CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepokea kwa
mshtuko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha na Uchumi na
Mbunge wa Kalenga, Dkt. William Mgimwa ambaye amefariki akiwa kwenye matibabu
Afrika Kusini.
Kwa masikitiko makubwa CHADEMA kinatuma salaam za pole kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwa kuondokewa na msaidizi
wake wa karibu na mtumishi mwenzake serikalini.
Chama kinatoa salaam za dhati kwa familia ya marehemu Mgimwa kwa
kuondokewa na baba na mpendwa wao, katika wakati ambao tunaamini walikuwa bado
wakimhitaji sana kama moja ya nguzo za familia.
CHADEMA pia inatuma salaam za pole kwa uongozi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kutokana na msiba huo wa kuondokewa na mmoja wa wanachama na
wabunge wake.
Mwenyezi Mungu awapatie moyo wa subira wakati huu wa majonzi
mazito ya kuondokewa na mpendwa wao, Dkt. Mgimwa.
No comments:
Post a Comment