Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, January 21, 2014

Wananchi; Shehena ya Mahindi ni ya kutupumbuza udiwani Mpwayungu?

WANANCHI wa Kata ya Mpwayungu, wilayani Chamwino,  mkoani Dodoma, wameihoji Serikali kuu iwapo Shehena ya Mahindi inayoingia Katika Kata yao ni ya kuwapumbuza dhidi ya Kampeni za   Uchaguzi Mdogo wa Udiwani wa Kata yao ya Mpwayungu.?

Maswali hayo magumu kwa Serikali yametolewa na wananchi hao mara baada ya Mbunge wa Mtela, Livingstone Lusinde, kuwa Mgeni Rasmi wa Uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi huo zilizozinduliwa karibuni, ambapo katika Hotuba yake aliponda Elimu ya Vijana wa sasa.

Hatua ya kuhoji Shehena hiyo ya Mahindi iliyoanza kuwasili kwa Lori siku moja kabla ya Uzinduzi huo, zimekuja baada ya Wasomi kijijini hapo kumshanagaa Mbunge Lusinde aliyekuwa akiporomosha matusi ya kuiponda Elimu, na kuona kwamba labda Mahindi hayo yalimtia kiwewe.

Sababu za Lusinde kuiponda Elimu ya sasa kuwa imetolewa na Chuo Feki, inatokana na kujulishwa kuwa, Mgombea wa Chama cha Mapinduzi anayemnadi, Edward Mgaya, anapambana na Msomi aliyehitimu Chuo Kikuu Sokoine, Josia Mtonyi, anayegombea kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kutokana na Msomi huyo (Mtonyi na wasomi wenzake wa Chuo Kikuu (UDOM) kurejea nyumbani (Kata ya Mpwayungu) kuwafundisha wanafunzi wenzao na hatimae Mtonyi kugombea Udiwani, Lusinde anaota ndoto kana kwamba Vyuo walivyosoma ni Feki, kumbe wanarejea kuiamsha Jamii.

Mmoja wa wasomi anayempigia Chapuo Mtonyi amesema, kama Chuo cha Sokoine ni Feki kwa nini CCM kianze kupeleka Shehena ya Mahindi kuwapumbaza wananchi kwa mulo wa siku moja na wakapata mateso ya miaka mitano? Chuo hicho ni kizuri ndiyo maana nguvu ya Mahindi inaongezwa.

“Ni Heri Chuo Feki kinachofundisha Maadili Mema ya kuwatoa watu katika maangamizi  na kutooa wake wengi na kuwatelekeza watoto bila Elimu, kuliko chuo kinachofundisha kuwatesa wananchi na kuibaka Elimu wakiwemo watoto wa walalahoi”.alisema mmoja wa wazee aliyesema, Fedha na Mahindi ya CCM watakula, lakini katika kura  watamchagua Mtonyi.

Aidha Chadema bado haijazindua Kampeni zake, lakini CCM wameshazindua Majuzi, lakini Chadema wamemwambia Lusinde, asubiri vidonge vyake vichungu ameze na wamehoji kwa nini Shehena hiyo ya mahindi ipatikane wakati huu wa uchaguzi? Wananchi Msidanganyike! 

No comments: