Kuna habari mtandaoni ambayo imeletwa na kada mmoja wa CCM; mada kuwa CCM imepita bila kupigwa Kata ya Mtae wilayani Lushoto, Mantiki ya mada ile ilikuwa ni kuonyesha kuwa CHADEMA imeshindwa kusimamisha mgombea na hivyo kuwapa unafuu CCM kupita bila kupigwa.
Mosi, Ifahamike kuwa CHADEMA tulisimamisha wagombea wa udiwani kwenye kata zote 27 zilizotangazwa kuwa wazi kata ya Mtae ikiwa moja ya kata ambazo ushindi kwa CHADEMA ungekuwa wa mapema asubuhi kutokana na kukubalika kwa CHADEMA na nguvu ya chama kwenye eneo hilo,
Baada ya CCm kulitambua hilo kutokana na kukua kwa kasi kwa CHADEMA kwenye mkoa wa Tanga hasa wakiwa na kumbukumbuku ya uchaguzi wa kata mbili za wilaya ya Muheza (Tingeni na Bombani) ambapo CHADEMA haikuwa na wagombea kwenye kata hizo 2010 lakini kwenye uchaguzi wa kata hizo baada ya kutangazwa kuwa wazi 2013 CHADEMA iliingia kwa kasi ambayo CCM hawakuitarajia na kwa yoyote aliyefuatilia kampeni za uchaguzi ule anajua ninacho ongelea hapa kuwa ni kitu gani.
Kuhusu swala la Mgombea udiwani kata ya Mtae, kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari Mratibu wetu wa kanda ya Kaskazini Bw Amani Golugwa amelitolea maelezo kama ifuatavyo;
"... Aidha chama kimesikitishwa sana na uhuni na ushenzi uliofanywa wa kumteka mgombea wa CHADEMA ndg. ALLY SAIDI JAHA saa nane mchana siku ya tarehe 15.01.2014 muda mfupi kabla ya muda kurudisha fomu kufungwa. Tukio hili limetokea huku tukiwa na taarifa zilizopatikana baadae kuwa mida ya saa nne asubuhi mgombea wetu alifuatwa na kiongozi mmoja wa CCM wa wilaya. Uongozi wa kanda tumesharipoti tukio hili polisi na kupewa RB namba LUS/RB/75/2014 TAARIFA.16.01.2014 ya kutekwa/kupotea kwa ndg ALLY SAIDI JAHA.
Hali kadhalika uongozi chama wa Jimbo la Mlalo umeshwandikia barua msimamizi wa uchaguzi kuhusu tukio hili la kutekwa nyara na kupotea kwa mgombea wetu na kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hili kwa kina chake, chama kitakuwa na mahali pa kuanzia.
Hivi sasa tumetuma timu ya intellijensia ya chama kuchunguza kwa kushirikiana na Red Brigade ya wilaya ili kupata undani wa tukio hili ambalo limetufedhehesha sana na ambalo litakuwa limewanyima demokrasia ya kuchagua kwa watu wa Mtae ya kiongozi na chama wanachokitaka. Niwahakikishie wakazi wa Mtae na Watanzania wote wapenda mabadiliko ambao jambo hili limetukera wote kuwa ndg Ally Saidi Jaha atatafutwa mpaka apatikane akiwa mzima au vinginevyo ili ifahamike nini kimemtokea na pia awaeleze watu wa Mtae na Watanzania wote hili jambo kuna nini nyuma yake. Hapa kuna mtu au watu watawajibika kwa gharama yoyote, hili jambo halitaisha kirahisi hivi hivi."
Kwa wanachadema na watanzania wengine wenye mapenzi mema na demokrasia ya nchi hii mliotaka kujua kiichotokea kata ya Mtae wilayani Lushoto halihalisi ndio hiyo.
No comments:
Post a Comment