VIGOGO wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Mvomero Morogoro, wamewakwamisha Madiwani wanne na wanachama wa Chama hicho waliopanga kumuandamia Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa, kwa kuchelewesha Malipo ya Wakulima wadogo wa Miwa.
Vigogo hao majina yamehifadhiwa, waliwazuia Madiwani na wanachama hao, wakidai wasifanye hivyo hadi watakapopata kibali cha Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC), Faustine Shilogile).
Hatua ya Madiwani hao kuwaunganisha wanachama hao, ilikuwa ni kumuiga Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Mtibwa, Luka Mwakambaya, ambaye wananchi wa Kata yake wakicheleweshewa Malipo wakiwepo Wafanyakazi wa Msimu na Wastaafu, huandamana hadi kwa Mwekezaji na kukesha nao nje ya Lango na Malipo hutolewa.
“Tangu asubuhi jana, Madiwani hao walionekana kukwepana ambapo ni mmoja tu alionekana katika Kijiji cha Kidudwe ambako walikuwa wakipanga Mkakati huo, lakini wengine wote waliokomea kinyemela huku wakirudi makwao”.alisema mtoa habari wetu.
Siku chache zilizopita, Diwani Mwakambaya (CHADEMA) kwa mara ya pili mfululizo, aliongoza Nguvu ya Umma iliyopelekea Wastaafu na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa kupata Malipo yao, huku wakulima wakisubiri makubaliano yaliyoingiwa na Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amosi Makala.
Aidha Naibu Waziri wa Maji Makala, siku chache zilizopita, alifanya Kikao na Wakulima wadogo wa Miwa na Uongozi wa Mtibwa katika Ukumbi wa Community Centre, ambapo Mwekezaji aliahidi kuwalipa kwa awamu wakulima hao hadi mwezi Februari Mwaka huu.
Aidha Imefahamika kuwa, Menjimenti ya Mtibwa imeshaingiza Fedha kwenye Amana ya Chama cha Wakulima Wadogo wa Miwa (MOA) na TUPPRICOS zaidi ya Milioni 28/- lakini wakulima wanadai fedha hizo ni kidogo hazitoshelezi wakulima wote, ila ni sawa na kuwalipa Vigogo wawili wenye Miwa Mtibwa.
No comments:
Post a Comment