MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye pia ni mjumbe wa
Bunge Maalumu la Katiba, jana alinusuru mchakato wa uchaguzi wa mwenyekiti wa
muda baada ya kuibuka vituko. Mbowe katika ushauri wake alitaka mchakato huo uanze upya kwa
karatasi za kura kugawiwa kwa utaratibu makini ili kila mmoja apige kura huku
milango ikiwa imefungwa. Ushauri wake ulikubaliwa na mwenyekiti wa kikao hicho ambapo
mchakato ulifanyika upya kwa usimamizi mkali wa polisi, huku Bunge likiahirishwa
kwa robo saa kutoa fursa ya kura kuhesabiwa.
Awali vituko kejeli na malumbano vilitawala zaidi uchaguzi huo
wa Bunge lililoanza vikao vyake jana mkoani hapa. Dalili za kuvurugika kwa uchaguzi huo zilianza kuonekana mapema
kutokana na idadi kubwa ya wajumbe kusimama na kuwasha vipaza sauti bila
kufuata taratibu walizoambiwa mapema. Kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba, mwenyekiti huyo wa
muda atakuwa na jukumu la kuandaa na kupitisha kanuni za Bunge hilo
zitakazotumika katika mijadala mbalimbali.
Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment