WARAKA NAMBA 3
CHAMA CHA MAPINDUZI
KIKAO CHA HALMASHAURI
KUU YA TAIFA
WARAKA
KUTOKA IDARA YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA
TAARIFA
KUHUSU RASIMU YA PILI YA KATIBA
Dodoma
Februari, 2014
|
UTANGULIZI
Mnamo tarehe 03/06/2013 Tume ya Mabadiliko ya Katiba
ilitangaza Rasimu ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
hivyo kuwapa fursa wananchi kutoa maoni yao kupitia Mabaraza ya Katiba ya
Wilaya na Mabaraza ya Taasisi.
Kati ya mwezi Juni na Agosti 2013 Chama Cha Mapinduzi
kilijiunda kama Baraza la Katiba la Kitaasisi kupitia mikutano ya wanachama na
viongozi kuanzia ngazi ya matawi hadi taifa. Maoni ya mabaraza haya ndiyo
yaliyokuwa msingi wa mapendekezo yaliyowasilishwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Tarehe 30/12/2013 Tume ya Mabadiliko ya Katiba
ilitangaza Rasimu ya Pili ya Katiba ambayo itawasilishwa katika Bunge la Katiba
ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kupata Katiba mpya.
Nia ya waraka huu ni kufanya uchambuzi utakaosaidia
kupata uelewa wa pamoja wa Rasimu ya Pili na kutoa fursa ya kujipanga vizuri
kwa hatua zinazofuata katika mchakato wa kuunda Katiba mpya. Kwa mantiki hii
waraka huu unabainisha yafuatayo:
·
Maeneo ambayo mapendekezo
ya CCM yaliyotolewa
katika Rasimu ya Kwanza yamezingatiwa moja kwa moja;
·
Maeneo ambayo hayakuzingatiwa moja kwa moja, lakini yamezingatiwa kwa
namna ambayo inakidhi mapendekezo yaliyotolewa na CCM;
· Mambo
mapya yaliyoingizwa kwenye Rasimu ya Pili;
· Uchambuzi
wa Rasimu na mapendekezo.
Taarifa hii ina sehemu tatu. Sehemu ya Kwanza
inaainisha jinsi mapendekezo ya CCM
yalivyopokelewa na Tume kama
ilivyotajwa hapo juu.
Sehemu ya Pili itabainisha changamoto za muundo
unaopendekezwa (kisheria; gharama; kitaasisi, kwa mtazamo wa kujenga umoja wa
taifa letu). Sehemu ya Tatu ina majumuisho na mapendekezo ya kurekebisha mfumo
uliopo kwa kuzingatia
changamoto zilizotajwa na haja ya kuuimarisha Muungano.
SEHEMU YA KWANZA
MAPENDEKEZO YA CCM
YALIVYOPOKELEWA NA TUME
1. MAPENDEKEZO
YALIYOZINGATIWA MOJA KWA MOJA
Ibara ya 9(3)
Ilipendekezwa ibara hii iondolewe kwa kuwa inazungumzia
Serikali ya Muungano
kuweka Katiba kwenye mitaala ya elimu, ilhali elimu si
mojawapo ya mambo ya
Muungano.
Pendekezo
hili limezingatiwa kwa kuondoa ibara hii.
Ibara
ya 22(3)
Ibara hii ambayo ilikuwa ibara ya 21(3) ya Rasimu ya
Kwanza ilihusu kuweka
ukomo kwa wastaafu wanaopokea pensheni ya umma kushika
nafasi za uenyekiti
au
ukurugenzi katika mashirika ya umma.
CCM ilipendekeza
ibara hii irekebishwe ili wastaafu
waruhusiwe kuendelea
kutumia ujuzi wao katika nafasi watakazokuwa wamepewa kwa
kuzingatia vigezo na uwezo wao wa kumudu majukumu hayo.
Pendekezo
hili limezingatiwa na ibara hiyo ya 21(3) imeondolewa.
Ibara
ya 26(2)
Hii ilikuwa ibara ya 25(2) katika Rasimu ya Kwanza. CCM ilipendekeza ibara hii ifafanuliwe ili
kubainisha kuwa ni
usafirishaji haramu wa
binadamu ndiyo
unaopigwa
marufuku.
Pendekezo
hili limezingatiwa kwa kueleza katika ibara ya 26(2)
kuwa ni biashara haramu ya kusafirisha na kuuza binadamu.
Ibara
ya 32
Hii likuwa Ibara ya 31ya Rasimu ya Kwanza.CCM ilipendekeza
ibara hii iimarishwe
kwa
kuandikwa upya ill itamke bayana kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano haina
dini; Iakini watu wake wana uhuru wa kuabudu.
Pendekezo hili limezingatiwa kwa Ibara 1(1) ya Rasimu ya
pili kutamka kuwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni Shirikisho lisilofungamana
na dini. Kadhalika,ibara ya 32(3) ya Rasimu inasema
shughuli za uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya
serikali. ·
Ibara ya 47(1)
Hii ilikuwa ibara
ya 46(l)(d) katika
Rasimu ya Kwanza
na ilihusu haki ya
mwanamke kupata ujira sawa na mwanaume. Ilipendekezwa irekebishwe ili haki
hiyo ihusu kupata ujira sawa kwa kazi zenye sifa
inayofanana.
2
Pendekezo
hili limezingatiwa kwa Rasimu ya Pili kueleza katika ibara ya 47(1)(d) kuwa
kila mwanamke ana haki ya kupata fursa
na ujira sawa na mwanaume katika kazi zenye sifa zinazofanana.
Ibara y.a 79
Hii ilikuwa ibara ya 75 katika Rasimu ya Kwanza na
ilihusu sifa za mtu anayetaka kugambea urais. CCM ilipendekeza wazazi wote
wawili wawe raia wa kuzaliwa.
Pendekezo hili limezingatiwa kwa kueleza katika ibara
ya 79(c) ya Rasimu ya Pili kuwa wazazi wote wawili wa mgombea wawe ni raia wa
kuzaliwa.
Ibara ya 80
Hii ilikuwa ibara ya 77 katika Rasimu
ya K anza. Ibara hii ilihusu kiwango cha ushindi kwa mgombea
urais. CCM ilipendekeza
kwamba mgombea wa
urais atangazwe kuwa mshindi iwapo ntapata zaidi ya asilimia hamsini ya
kura zote halali zilizopigwa.
Pendekezo
limezingatiwa kwa_kueleza kuwa mshindi ni yule aliyepata asilimia hamsini ya kura
halali zilizopigwa.
Ibara ya 83
Katika Rasimu ya Kwanza hii
ilikuwa ibara ya 76 na ilihusu haki ya mtu kuchaguliwa kuwa Rais na ukomo wake.
Ibara ndogo ya (4) ya ibara hii ilikuwa na mkanganyiko kuhusu uwezekano wa
Makamu wa Rais aliyeko madarakani
kugombea urais endapo Rais ameshindwa kutekeleza. majukumu yake. Ibara hii
haikueleweka vizuri kama Makamu huyu angeweza kuchaguliwa kwa
kipindi kimoja tu au viwili kuwa Rais kwa kuzingatia muda ambao alikuwa
akitumikia nafasi ya Makamu wa Rais. CCM ilipendekeza ibara hii ifafanuliwe
vizuri kwani ilikuwa inakinzana na ibara nyingine zilizohusu nafasi ya Makamu
wa Rais. '
Pendekezo limezingatiwa ambapo Rasimu ya Pili katika
ibara ya 83(4) imefafanua kuwa endapo Makamu wa Rais atashika nafasi ya
madaraka ya Rais pale ambapo nafasi ya Rais iko wazi kwa kipindi kisichozidi
miaka mitatu, ataruhusiwa kugombea nafasi ya Urais kwa vipindi viwili, lakini
kama atashika madaraka ya nafasi ya Rais kwa kipindi cha miaka mitatu au zaidi
ataruhusiwa kugombea madaraka ya Rais kwa kipindi kimoja tu.
Ibara
ya 90
Katika
Rasimu ya Kwanza hii ilikuwa ibara ya 86(2) kuhusu Makamu wa Rais. Pendekezo la
CCM lilihusu matumizi mazuri ya Kiswahili kwamba maneno Makamu atakuwa na
jukumu la "kusababisha utekelezaji" yasomeke '"atawezesha au
atasimamia utekelezaji".
Pendekezo
limezingatiwa kwa kufafanua katika ibara ya 90(2) kuwa Makamu wa Rais
atatekeleza au atasimamia utekelezaji wa jambo lolote...
3
Ibara
ya 125
Katika Rasimu
ya Kwanza hii
ilikuwa ibara ya
117(1)(a), inahusu sifa za
kuchaguliwa
kuwa Mbunge. CCM il!pendekezwa umri uwe miaka 21 badala ya 25.
Pendekezo
hili limezingatiwa katika ibara ya 125(1)(a) kuwa mgombea ubunge aliyefikisha
umri wa miaka ishirini na moja anaweza kugombea ubunge.
Ibara
ya 128
Katika Rasimu ya Kwanza hii
ilikuwa ibara ya 123 na ilihusu mbunge kutopoteza ubunge wake iwapo atafukuzwa
na Chama chake, isipokuwa kama amejitoa
mwenyewe. CCM ilipendekeza mbunge apoteze ubunge iwapo atafukuzwa au kwa hiari
yake atajivua uanachama, na kwamba kigezo cha kupoteza ubunge kiwe ni uanachama
na si namna mbunge alivyotoka kwenye chama chake.
Pendekezo
limezingatiwa ambapo kwa mujibu wa ibara ya 128(1)(g) Mbunge atapoteza ubunge
iwapo kwa ridhaa yake atajitoa au kujivua uanachama wa chama chake cha siasa,
atafukuzwa au kuvuliwa uanachama wa chama chake cha siasa.
Ibaraya
133
Katika Rasimu
ya Kwanza hii
ilikuwa ibara 129 ycnye
maelezo ya pembeni
yaliyosomeka
“ukomo wa mamlaka ya Bunge" huku maudhui yake yakihusu ukomo
wa Spika.
CCM ilipendekeza maelezo ya pembeni (marginal notes) ya ibara hii yasomeke
"ukomo wa mamlaka ya Spika". Ibara ya 129(1)(d) ilisema Spika
atapoteza nafasi yake endapo atashindwa kuwasilisha "tamko rasmi" kwa
Rais. CCM ilipendekeza utolewe ufafanuzi hili nitamko gani.
Mapendekczo
ya kubadilisha maneno ya pembeni na ufafanuzi wa tamko rasmi yamczingatiwa
ambapo imefafanuliwa katika ibara 133(1)(d) kuwa ni, tamko rasmi kuhusiana na
mali na madeni yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
Ibaraya
190
Katika
Rasimu ya Kwanza hii ilikuwa ibara ya 181 iliyokuwa inaunda Tume Huru
ya
Uchaguzi. Katika ibara ndogo ya (1) Rasimu iliipa Tume jukumu la kusimamia na
kuratibu shughuli za vyama vya siasa. CCM ilipendekeza masuala haya yasiwe
sehemu ya majukumu ya Tume.
Pendekezo limezingatiwa na jukumu
la kuratibu na kusimamia shughuli za vyama vya siasa amepewa Msajili wa Vyama
vya Siasa ambaye ofisi yake sasa hivi inapendekezwa kuwa taasisi huru.
Ibara
ya 219
Katika
Rasimu ya Kwanza hii ilikuwa ibara ya 204, ilihusu kuondolewa madarakani
kwa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. CCM i!ipendekeza ibara ya 204
iboreshwe kwa kipengele kinachohusu
utaratibu wa kumwondoa
4
kazini
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Ser:ikali kama ilivyo katika ibara ya 114(1)-(7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ya mwaka1977.
Pendekezo limezingaliwa
ambapo katika ibara
ya 219 vimeongezwa
vipengele vinavyoelezea namna na
utaratibu ambao Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ataweza kuondolewa
kazini pale itakapobidi.
Mpangilio
wa namba za ibara
Katika
Rasimu ya Kwanza kulikuwa na ibara ya 229 na ya 231. CCM ilipendekeza
mpangilio
wa namba za ibara urekebishwe iii kuondoa kasoro ya kutokuwepo ibara ya 230.
Pendekezo limezingatiwa
kwa namba za
ibara kurekebishwa kwa kuhakikisha
mpangilio wa namba za ibara unafuata utaratibu.
Ibaraya
243
Katika
Rasimu ya Kwanza hii ilikuwa ibara ya
232, ambayo pamoja na ibara ya 227
zinahusu
kuundwa kwa Jeshi la Polisi la Jamhuri
ya Muungano, ibara 232(1)
inaruhusu
nchi washirika kuunda vikosi vya Polisi.
CCM ilip.endekeza_ibara hii
iondolewe kwa nia ya kuepuka
mgongano wa kiutendaji na kiusalama.
Pendekezo limezingatiwa ambapo
kipengele cha 232(1) kinachohusu polisi wa nchi washirika kimeondolewa.
Ibara
ya 248
Katika
Rasimu ya Kwanza hii ilikuwa ibara ya 235 na ilihusu usalama wa Taifa
ambapo
ibara.ya 235 ilihusu nchi washirika kuanzisha idara zao za usalama. CCM
ilipendekeza
ibara hii iondolewe ili kuepuka
mgongano wa kiutendaji na wa kiusalama.
Pendekezo limezingatiwa ambapo
kipengele cha 243(1)
kinachohusu kila nchi mshirika kuanzisha taasisi yake ya usalama wa Taifa
kimeondolewa.
2.
MAMBO AMBAYO YAMEZINGATIWA KWA
NAMNA INAYOKIDHI
MAPENDEKEZO
YA CCM
Ibara
ya 32
Hii
ilikuwa ibara ya 31 iliyohusu uhuru wa imani ya dini. CCM ilipendekeza kwamba ibara
hii iandikwe upya kwa kutamka bayana kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano
haina dini lakini watu wake wana uhuru wa kuabudu.
Pendekezo hili limezingatiwa katika ibara 1(1) ya
Rasimu ya pili iliyotamka
Kuwa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania ni Shirikisho lisilofungamana na
dini.
Kadhalika ibara ya 32(3) ya
Rasimu inasema shughuli za uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya
shughuli za mamlaka ya serikali.
5
lbaraya56
Ibara hii inahusu uraia na katika Rasimu ya Kwanza maudhui
yake yalikuwa katika
ibara za 54 hadi 56. CCM ilipendekeza
kuweko uraia a nchi mbili.
Pendekezo hili limezingatiwa
katika ibara ya 59 ya Rasimu ya Pili kwa kutoa
hadhi maalum kwa watu walioacha uraia
wa Tanzania lakitti wana asili au
nasaba ya Tanzania.
lbaraya 97
Maudhui ya ibara
hii yamo katika
ibara ya 92 ya
Rasimu ya Kwanza CCM
ilipendekeza
ibara ya 92(1) itaje kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye Mwenyekiti wa Baraza
la Mawaziri kama ilivyo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977.
Pendekezo hili limezingatiwa kwa ibara ya 72(3)(a) na
97(2) kutaja kwamba Rais ataongoza mikutano ya Baraza la Mawaziri.
lbaraya125
Hii ilikuwa
ibara ya 117 ya Rasimu ya Kwnnza. CCM ilipendekeza marekebisho ili mtu
aliyetiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai asiwe na sifa ya kugombea Ubunge.
Pendekezo limezingatiwa ambapo kwa mujibu wa ibara ya
(125)(2)(c) mtu aliyehukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita kwa kosa lolote
anakosa sifa ya kugombea.ubunge.
Ibara 137
Katika Rasimu ya Kwanza hii
ilikuwa ibara ya 133 na ililmsu uteuzi wa Katibu wa
Bunge kufanywa na Tume ya
Utumishi ya Bunge. CCM ilikuwa na maoni kwamba Tume ya Utumishi ya Bunge ndiyo
ipendekeze majina matatu kwa Rais ambaye atafanya uteuzi wa jina moja la Katibu
wa Bunge.
Pendekezo limezingatiwa katika ibara ya 137(1) ambapo
Katibu wa Bunge atapatikana kwa Tume ya Utumishi wa umma kupendekeza majina
matatu kwa Rais ambaye atateua jina moja.
3. MAMBO MAPYA
Kimsingi
na kimaudhui Rasimu ya Pili haitofautiani sana na rasimu ya Kwanza. Rasimu ya
Kwanza ilikuwa na sura 16 zenye ibara 239; Rasimu ya Pili ina sura 17 na ibara
271. Sura ya 17 haikuwepo, hivi sasa imeongezwa ili kubeba ibara zinazohusu
masuala ya mpito.
Ibara
ya 4(2) '
Ibara hii inaelekeza kuwa lugha ya Kiingereza au lugha
nyingine yoyote inaweza
kutumika kuwa lugha rasmi ya mawasiliano ya kiserikali pale
itakapohitajika.
6
Ibara hii inaleta utaratibu mpya wa
kurasimisha matumizl ya lugha mbalimbali katika mawasiliano ya kiserikali. Ikumbukwe
kwamba hivi sasa upo utaratibu wa tafsiri kutolewa pale inapobidi kwa mfano
mahakamani, kwa daktari na maeneo rnengine. Ingawaje ibara hii inapanua wigo wa
mawasiliano ni vema ikachukuliwa kwa
tahadhari ili isije
ikafifisha umoja wa
kitaifa uliojengwa na
lugha ya Kiswahili.
Ibara ya 49(1)(b)
Ibara
hii inaeleza kuwa kila raia ana wajibu wa kulinda na kuheshimu Tunu za Taifa.
Katika ibara ya 49(2) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajlli ya kuwawezesha
raia kutekeleza masharti ya ibara hii.
Ibara inaainisha jambo la msingi
kitaifa lakini si rahisi kuelewa ni katika mazingira gani raia anaweza
akawajibishwa kisheria kulinda na kuheshimu tunu za Taifa.
Ibaraya 113
Kwa
mujibu wa ibara hii Bunge la Muungano lifakuwa na Wabunge 50 toka Tanganyika,
20 toka Zanzibar na 5 kutoka kundi la watu wenye ulemavu watakaoteuliwa na
Rais. Kila jimbo litatoa wabunge wawili mwanamke na mwanaume. Tume Huru ya
Uchaguzi ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza majimbo ya uchaguzi.
Rasimu ya Kwanza ilitaja mikoa
kwa Tanzania Bara na wilaya kwa Zanzibar kama
majimbo ya uchaguzi. Hoja iliyojitokeza wakati
wa kutoa maoni kuhusu Rasimu hii ni uwezekano wa majimbo
kubadilika kwa kuwa tawala za mikoa si suala la Muungano. Rasimu ya pili
inaleta utata zaidi kwa
kutaja idadi ya wabunge na kuipa Tume Huru ya Uchaguzi mamlaka ya kugawa na
kutangaza majimbo ya uchaguzi. Wakati katika Rasimu ya Kwanza ilikuwa rahisi kujua kwamba mikoa au wilaya ingekuwa
kianzio cha kuunda majimbo, ibara hii ya
Rasimu ya Pili haitoi kiashiria chochote cha aina hiyo, kwakuwa nchi washirika
zitakuwa na mabunge yao na utaratibu wao wa kugawa rnajimbo ni vigumu kutabiri namna
Tume hii itakavyofanya kazi yake kwa murua
katika nchi washirika na Tume zake za uchaguzi.
Suraya17
Sura hii ni mpya. Inahusu mambo ya mpito ambayo yatashughulikiwa katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia
Aprili 2015 hadi 31 Desemba 2018.
Utaratibu wa kuwa na kipindi cha mpito ni wa kawaida
katika mabadiliko ya aina hii. Rasimu inaleta mapendekezo makubwa mno ambayo
yatabadilisha kabisa sura ya taifa letu. Muda wa mpito ni mfupi sana, kwani ni katika kipindi hicho baadhi ya
7
mabadiliko yatokanayo na
muundo wa serikali tatu yanatakiwa yawe yamekamilika. Kwa mfano:
· Katiba
ya Tanganyika kuundwa;
· Katiba
ya Zanzibar kubadilishwa ili iakisi mapendekezo ya mundo wa serikali tatu;
· Kugawana
raslimali na madeni kati ya serikuli ya Muungano, Zanzibar na Tanganyika;
· Kutunga
na kurekebisha sheria mbali mbali za nchi washirika ili kuwiana na Katiba mpya;
·
Mgawanyo wa watumishi wa umma;
·
Kuundwa kwa Tume na taasisi za kikatiba zilizoainishwa kwenye Rasimu.
Mambo yanayoelezwa katika
sura hii pamoja na kulenga kipindi cha mpito, yanaonesha kwamba hata gharama za
muundo huu hazitabiriki. Vile vile katika kipindi hicho cha.mpito kuna hatari
ya mipango mingi ya.kushughulikia matatizo ya wananchi kusimama.
4. MAPENDEKEZO, AMBAYO HAYAKUZINGATIWA NA, AMBAYO
BADO YANAHITAJI KUTAZAMWA UPYA
Katika Rasimu ya Kwanza
CCM ilizitolea mapendekezo lbara kadhaa
arnbazo tuliona ni vema zikaangaliwa kwa madhumuni yafuatayo:
·
Kupata mtiririko mzuri wa maudhui ya Katiba ili iwe nyepesi kueleweka. Hili lilikuwa
rnuhimu kama sehemu ya kuifanya iwe kweli Katiba ya wananchi
kwa ufasaha na matumizi yake. Kwa mfano:
·
Ibara za 52; 53, 54 na 55 ambazo zilikuwa ibara za 50, 51, 52 na 53 mtawalia
katika Rasimu ya Kwanza zina vipengele vingi vinavyohusu haki ya binadamu.
Ilipendekezwa ibara hizi zifupishwe na zirudishwe katika Suraa ya Nne ya Rasimu
inayohusu Haki za Binadamu. Pendekezo hili halijazingatiwa. Lengo ni kuwa na
mtiririko mzuri wa vifungu vya Katiba ili mambo yanayofanana yakae sehemu moja.
· Katiba ni sheria kuu na
utamaduni unaozingatiwa duniani kote ni kuifanya iwe rahisi kueleweka lakini ni
vigumu kuibadilisha. Rasimu hii kama ilivyokuwa Rasimu ya Kwanza imebeba mambo
mengi mno na yanayokwenda kwa kina mno kwa sheria kuu. CCM inaamini bado ipo
haja kwa Rasimu ya
Tatu kuzingatia suala
hili ili yale
ambayo yanaweza kutungiwa sheria, ifanyike hivyo. Sheria za kawaida ni rahisi
zaidi kuzifanyia marekebisho kuliko Katiba. Kwa
mfano:
8
Ibara ya 43 ambayo ilikuwa ibara ya 42 katika Rasirnu ya Kwanza. CCM ilipendekeza haki za mtato
zitajwe kimsingi katika Rasimu lakini zianishwe kwa ufasaha
katika Sheria ya
Mtoto. Pendekezo hili
halijazingatiwa. Ukweli ni kwamba haki za mtoto zinaweza kubadilika,
kuimarishwa au kuongezwa, jambo ambalo litafanyika kwa urahisi kwenye sheria ya
kawaida, tofauti na Katiba ambayo ina utaratibu
mrefu na mgumu
wa kuifanyia marekebisho. Hii pia
itaondoa wingi wa
ibara kwani kwa
asili yake Katiba ilipaswa
kubeba mambo makuu
na ya msingi
ili yawe dira katika sheria nyingine.
Mifano hii inaonesha kuwa mapendekezo ya CCM yalilenga
kuona kwamba Katiba inaweka misingi na ulinzi madhubuti wa jumla wa haki za
binadamu ili baadaye zifafanuliwe vizuri katika sheria mbalimbali za nchi. Hii itaepusha
kuweka mambo mengi mno kwenye Katiba, na pia italeta urahisi endapo sheria
itahitaji marekebisho, tofauti na Katiba ambayo utaratibu wa kuirekebisha ni
mrefu na mgurnu. Maoni mengine ya CCM ambayo hayakuzingatiwa yalihusu ibara
zifuatazo:
Ibara ya 2
CCM ilipendekeza
maneno katika ibara hii yasomeke ''eneo lote la Tanzania Bara na
eneo lote la Zanzibar pamoja na sehemu zake zote za bahari, maziwa, rnito na maeneo rnengine
yatakayoongezwa" Maneno: "Maziwa, mito na maeneo mengine yatakayoongezeka”
hayajazingatiwa.
Maeneo ya ndani yenye maji ambayo
ni sehemu ya nchi yasipotajwa bayana kunaweza kuwa na changamoto ya tafsiri ya mipaka
kati ya nchi yetu n anchi nyingine jirani. Kwa mfano pale mpaka rmapopita juu
ya maji mfano mgogoro unaotaka kujitokeza kuhusu umiliki wa Ziwa Nyasa.
Ibara ya 10
Hii ilikuwa ibara ya 11 katika Rasimu ya Kwanza ikihusu
malengo makuu ya Serikali
na utekelezaji
wake. CCM ilikuwa na maoni
kwamba kutokana Muundo wa Serikali unaopendekezwa
malengo haya hayawezi kutekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano bali nchi
washirika.
Malengo yanayotajwa yako katika
maeneo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, kisiasa hususan katika ngazi ya
kijamii na kimazingira. Hata hivyo kwa mundo wa Muungano unaopendekezwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano haina mamlaka wala madaraka ya kuyashughulikia
mambo haya kwa sababu si mambo ya Muungano.
Ibara 11(2)
Ibara hii inahusu Serikali kutakiwa kutoa tarifa Bungeni
si chini ya mara moja kwa mwaka kuhusu utekelezaji wa malengo haya.
9
Muundo wa serikali tatu
unaopendekezwa hautaliwezesha Bunge la Muungano kuhoji utekelezaji wa malengo
haya kwa sababu yatakuwa kwenye himaya ya washirika wa Muungano, ambapo malengo
yatajadiliwa kwenye mabunge yao.
Ibara ya 84 na 85
Ibara hizi zilikuwa
za 80 na 81 kwenye Rasimu ya Kwanza mtawalia. CCM ilipendekeza ibara
hizi ziangaliwe upya kwa kuzingatia mapendekezo ya mundo wa serikali mbili.
Pendekezo hili
halikuzingatiwa
Hali ya hatari na vita katika nchi ni jambo zito na
ndiyo maana kuwekwa kwenye Katiba. Kwa mujibu wa orodha ya Mambo ya Muungano ya 1964 na
orodha iliyoko sasa kwenye Katiba ya 1977, hali ya hatari ni jambo la Muungano.
Rasim ya Pili imeliondoa kwenye orodha ya mambo ya Muungano. Tafsiri iliyo wazi
ni kuwa Rais wa Muungano hana mamlaka ya kutangaza hali ya hatari popote ndani
ya Muungano kwani mambo ya hali ya hatari si jambo la Muungano tena.
lbara ya 233 na 234
Ibara hizi zilikuwa ibara za 217 na 218 za Rasimu ya
Kwanza mtawalia na CCM ilipendekeza ziboreshwe na 217(1) iongezwe kipengele €
chenye maneno “kuandaa na kusimamia sera za kifedha na sera za kibajeti.”
Vilevile ilipendekezwa katika ibara ya 213 majukumu hayo yaondelewe kutoka
Benki nyinginezo.
Pendekezo hili halijazingatiwa.
Moja kati ya kazi za Benki Kuu ni
kusimamia mfumo mzima wa benki za biashara katika nchi. Rasimu ya Pili ibara ya
234 inatoa mamlaka kwa benki za washirika kuhifadhi fedha za serikali zao na
kusimamia sera za fedha za benki hizi. Haya ni mamlaka ya Benki Kuu kupanga
viwango vya riba, kudhibiti mfumuko wa bei, kusimamia viwango vya kubadilisha
fedha za kigeni na masuala mengine yanayohusu sera za kifedha. Pia Rasimu
katika ibara ya 233(2) inaeleza kuwa Benki Kuu itakuwa huru katika kufanya kazi
zake. Lakini ibara ya 233(3) inasema itatungwa sharia itakayoweka muundo
utakaozingatia uwakilishi wa pande zote za Muungano, mamlaka, shughuli na
utendaji wa Benki. Uhuru wa Benki hii utakuwa mashakani kutokana na utekelezaji
wa ibara hii ndogo yay a 233(3).
10
SEHEMU YA PILI
CHANGAMOTO ZA SURA YA SITA
1. MUUNDO
WA MUUNGANO
Eneo kubwa ambalo halikuzingatiwa ni Sura ya Sita ya
Rasimu ya Kwanza ibara za 60-69 zilizohusu muundo wa Muungano. Muundo wa
Muungano ndiyo moyo wa Rasimu na ndiyo unaoamua ibara nyingine zikae vipi. Kwa
hiyo haishangazi kwamba maoni mengi ya CCM katika Sura hii yalikataliwa kwani
CCM ilipendekeza muumdo wa sasa wa serikali mbili uendelee.
Mapendekezo ya CCM kuhusu muundo yanatokana na sera yake,
lakini ieleweke wazi kwamba hii si sababu peke. Katika maoni yake kwenye Rasimu
ya Kwanza CCM iliainisha sababu kadhaa
za kiuchumi, kijamii,
kisiasa na kiusalama
ambazo zina maslahi mapana zaidi kwa taifa letu kuliko sera yake. CCM
inaendelea kuamini kuwa mfumo wa serikali mbili ni bora zaidi na unajenga
mazingita mazuri zaidi ya kuimarisha Muungano
wetu endapo yale
yanayoleta kero hivi
sasa yatashughulikiwa kikamilifu na kwa dhati. Uchambuzi wetu wa Taarifa
ya Tume na viambatisho vyake unaonesha kwamba yapo mambo makuu mawili ambayo
ndiyo msingi wa pendekezo la muundo wa serikali tatu. Kwanza ni malamiko ya
pande zote mbili za Muungano na pili ni rnfululizo wa matukio yaliyosababisha
mgongano wa Katiba.
(i) Malalamiko
Kwa upande wa Zanzibar
malalamiko yanayotajwa:
·
Kuondolewa kwa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano;
·
Kuongezeka kwa mambo
ya Muungano na hivyo
kuathiri madaraka ya Zanzibar
(autonomy) na kufifisha
utambulisho (identity) wake na Zanzibar kuendelea kumezwa;
·
Hisia kuwa Tanzania Bara imevaa koti la Serikali ya Jamhuri ya Muungano na
hivyo kutumia mamlaka hayo kujinufaisha yenyewe kwa gharama ya Zanzibar; na
inafanya hivyo kwa kutobainisha marnlaka ya Serikali ya Muungano kwa mambo
yaliyo ya Muungano kwa upande
mmoja; na mamlaka hayo
hayo kwa mambo yasiyo ya Muungano
kwa upande mwingine;
·
Mkanganyiko kuhusu ugawaji wa mapato na jinsi ya kuchangia gharama za
uendeshaji wa shughuli za Muungano vaina ya Serikali ya Muungano na Serikali ya
Zanzibar.
11
Malalamiko ya Tanzania Bara
· Zanzibar
imekuwa nchi huru, ina bendera yake, ina wimbo wake wa Taifa, ina Serikali yake
na imebadili Katiba yake ili ijitambulishe kama nchi, wakati Tanzania Bara
imepoteza utambulisho wake. Katiba ya Jamhuri inasema Tanzania ni nchi moja
lakini Katiba ya Zanzibar inasema ni nchi mbili;
[Ibara ya (1) inatamka “Zanzibar ni nchi ambayo eneo la
mipaka yake…”; Ibara ya (2) ya Katiba ya Zanzibar inasomeka: “Zanzibar ni
miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano ya Tanzania]
· Zanzibar
imebadili Katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamhuri ya Muungano, kama kama
vile kuelekeza sharia za Muungano zilizopitishwa na Bunge la Muungano zipelekwe
kwenye Baraza la Wawakilishi. Maana yake ni kuwa Katiba ya Zanzibar sasa ipo
juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano;
· Ushiriki
wa wabunge wa Zanzibar katika kujadili na kupitisha sheria kwa masuala yasiyo
ya Muungano ndani ya Bunge na kwa wabunge wa Zanzibar kuwa mawaziri kwa masuala
yasiyo ya Muungano; na
· Haki
ya kumiliki ardhi – wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi
Zanzibar wakati wenzao wenzao upande wa Zanzibar waba haki hiyo Tanzania Bara.
(ii) Mgongano wa Katiba
Hoja ya pili
inayochukuliwa kama sababu ya kutaka serikali tatu ni migongano iliyopo kati ya
Katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano, ni upande wa Serikali ya
Muungano kutotimiza majukumu yake kikatiba. Utafiti uliofanywa na Tume kuhusu
masuala yanayogusa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unabainisha maeneo
yafuatayo yenye migongano ya kikatiba:
a. Katiba ya Zanzibar
Mamlaka ya Dola
Ibara ya (i) ya Mkataba
wa Muungano wa mwaka 1964 iliainisha kuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya
Watu wa Zanzibar zitaungana na kuwa nchi moja
yenye mamlaka moja ya kidola. Vile vile Ibara ya 1 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano inatamka kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi moja.
Hata hivyo ibara ya (1) ya Katiba ya Zanzibar inatamka kuwa Zanzibar ni nchi.
Tume inaonesha kuwa ibara hii ya Katiba ya Zanzibar inakinzana na Katiba ya
Muungano kwa kuwa Jamhuri ya Muungano ni nchi moja na dola moja.
12
Majeshi ya Ulinzi na Usalama
Ibara ya 147 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imekataza
mtu yeyote au shirika au kikundi cho chote kuunda na kuweka Jeshi katika
Tanzania isipokuwa Serikali ya Jamhuri ya Muumgano pekee yenye mamlaka ya
kuunda majeshi ya Ulinzi na Usalama. Katiba ya Zanzibar, kupitia ibara ya 12
1imeanzisha idara maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zikiwemo "Jeshi1a
Kujenga Uchurni (JKU), Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) na Chuo cha
Mafunzo (cha wahalifu). Kwa mujibu waTume, Katiba ya Zanzibar inakinzana na
Katiba ya Jamhuri ya Muungano kwa kuanzisha majeshi wakati hilo ni jukumu la
Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Utungaji wa Sheria za Muungano
Ibara ya 64(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inalipa
mamlaka Bunge Ia Muungano kutunga sheria ambazo zinaweza kutumika Zanzibar. Katiba
ya Zanzibar, ibara ya 132(1) inaweka masharti ya kutumika kwa sheria
iliyotungwa na Bunge la Muungano kwa kutaka sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya
mambo ya Muungano tu. Ibara ya 132(2) inafafanua kwamba Sheria hiyo
lazima ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika. Tume
inaeleza kuwa hali hii inaleta mgogoro wa kikatiba.
Mahakama ya Rufani
Wakati Mahakama ya Rufani, kwa mujibu wa mujibu wa Katiba
ya Jamhuri ya Muungano ni mahakama yenye uwezo wa kuamua rufaa zote nchini,
ibara ya 99 ya Katiba ya Zanzibar inatakata mtu yeyote yule wa Zanzibar
kupeleka kwenye Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesi
zozote zinazohusu tafsiri ya Katiba ya Zanzibar, mambo ya Kiislamu ambayo
yameanzia katika Mahakama ya Kadhi na mambo mengine yoyote yaliyoainishwa
katika Katiba ya Zanzibar na sheria nyingine yoyote iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi. Ibara hii inaonekana kukinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano
kuhusu mamlaka ya Mahakama ya Rufani.
Mamlaka ya Kugawa Mikoa
Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inampa
Rais wa Jamhuri ya Muungano kugawa mikoa nchini. Wakati huo huo, Katiba ya
Zanzibar inampa Rais wa Zanzibar mamlaka kama hayo na hivyo kukinzana na Katiba
ya Jamhuri ya Muungano.
b.
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano na Katiba
Kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Tume
katika Ripoti yake inabainisha maeneo kadhaa ambayo yameleta mkanganyiko katika
13
utekelezaji wa katiba, lakini haikutamka bayana kwamba
mkanganyiko huo ni matokeo ya Katiba kutozingatiwa kikamilifu na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano.
Kutotenganisha Mambo ya Tanzania Bara na ya Jamhuri ya
Muungano
Ibara ya 34 ya Katiba ya mwaka 1977 inaainisha mambo
ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano itaakuwa na mamlaka nayo. Ibara hiyo
inafafanua wajibu wa Serikali ya Muungano kwa mambo ya muungano na mambo yasiyo
ya muungano yanayohusu Tanzania Bara.
Ilitarajiwa kwamba ibara hii ingetekelezwa kwa Serikali
ya Muungano kuweka wazi mipaka yake, wakati gani inasimamia mambo ya Muungano
na wakati gani inasimamia mambo ya Tanzania Bara. Matokeo yake ni malalamiko
kwamba Tanzania Bara imevaa koti la Serikali ya Jamhuri ya Muungano na hivyo
kutumia mamlaka hayo kujinufaisha yenyewe kwa gharama ya Zanzibar. Kushindwa
kutenganisha mipaka hiyo ni mojawapo ya kero za Muungano.
Uundaji wa Tume ya Pamoja ya Fedha na Akaunti ya Fedha ya
Pamoja
Ibara ya 133 inaitaka Serikali ya Muungano kuanzisha
Akaunti ya Fedha ya Pamoja (Joint Finance Account). Lakini akaunti hii
haijaanziswa na hivyo kuwa sehemu ya manung’uniko ya Zanzibar na Zanzibar
kushindwa kuchangia matumizi ya Muunagano na kushindwa kufaidika na mapato
ambayo yangetokana na akaunti hii.
Ibara ya 134 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inaitaka
Serikali ya Jamhuri ya Muungano iunde Tume ya Pamoja ya Fedha (Joint Finance
Commission). Tume hii ilichelewa sana kuundwa. Tume ilizinduliwa mwaka 2003,
lakini haikufanya kazi hadi mwaka 2006 ambapo jukumu lake la kwanza lilikuwa ni
kufanya uchambuzi wa masuala mbali mbali ya Muungano na kuyatolea mapendekezo
Serikalini. Mapendekezo hayo vado hayajafanyiwa kazi kwa mujibu wa hadidu za
rejea.
MUUNDO WA SERIKALI TATU UTAJIBU CHANGAMOTO HIZI?
Malalamiko ya migongmo
iliyoainishwa ina uzito wake. Changamoto hizi zimekuwepo kwa muda
mrefu na kumekuwa na jitihada za mara kwa mara
kuzikabili. Tume na kamati mbali mbali ziimejishughulisha kutafuta ufumbuzi.
Kumekuwa na hoja kwamba Tume na Kamati nyingi za nyuma zilitoa pendekezo la
serikali tatu na hivyo sasa wakati umefika wa kuzingatia mapendekezo hayo. Je,
baadhi ya Tume na Kamati za nyuma zilisemaje? Tume ya Nyalali ilikuwa na
wajumbe 22, wajumbe 13 walipendekeza muundo wa serikali tatu, wajumbe 9
hawakuafiki mundo huu. Kamati ya Jaji Kisanga ilikuwa na wajumbe 15 ambapo 12
walipendekeza muundo wa Serikali tatu na 3 walitaka muundo wa serikali mbili
14
uendelee. Kwa kuangalia mtiririko huu imejengeka dhana
kwamba Tume nyingi zimmetoa mapendekezo hayo na wananchi wanataka hivyo. Lakini
hata kalika Tume na Kamati hizi hakukuwa na makubaliano ya moja kwa rnoja. .
Swali ambalo CCM inajiuliza, je, mundo wa serikali tatu utajibu
changamoto za Muungano? CCM haiamini hivyo, kwani kwa maudhui yake Rasimu ya
Pili ina
uwezekano mkubwa wa kuendeleza changamoto zile zile,
kuzua mpya au nyingine nyingi zaidi ambazo zitadhoofisha Muungano wetu. Changamoto
hizo ni pamoja na hizi zifuatazo:
(i) Ukuu wa Katiba na tekelezaji wa sheria
Maoni yetu ni kwamba
Katiba ni waraka wa kisheria, matukio yote yaliyochukuliwa kama sababu ya
pendekezo la muundo wa serikali tatu yanatokana na Katiba kutozingatiwa.
Hatuamini kwamba idadi ya serikali ndiyo itakuwa tiba endelevu kama hakutakuwa
na misingi madhubuti ya kuheshimu Katiba. Kama Katiba haizingatiwi, hilo litadhoofisha
Muungano wowote ule, uwe wa serikali mbili au tatu.
Kwa kuzingatia umuhimu wa
Katiba kuheshimiwa Tume inapendekeza kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano:
·
itamke bayana kuwa Katiba ya Muungano ndiyo itakuwa na nguvu kuliko Katiba
zingine. Kwahiyo Katiba ya mshirika wa Muungano ikikinzana na Katiba ya
Muungano basi itakuwa ni batili;
·
itamke kuwa ikianza kutumika ni lazima Washirika wa Muungano wabadilishe
Katiba zao ndani ya muda Fulani ili ziweze kuendana na Katiba ya Muungano.
Mapendekezo haya yanayohusu ukuu wa Katiba si mapya.
Katiba ya 1977 ina vipengele hivyo hivyo na huenda vilivyokaa kimadhubuti zaidi
ya hivi vilivyopendekezwa na Tume. Ni wazi kwamba tatizo si kutokuwepo kwa
vipengele vinavyohusu ukuu wa Katiba.
Kwani migongano mingi iliyotokea haikusababishwa na ukosefu
wa ibara zinazohusu ukuu wa Katiba bali Katiba yenyewe kutozingatiwa.
Hali kadhalika masuala mengine yenye utata wa kikatiba au
kisheria yanaweza kushughulikiwa na mfumo uliopo ndani ya Katiba yenyewe. Katiba
ya Jamhuri ya Muungano inaunda Mahakama Maalum ya Katiba ambayo ina jukumu la kusikiliza
na kusuluhisha suala lolote linalohusu tafsiri ya Katiba.
Mamlaka ya Mahakama hii yanaweza kupanuliwa ili iweze
kushughulikia changamoto ambazo zina sura ya mgongano wa kikatiba au kisheria.
Kwa mfano mgongano ulioelezwa kuhusu uundwaji wa majeshi ya ulinzi na usalama,
ungeweza ukatatuliwa kupitia Mahakama hii. Kuundwa jwa vikosi kama JKU, KMKM na
15
Chuo cha Mafunzo kulifanywa kwa sababu maalum. JKU
iliundwa kuhamasisha shughuli za kiuchumi na za kijamii hasa kwa vijana. KMKM
kuzuia magendo ya karafuu na Chuo
cha Mafunzo kwa
ajili ya kurekebisha
mwenendo wa watu waliotiwa
hatiani (ni kama idara ya magereza kwa Zanzibar).
Kwa hiyo kama kuna utata wowote kuhusu hadhi ya vikosi
hivi kwa namna vilivyoanzishwa au jinsi vinavyoendeshwa hivi sasa, basi
Mahakama hii ingeweza kabisa (ikiwa na mamlaka iliyoimarishwa) kuamua kama
vikosi hivi vina sura ya uanzishwaji wa majeshi kwa namna inayokatazwa na ibara ya 147 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano ya mwaka 1977. Kwa mantiki hii, suluhisho si idadi ya serikali bali
mfumo wa kisheria wa kushughulikia masuala haya.
(ii) Changamoto za kimfumo na
kitaasisi katika mfumo unaopendekezwa
· Kiutawala
na kwa mamlaka iliyopewa na Rasimu, Serikali ya Muungano imeundiwa mfumo ambao
unaitenganisha na wananchi, kwani serikali
hiyo haina mamlaka ya kushughulikia masuala yanayowagusa moja kwa moja. Masuala
kama elimu, kilimo, maji, yote yamo kwenye mamlaka ya washirika wa Muungano.
Hali kadhalika Rasimu inatamka kuwepo kwa Mawaziri Wakaazi (ibara ya 67) ambao
jukumu lao ni kuratibu na kusimamia mahusiano vaina ya Serikali z anchi
washirika; na kati ya Serikali ya nchi mshirika na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano.
· Rasimu
inaunda Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali itakayokuwa na jukumu maalum la
kuwezesha uratibu na utekelezaji wa masharti ya Katiba, será, sheria na mipango
baina ya Serikali ya Muungano na serikali za nchi washirika na baina ya
serikali za nchi washirika. Kuwepo kwa vyombo hivi kunaongeza matabaka mapya na
mengi ya urasimu na hivyo kuzidi kuiweka Serikali ya Muungano mbali na
wananchi.
· Rasimu
ya Katiba imetoa jukumu kwa viongozi wakuu wa Muungano n anchi washirika
kuulinda Muungano. Hili ni lengo zuri lakini Rasimu ilipaswa kwanza kuweka
mundo madhubuti wa Muungano ambao ndiyo ungekuwa msingi wa kuulinda. Badala
yake Rasimu inaunda Muungano dhaifu ambao unaonyesha dalili nyingi za kuvunjika
huku ikiaminika kwamba marais watatu wanaweza kuulinda usivunjike.
· Rasimu
imeondoa mundo wa Serikali ya Muungano w anchi mbili na kuleta shirikisho la
serikali tatu, ambalo linadhoofisha Muungano;
· Rasimu
imepunguza orodha ya mambo ya Muungano bila kuangalia taathira yake kwa nchi.
Hatua ya kupunguza mambo ya msingi yanazileta nchi zilizo kwenye Muungano
pamoja haiwezi kuhesabiwa kama inaimarisha
16
Muungano.
Kwa mfano Ulinzi na Usalama ni jambo la Muungano lakini mawasiliano, usafiri wa
anga na bandari si mambo ya Muungano. Katika hali hii nchi haiwezi kuwa na
ulinzi madhubuti kama haidhibiti mawasiliano, usafiri wa anga na bandari.
· Uraia
unachukuliwa kuwa ni jambo la Muungano. Lakini mfumo wote unaopendekezwa
unajenga mazingira ya “kila mtu kuchukua chake” kwa namna ambayo unaweza ukazua
será za ukaazi, ardhi na biashara ambazo hazitalazimika kufuata tunu za
Muungano kama vile umoja. Mfumo huu utaibua kwa urahisi dhana ya “Utanganyika”
na “Uzanzibari”, ambazo zitachukua nafasi ya “Utanzania”. Na hivyo kuuweka
mashakani umoja na utangamano wa taifa letu.
Uchambuzi wetu wa sababu zinazotumiwa kuhalalisha serikali .tatu unaonesha kwamba changamoto za
mfumo mpya ni nyingi na ngumu zaidi kuliko mundo wa serikali mbili.
(iii)
Changamoto
za gharama za uendeshaji wa Serikali ya Muungano
Mojawapo ya mambo ambayo yanahitaji kutazamwa kwa kina
katika mundo unaopendekezwa ni gharama za kuendesha Serikali ya Muungano,
lakini pia athari za gharama hizi kwa nchi washirika. Rasimu inaainisha vyanzo
vya mapato katika ibara ya 231 ya Rasimu kuwa:
· ushuru
wa bidhaa;
· mapato
yasiyo ya kodi yatokanayo na taasisi za Muungano;
·
mchango kutoka kwa nchi washirika;
· mikopo
kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya
Muungano; na
·
mapato mengine.
Ushuru wa bidhaa ni
ushuru unaotozwa katika bidhaa mbali mbali ili kuongeza mapato (bidhaa kama
soda, bia, vinywaji vikali, maji ya matunda au huduma za simu za mkononi) au
wakati mwingine kupunguza matumizi ya bidhaa Fulani Fulani (kama mifuko ya
plastiki, sigara na nyinginezo).
Chanzo hiki ni mojawapo
ya vyanzo vya kugharimia uendeshaji wa Serikali ya Muungano. Hata
hivyo Serikali ya Muungano haina sekta za kiuchumi ambazo zinazalisha. Kwahiyo
kodi inayoelezwa ni ile iliyo ndani ya será zakodi z anchi washirika na ambayo
itakusanywa na nchi washirika wenyewe, lakini wanalazimika kuiwasilisha kwenye
Serikali ya Muungano. Haifahamiki makusanyo hayo yatatosheleza kiasi gani
lakini uzoefu uliopo wa bajeti ya Serikali ya Muungano, unaonyesha kwamba kiasi
cha ushuru wa bidhaa kinachokusanywa hakilingani na majukumu ya serikali kwani
ni kidogo. Kwa mfano, wakati makadirio ya matumizi kwenye mambo ya Muungano
yaliyoainishwa na Rasimuni kiasi cha shilingi trilioni 2.354, makusanyo ya
ushuru wa bidhaa kwa mwaka 2012/2013 yalikuwa kiasi cha shilingi trilioni 1.3.
17
Chanzo kingine cha mapato kinachotajwa ni mchango w anchi
washirika. Katika eneo hili Rasimu inatoa mwongozo uchangiaji huu utafanyika
vipi na kwa uwiano gani. Huu ni upungufu
unaofanana na tatizo lililokuwepo kwa muda mrefu katika Katiba ya mwaka 1977,
lililohusu kutoanzishwa kwa Akaunti ya Pamoja ya Fedha na utaratibu wa
kuchangia na kugawana mapato ya Muungano. Mwongozo huu ni wa muhimu sana
kutokana na mambo mawili. Rasimu inasema kwamba washirika wa Muungano watakuwa
na hadhi sawa [ibara ya 64(4)]. Hii inaweza kueleweka kwamba mchango w anchi
washirika utakuwa sawa kwa sawa. Hata hivyo ukweli ulio wazi ni kwanza uchumi
wa Tanganyika ni mkubwa kuliko ule wa Zanzibar. Kwahiyo kama suala hili
halijaeleweka vizuri ndani ya Katiba litakuwa ni chanzo cha kutoelewana na
kuudhoofisha Muungano.
Suala jingine linalohusu chanzo hiki cha mapato ni kwamba
washirika watatakiwa kuchangia tena kwenye Serikali ya Muungano wakati ambapo
tayari chanzo chao kingine (ushuru wa bidhaa) kimeshatolewa kwa Serikali ya
Muungano kama Katiba Inavyotaka. Hii italeta manung'uniko mapya hasa kutoka
Zanzibar ambayo uchumi wake mdogo utaathirika zaidi kuliko wa Tanganyika.
Hapana shaka kwamba kwa ujumla wake
mundo huu unaopendekezwa utaongeza gharama kwa nchi washirika.
Vilevile, Rasimu inaainisha mikopo toka ndani na nje kama
chanzo kingine cha mapato kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, kwa
mujibu wa orodha ya mambo ya Muungano Serikali ya Muungano haitajishughulisha
na uzalishaji wenye faida ya kipato na haina raslimali zozote za kiuchumi
(investable resources). Kwa hali hiyo haikopesheki ndani wala nje ya nchi. Hii
ni kwa sababu mambo ya Muungano yote ni ya huduma kwa wananchi (Katiba na
Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania; Ulinzi na Usalama; Uraia na
Uhamiaji; Sarafu na Benki Kuu; Mambo ya Nje; Usajili wa Vyama vya Siasa; ushuru
wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na mambo ya Muungano).
Kwa upande wa mapato yasiyokuwa ya kodi yatokanayo na
taasisi za Muungano kikubwa kinachotegemewa hapa ni maduhuli (kama vile malipo
ya viza kwa wageni wanaoingia nchini; malipo ya kuanzisha kampuni na mengineyo)
ambayo ni kiasi kidogo sana cha fedha. Hivyo basi, kwa kuzingatia kodi
itokanayo na ushuru wa bidhaa ni ndogo, maduhuli pia ni kidogo, Serikali ya
Muungano haitaweza kujiendesha kwa
vyanzo hivi ambavyo ndivyo vinaonekana kupewa kipaumbele.
Rasimu vile vile inabainisha kuwa Serikali ya Muungano
itakuwa na vyanzo vya mapato ambavyo havijaainishwa kwa kusema "mapato
mengine." Chanzo hiki hakieleweki kwani Rasimu haijaweka wazi hayo mapato
mengine ni yepi. Chanzo chochote cha mapato lazima kielezwe vizuri kwani mapato
siyo tu suala la kodi bali la kisheria, na
mazingira ya kupatikana na kutozwa kwake lazima yafahamike wazi kwa wanaotozwa.
Kwa ujumla, ni wazi kwamba gharama za kuendesha Serikali
ya Muungano zitakuwa ni kubwa kuliko mapato.ya Muungano kama tulivyoonesha hapo
juu. Na
18
bado haijulikani
uendeshaji wa taasisi nyingine utakuwaje ambazo zitahusika na usimamizi
wa baadhi ya mambo ya Muungano kwa upande mmoja, na kughalimia vyombo muhimu kama
vile Ofisi ya Rais wa Jamhuri wa Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano; chombo
cha kusimamia manunuzi ya umma; chombo cha uendeshaji wa Mfuko Mkuu wa Hazina;
chombo cha kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali ya Muungano; Tume ya
Uhusiano na Uratibu wa Serikali na taasisi nyingine nyingi zitakazoundwa.
Hivyo basi, muundo unaopendekezwa na Rasimu utakuwa na
gharama kubwa sana za uendeshaji kuliko vyanzo vya mapato vilivyoaninishwa.
19
SEHEMU
YA TATU
HITIMISHO
NA MWELEKEO
CCM inatambua changamoto zilizoainishwa na umuhimu wa
kuzishughulikia kwa njia endelevu kwa kutumia Katiba, sheria na taratibu za
uendeshaji. Mapendekezo yetu ya kuendelea na mfumo wa serikali mbili hayatokani
tu na será ya CCM, bali udhaifu mkubwa uliojionesha katika pendekezo la mundo
wa serikali tatu. Hivyo basi CCM inapendekeza kwamba mfumo wa serikali mbili
ufanyiwe marekebisho ambayo yatashughulikia changamoto zilizopo. Marekebisho
hayo ni pamoja na kuzingatia:
yetu ya kuendelea na•n-.ft.uno wa serikali mbiii
h.c1yr.:o:.:mi tll na sera ya CCM, bnli udhaifu mku"bwa dicjione:;ha
katika pendekezo Ja znuunJo wa: serikali tatu. Hivyo basi cc.M U16.pendekeza
kwiunba Infumo wa 5CiikaU mbU.i u{imyi\ve•\iuirekibisho ambayo yatashii:ghu!iki
ch.angamoto ilizop . ]..1arel<ebi h • .,hayci •111.paJI1oj na kuzingatia:
1. Nafasi
ya Rais wa Zanzibar katika Muungano
Rais wa Zanzibar awe
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa msaidizi wake kwa masuala
ya Zanzibar na mmoja wa viongozi wakuu wan chi. Hii itaongeza kuweka wazi
madaraka ya Rais wa Zanzibar ndani ya Serikali ya Muungano na nje ya nchi.
2. Akaunti
ya Fedha ya Pamoja
Ifunguliwe
Akaunti ya Fedha ya Pamoja ambamo zitawekwa fedha zote zitokanazo na mapato ya
vyanzo vya Muungano kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Aidha,
uwepo utaratibu wa kisheria utakaoelekeza uendeshaji wa akaunti hii pamoja na
kuweka mgawanyo wa mapato hayo kwa pande mbili za Muungano. Hii itasaidia
kuwianisha uchumi wa pande hizo mbili. Sheria kuhusu utaratibu huu isimamiwe na
Tume ya Uhusiano na Uratibu kama ilivyoperidekezwa katika Rasimu.
3. Tume
ya Pamoja ya Fedha
Tume
hii ambayo imetamkwa kwenye Katiba na
kwa kupitishwa na sheria ya Bunge imeshaundwa hivi sasa, na mamlaka yake
yanafahamika. Tunapendekeza tume hii ipewe nguvu zaidi , iwekewe mfumo
madhubuti wa kuendesha na kusimamia kwa karibu. Mapendekezo yanayotolewa na
Tume yashughulikiwe na serikali zote mbilikwa haraka , ili kama hakuna kikwazo
mapendekezo yake yatekelezwe bila kuchukua muda mrefu.
4. Sheria
mahususi kuhusu Uratibu wa Mambo ya Muungano
Iwepo
Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo ya Muungano kikatiba na uendeshaji wake
ulingane na mwenendo wa sasa wa vikao vya pamoja vya kero. Uratibu na usimamizi
wa masuala ya Muungano uwekwe kisheria na Tume ipewe mamlaka ya kuzisirnamia
taasisi zote za Muungano katika makubaliano yatakayoafikiwa na pande zote mbili.
20
5. Uhusiano
wa kimataifa na mashirika/taasisi za nje
Zanzibar
iweze kuwa na uhusiano wa kimataifa katika masuala yasiyo ya Muungano, kwa
kuihusisha Wizara ya Mambo ya Nje.
6. Uwezo
wa Zanzibar kukopa ndani na nje
Katika
maeneo ambayo si ya Muungano Zanzibar iwe huru kutafuta misaada na mikopo
yenyewe bila vikwazo ila Wizara za Fedha na Mambo ya Nje zishirikishwe.
7. Kutenganisha
mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano
Ili
kuondoa rnkanganyiko wa Tanzania
Bara kuvaa koti
la Serikali ya Muungano, tunapendekeza mabadiliko katika
vyombo vya Muungano:
(i)
Bunge
· Pendekezo
la kwanza: kuwe na Baraza la Wawakilishi la Tanzania Bara kwa ajili ya kushughulikia masuala ya
Bara tu. Katika pendekezo hili majimbo ya Jamhuri ya Muungano yaundwe upya ili majimbo ya uchaguzi ya Baraza la
Wawakilishi la Zanzibar yawe ndiyo hayo hayo majimbo ya uchaguzi ya Bunge la
Jamhuri ya Muungano.
· Endapo
muundo huu utaafikiwa basi masuala ya Muungano yatakuwa yakitekelezwa na Bunge litakalowashirikisha
wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar (ambao watatumika kama wajumbe wa
Bunge la Muungano na Wabunge wa Tanzania Bara (ambao watashughulikia masuala ya
Tanzania Bara katika Baraza lao la Wawakilishi)).
· Pendekezo
la pili: Bunge la Muungano wakati
linajadili mambo ya Muungano wabunge wote washiriki majadiliano na itapofikia
kujadili mambo ya Bara washiriki wabunge wanaotoka Bara tu. Kama Spika anatoka sehemu moja ya Muungano, Naibu
wake atatoka upande wa pili na wakati wa vikao vya masuala ya Bara Spika/Naibu
Spika anayetoka Bara ndiye atakayeendesha kikao. Inapendekezwa Bunge la Jamhuri
ya Muungano liwahusishe Wabunge w apande zote za Muungano linapojadili masuala
ya Muungano. Kwa mambo yanayohusu mambo yasiyo ya Muungano, haya yatekelezwe na
Wabunge wa Tanzania Bara pekee.
(ii) Mawaziri Katika Serikaii ya Muungano
Wajumbe
wa Bunge la Muungano wanaweza kuwa mawaziri wa wizara za mambo ya Muungano tu.
Wizara zisizo za Muungano ziongozwe na wabunge wanaotoka Tanzania Bara tu.
(iii) Mambo
ya Muungano
Pamoja na orodha ya mambo ya Muungano ambayo yatakuwa kwenye Katiba,
mambo yasiyo ya Muungano yaorodheshwe kwenye sheria itakayoainisha pia
usimamizi, utekelezaji wake na gharama zake.
21
(iv) Muundo
wa Mahakama ya Juu
Ndani ya Mahakama ya Juu kiwepo kitengo maalum kitakachoshughulikia
masuala ya Katiba tu
(v) Misaada
na mikopo nafuu kutoka kwa wahisani
Serikali
ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zijadili kwa kina kanuni ya
mgawanyo wa fedha zinazopatikana toka
chanzo hiki. Kuwekwe utaratibu wa kisheria
kutenganisha misada inayotekelezwa kwenye miradi ya Muungano na isiyo ya
Muungano.
No comments:
Post a Comment