Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshangazwa na uamuzi wa serikali wa
kuwalipa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba posho ya Sh. milioni tisa kwa
mwezi, huku ikiacha kuwatoza Kodi ya Mapato (Paye) kutoka katika fedha hizo,
kinyume cha sheria za nchi.
Pia kimewashangaa wajumbe hao, ambao ni
watunga sheria mama ya nchi (katiba) kuwa wavunjifu wa sheria ya kodi kwa
kutolipa kodi.
Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa Chama hicho, John
Mrema, alisema:
“Haiwezekani (wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba) walipwe
milioni tisa kwa mwezi bila kukatwa kodi wakati mwalimu analipwa 298,000 kwa
mwezi na anakatwa kodi.”
Alisema daima katiba ya nchi hutakiwa kutungwa na
wazalendo na kwamba, kipimo kimojawapo cha uzalendo ni pamoja na kulipa kodi
ili kutekeleza sheria za nchi bila shuruti na kuwataka wajumbe wote wa Bunge
hilo kulipa kodi hiyo kwa mujibu wa sheria.
Pia aliitaka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kukusanya kodi ya mapato kwa mujibu wa sheria za nchi.
“Haiwezekani
watunga sheria mama wawe wavunjifu wa sheria ya kodi. Hiyo katiba wanamtungia
nani akaitekeleze kama wao wenyewe siyo watiifu wa sheria za nchi?” alihoji
Mrema.
Aliongeza: “Ni wakati sasa wa TRA kuonyesha kwa vitendo na siyo
kuwaumiza wafanyabiashara wadogo na wafanyakazi kwa mashine zao za EFD, huku
wanasiasa wakiachwa bila kodi.”
Muhibu S. /Ippmedia-Nipashe
No comments:
Post a Comment