Mmoja wa wanachama watatu wa CHADEMA waliovuliwa nafasi zao
za uongozi ndani ya chama, Zitto Kabwe kupitia kwa Wakili wake, Alberto Msando,
leo ameanza kufanya ‘FORUM SHOPPING’ kwa kupeleka maombi Mahakama Kuu ya
Tanzania, akiomba Kamati Kuu isijadili na kuamua jambo lolote kuhusu uanachama
wake, kwenye kikao maalum kinachofanyika kesho.
Awali muombaji kwa namna ambayo inaweza kuitwa kuwa ni
kuvizia, alitaka Mahakama Kuu hiyo itoe amri kutokana na ombi lake hilo, bila
upande wa chama kuwepo mahakamani, lakini kwa bahati nzuri mawakili wa chama,
Mwanasheria Mkuu wa chama, Tundu Lissu na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za
Binadamu, Peter Kibatala; wakafanikiwa kuwepo kortini, hivyo wakawa-served
maombi hayo kisha mahakama ikalazimika kusikiliza Preliminary Objections (PO)
kutoka kwa mawakili wa CHADEMA dhidi ya waleta maombi.
Maombi hayo ya wakili Msando kwa niaba ya Zitto yamefunguliwa
mahakamani dhidi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA na Katibu Mkuu wa Chama.
Hoja za mawakili wa CHADEMA katika PO zilikuwa ni katika
maeneo matatu ambayo ni vifungu vya kisheria ambavyo waombaji walikosea;
1. Vifungu vya sheria walivyotumia waombaji kuomba court
injunction, haviipatii Mahakama Kuu mamlaka ya kufanya maamuzi hayo wanayoomba
ifanye. Kwa sababu kwa ujumla ukikosea vifungu hasa vinavyohusu msingi wa kesi,
ni sawa na kwamba hakuna kesi.
2. Hati ya kiapo ya waleta maombi haikuwa na facts kama
inavyotakiwa badala yake ilikuwa imejaa maneno ya ubishi ubishi.
3. Mahakama haiwezi ku-entertain kusikiliza migogoro ya ndani
katika vyama vya hiari mf; vyama vya siasa, dini na michezo (ambavyo uanachama
wake ni wa hiari), kwa sababu mojawapo ya principle ni kwamba ili mtu awe
mwanachama anakuwa amekubaliana na katiba, kanuni, taratibu na makatazo ya
chama husika.
Aidha katika maombi yake kuna vitu vingine ‘muhimu’ ambavyo
mleta maombi amejikuta akivionesha kuwa anakubaliana na taratibu za chama
lakini wakati huo huo tena anataka mahakama imsikilize;
· Amekiri kuwa amevuliwa nafasi za uongozi na amekata rufaa
· Amekiri kuwa ameandikiwa mashtaka kwa maandishi na yeye
amejibu
· Amekiri kuwa ameandikiwa kuitwa mbele ya kikao cha Kamati
Kuu ili asikilizwe utetezi wake kwa mdomo.
Kwa maneno yake hayo ni kwamba anakubaliana na na process ya
chama na kwamba anajua atasikilizwa lakini tena wakati huo huo anataka mahakama
imsikilize. Huo ndiyo msingi wa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA kusema kuwa
kuhangaika huko ni sawa na kufanya ‘FORUM SHOPPING’.
Mleta maombi angeweza kuwa na hoja katika maombi yake iwapo
angeona kuna breach of natural justice kwenye suala lake. Kitu ambacho
hakijatokea na hata yeye kwenye maelezo yake anakiri hivyo.
Uamuzi wa Mahakama Kuu
Katika uamuzi wake, Jaji Utamwa amesema chama kitaendelea na
shughuli zake kama kawaida.
Hivyo kikao maalum cha Kamati Kuu kilichopangwa kufanyika
kesho Januari 3, 2014, kitafanyika na kitajadili agenda zote (kama
zilivyotolewa awali) na masuala yote yanayohusu uendeshaji wa chama, isipokuwa
hakitajadili na kuamua kuhusu uanachama wa Zitto pekee, hadi Mahakama Kuu
itakaposikiliza ombi lake kesho saa 3 asubuhi.
Kurugenzi Ya Habari CHADEMA
No comments:
Post a Comment