Kada wa CCM kwa maisha yake
yote (miaka 80) Mzee Mwang'ombe anayeishi Chimala, Mbarali, ametoa kiwanja
kwaajili ya tawi la CHADEMA kwa vijana wa bodaboda.
Inaaminika kada huyo bado
hajarudisha kadi ya CCM lakini anaamini CCM imepoteza misingi na inahitaji
mbadala.
Yeye anasema
siasa amekaa pembeni, lakini anatoa maisha yake yaliyo bakia, misaada na mawazo
kwa watu na vyama vyenye muelekeo mzuri wa kulikomboa Taifa letu alipendalo kwa
dhati " TANZANIA"
Baada ya mkutano wa Operation Pamoja
Daima kuisha viwanja vya stand mpya kijiji cha Chimala. Wana MBARALI walitembea
zaidi ya kilometer moja kwaajili ya ufunguzi wa tawi la bodaboda stend ya
zamani. Pichani maelfu ya watu wa Chimala na vitongoji vyake wakishuhudia
ufunguzi huo ulio ongozwa na Dr. Na Mh. Mbilinyi aka Sugu




No comments:
Post a Comment