Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, January 25, 2014

KUHUSU AJALI MWENYEKITI WA TAIFA MBOWE

Taarifa ya awali kuhusu ajali iliyohusisha pikipiki na gari alilopanda Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe leo majira ya saa 6 mchana.

Mwenyekiti Mbowe tangu alfajiri alikuwa safarini akitokea Dar es Salaam kwenda Ngara, Kagera akiingia rasmi kujiunga na wapiganaji wengine kwa ajili ya mikutano ya M4C- Operesheni Pamoja Daima inayoendelea maeneo mbalimbali nchi nzima.

Wakiwa umbali wa takriban kilometa 1.5 kabla ya kufika mji wa Katoro, wakitokea Geita mjini, ghafla mbele ya gari hiyo alitokea mwendesha pikipiki, ambaye aliingia barabara kuu kwa mwendo wa kasi.

Kutokana na hamaki iliyomkumba 'bodaboda' huyo baada ya kuingia barabarani kwa kasi, pikipiki yake ikamshinda na ikawa inakwenda upande wa gari aliyokuwa amepanda Mwenyekiti Mbowe.

Mwendesha pikipiki huyo akaamua kuruka na kuiachia pikipiki yake, iliyokwenda kugongana uso kwa uso na gari alilopanda Mwenyekiti.

Abiria wote waliokuwa kwenye gari wametoka salama usalimini. Gari imeharibika kiasi fulani sehemu ya mbele, ikiwemo kupasuka kioo. Mwendesha pikipiki amepatwa na majeraha/michubuko kutokana na kuruka, hivyo kuangukia kwenye lami. Ameweza kupanda baiskeli kwenda kituo cha polisi.

Baada ya kuandikisha maelezo kituo cha polisi, Mwenyekiti Mbowe amepanda gari nyingine kuendelea na safari ili aweze kuwahi mkutano aliopangiwa kuhutubia leo jioni Ngara Mjini.


Makene

No comments: