Kutokana na maswali kutoka kwa wanahabari wa vyumba mbalimbali
vya habari juu ya agenda za kikao cha Kamati Kuu kesho, Chama kimetoa kauli
ifuatayo;
Ni kweli kutakuwa na mkutano maalum wa Kamati Kuu ya chama kesho
tarehe 3 Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano huo ni
tatu;
Mosi; Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko
ya katiba
Kamati Kuu itapokea taarifa juu ya kupitishwa kwa marekebisho ya
sheria ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa
2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.
Pili; Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma
mbalimbali zilizoelekezwa kwao.
Wanachama hao walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na
wamewasilisha utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa kuzingatia
matakwa ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya
kikao kinachohusika.
Tatu; Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014
Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango
Mkakati wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati
makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na taifa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano
No comments:
Post a Comment