Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Freeman Mbowe ametangaza LEO kuanza
kwa ziara Pamoja Daima yenye lengo la kuwaandaa Wananchi kushiriki kikamilifu
kwenye Mchakato wa Katiba na kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura baada
ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutangaza watu kujiandikisha.
Akizungumza
na Waadishi wa Habari jijini Dar es Salaam LEO katika Mkao Kuu ya chama hicho,
Mbowe amesema kuwa operesheni au shughuli hiyo itaongozwa na timu tatu
zitakazoanzia mikoa ya Mwanza, Ruvuma na Tanga.
Mwenyekiti huyo
amesema pia ziara hiyo itakuwa ni ya wiki mbili na siku zinaweza kuongezeka
kadiri itakavyohitajika.
"Katiba Mpya ni
lazima na kama haitapatikana kwa utaratibu uliowekwa kwa mapenzi tu ya Rais na
Wabunge wachache wa CCM, Watanzania wataitafuta Katiba Mpya kwa utaratibu
mwigine,"amesema.
No comments:
Post a Comment