CHAMA CHA
DEMOKRASIA NA MAENDELEO – CHADEMA KANDA YA KASKAZINI
(Tanga,
Kilimanjaro, Arusha & Manyara)
TAARIFA KWA
UMMA WAGOMBEA WA UDIWANI - KANDA YA KASKAZINI
Tarehe
15 Januari 2014, wagombea wafuatao wa CHADEMA walipitishwa na TUME YA UCHAGUZI
kuwania nafasi za uwakilishi (UDIWANI) katika maeneo ya kata mbalimbali za
kanda ya Kaskazini.
Wagombea
hawa walipita katika mchujo wa uteuzi wa chama. Chama kina matarajio makubwa
sana kuwa wananchi wa maeneo haya ya kata hizi watapata fursa nzuri ya
kuwachagua wagombea wa CHADEMA ambao wana dhamira njema sana na ya kweli katika
kuwatumikia.
Wagombea waliopitishwa pamoja na
mikoa yao ni:
Katika
uchaguzi huu CHADEMA imejipanga kushiriki kikamilifu sana tukiwa na uhakika
kuwa chama kimewapa wananchi wapiga kura chaguo lao kwa kuzingatia uwezo wa
wagombea, utayari wa wagombea wetu kushirikiana na kuwatumikia wananchi na
dhamira njema ya kutatua matatizo na kero za wananchi zilizoletwa na CCM kwa
kushindwa kutimiza wajibu wao.
Aidha
chama kimesikitishwa sana na uhuni na ushenzi uliofanywa wa kumteka mgombea wa
CHADEMA ndg. ALLY SAIDI JAHA saa nane mchana siku ya tarehe 15.01.2014 muda
mfupi kabla ya muda kurudisha fomu kufungwa. Tukio hili limetokea huku tukiwa
na taarifa zilizopatikana baadae kuwa mida ya saa nne asubuhi mgombea wetu alifuatwa
na kiongozi mmoja wa CCM wa wilaya. Uongozi wa kanda tumesharipoti tukio hili
polisi na kupewa RB namba LUS/RB/75/2014 TAARIFA.16.01.2014 ya kutekwa/kupotea
kwa ndg ALLY SAIDI JAHA. Hali kadhalika uongozi chama wa Jimbo la Mlalo
umeshwandikia barua msimamizi wa uchaguzi kuhusu tukio hili la kutekwa nyara na
kupotea kwa mgombea wetu na kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hili kwa kina
chake, chama kitakuwa na mahali pa kuanzia.
Hivi
sasa tumetuma timu ya intellijensia ya chama kuchunguza kwa kushirikiana na Red
Brigade ya wilaya ili kupata undani wa tukio hili ambalo limetufedhehesha sana
na ambalo litakuwa limewanyima demokrasia ya kuchagua kwa watu wa Mtae ya
kiongozi na chama wanachokitaka. Niwahakikishie wakazi wa Mtae na Watanzania
wote wapenda mabadiliko ambao jambo hili limetukera wote kuwa ndg Ally Saidi
Jaha atatafutwa mpaka apatikane akiwa mzima au vinginevyo ili ifahamike nini
kimemtokea na pia awaeleze watu wa Mtae na Watanzania wote hili jambo kuna nini
nyuma yake. Hapa kuna mtu au watu watawajibika kwa gharama yoyote, hili jambo
halitaisha kirahisi hivi hivi.
Niwaombe
wakazi wa Kanda ya Kaskazini, kwenye uchaguzi huu tuunganishe nguvu zetu kwa
sisi wenyewe kujitolea na muda wetu na rasilimali zetu, ili tuwashughulikie CCM
ambao wamekuwa wakiendelea kuwatesa Watanzania kwa sera zao mbovu na uongozi wa
kihuni ambao haujali kabisa maisha ya Watanzania.
Imetolewa leo tarehe 16
Januari 2014.
Amani Golugwa
Katibu wa Kanda ya
Kaskazini
+255 754 912 914 au 0784
343 275
golugwa@gmail.com

No comments:
Post a Comment