ya Toba ile iliyofanywa kwa Biblia na kumtaja, anaingilia kati na kutoa Wito wake huu,
“Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, …[Jina la Mjumbe]…….. ..yeye aliyekuumba, Ee Israeli,….[… …[Jina la Mjumbe]…….. asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
“Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza”. Isaya 43:1-2 unaitwa hivyo Mungu si Kikwete tena ili uitende kazi yake kwa ajili ya watanzania ambao ni watu wake.
Sasa ikifika mahali mtu aliyeitwa kwa wito huo wa Mungu baada ya kufutwa wito wa Kikwete, ambao pengine ndani yake tunasema kulikuwa na Hati ya Mashitaka na Hukumu….yaani…
“Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;
Akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo” Kolosai 2:14-15 halafu anatokea mtu anafanya madudu humo bungeni, Kitakuwa kilio na watu wanaweza wakaehuka, wakapoteza viungo au kufa, maana ataona amedharauliwa.
Biblia inasema hivi, “Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake”. Kitabu cha Kwanza cha Wafalme 2:10.
Hivyo nawasihi sana Wabunge wa Bunge Maalum wasijaribu kumuuthi Mungu ili hali wamemuomba kwa vitabu vyake na kukiri kuwa watatenda haki halafu wakakiuka, maana Ushahidi wa hati ya Mashitaka na Hukumu yenu ni ukiri kupitia vitabu hivyo.
Kwa nyakati fulani tumeshuhudia Viongozi wa Siasa katika Vyama na Serikali, wamekuwa wakiapa na wakikiri kwa kiapo hicho, lakini baada wanapoenda kuwatumikia wananchi wamekuwa wanafaanya tofauti na tukaona walivyofanywa!.
Wengine wamepoteza Maisha, Viungo, Nyadhifa zao, Familia zao, kwa Ajali na Ulemavu mbalimbali na kudhani ni Mikosi kumbe wamesahau, katika kiapo walichomuapia Mungu kufanya, na wamekikiuka.
Humo bungeni mnao wachungaji na waombaji, na huku nje wako waombaji ambao wengine wanafunga na kuomba hadi mwisho wa Bunge hilo, hivyo ni rai yangu msithubutu kuleta utoto kama ule wa Posho na mMengine ya kuchelewsha Muda. Kwaherini
No comments:
Post a Comment