MWENYEKITI
wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amesema
kuwa chama cha siasa, taasisi, asasi yoyote ya kiraia kuweka msimamo wake
kwenye hatua ya sasa ya mchakato wa katiba mpya ni jambo lisilokubalika kwa
sababu linakwenda kinyume na maoni ya wananchi.
Amesema
kuwa wakati wa vyama vya siasa au makundi mengine katika jamii kuwa na misimamo
yake kwenye suala la katiba mpya ulishapita, ambapo kila chama au taasisi
iliwasilisha maoni yake kwenye hatua ya awali mbele ya Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, chini ya Jaji Joseph Warioba.
Akizungumza katika
maeneo mbalimbali ya Jimbo la Kalenga kwenye mikutano ya kampeni za uchaguzi
mdogo jimboni humo, akimnadi mgombea wa CHADEMA, Grace Tendega, Heche
aliwaambia wananchi kuwa kitendo cha CCM kuandika waraka, kikiweka msimamo wa
chama hicho dhidi ya rasimu ya pili ya katiba mpya, ni dalili ya wazi kuwa
hakina dhamira ya njema katika mchakato huo nyeti.
Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment