WAZIRI wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amekikejeli Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kwamba kinaufanya uchaguzi wa rais kama uchaguzi wa kiongozi
mkuu wa Kanisa Katoliki duniani (Papa). Membe
alitolea mfano wa uchaguzi wa Papa jana wakati akijibu maswali ya waandishi wa
habari waliotaka kupata maoni na hatima yake kisiasa, baada ya CCM kumfungia
kwa miezi 12 na kumuweka chini ya uangalizi, baada ya kumtia hatiani kwa makosa
ya kukiuka kanuni za chama hicho kwa kuanza mbio za urais mwaka 2015 mapema.
Waziri Membe alisema
kuwa mataifa mengi duniani yameiga mambo mengi yakiwemo mavazi ya majaji,
wanasheria na spika wa bunge kutoka utamaduni wa Kirumi unaotumiwa na kanisa
hilo, lakini yameshindwa kuiga uchaguzi wa Papa.
Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment