- Adai madiwani wao waliojiuzulu Shinyanga wamenunuliwa
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.
Willibrod Slaa, amesema kuwa mbunge au diwani anayetaka kuondoka CHADEMA
milango iko wazi, kwa sababu hawawezi kumvumilia kiongozi msaliti wa chama. Dk. Slaa alitoa msimamo huo jana wakati akimnadi mgombea ubunge
wa CHADEMA jimboni Kalenga, Grace Tendega, katika mkutano wa kampeni
uliofanyika kwenye uwanja wa mnadani, Kijiji cha Kidamali, Kata ya Nzihi huku
akisisitiza kuwa wameridhia kujiuzulu kwa madiwani wao wawili mkoani Shinyanga. Alisema kujiuzulu kwao ni mpango maalumu uliotengenezwa na
wapinzani wao kisiasa kwa lengo la kuwadhoofisha na kuwavuruga.
Mlowe, D. / Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment