Utaratibu unaelekeza pale Rais
anapofanya uteuzi wa mawaziri hushauriana na Makamu wake na Waziri
Mkuu. Chanzo kimoja kilidokeza kuwa kikao baina ya viongozi hao wawili
kitaifa kilianza jana mchana. “Kaka nakueleza tu wakuu wamekutana na hivi
sasa ninavyoongea na wewe wanaendelea kujadili suala hilo ila sina uhakika
mabadiliko haya yatangazwa lini,” kilidokeza chanzo hicho. Alipoulizwa
kuhusu suala hilo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema: “Wananchi
watulie na kumpa nafasi Rais Kikwete kupanga safu yake ya mawaziri. Siwezi
kusema atatangaza lini kwa sababu siwezi kumpangia siku ya kutangaza baraza,
nadhani tusibiri tu mpaka siku atakapotangaza ndipo tutajua.” Aliongeza:
“Najua watu wana shauku kubwa lakini wanatakiwa kutulia tu muda mwafaka
ukifika, kila kitu kitawekwa wazi.” Balozi Sefue alisema uteuzi huo ni
mzito na unahitaji umakini na muda huku akigoma kutoa ufafanuzi baada ya
kuulizwa kuhusu kufanyika kwa kikao kati ya Rais na Makamu wake.
Uteuzi huo unafanyika
baada ya Desemba 20 mwaka jana Rais Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri hao
kutokana uchunguzi uliofanywa na kamati ndogo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Mazingira iliyoongozwa na James Lembeli. Ripoti ya Kamati Ndogo ya Bunge
ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyoundwa kuchunguza Operesheni Tokomeza
ndiyo iliwang’oa mawaziri hao baada ya kueleza athari zilisababishwa na wizara
nne walizokuwa wakiziongoza. Taarifa za Rais Kikwete na Bilal zimekuja wakati
kuna habari kuwa Rais amekutana mara mbili na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
takriban siku tano zilizopita kujadili suala hilo. Hata hivyo, Pinda jana
alikuwa mjini Dodoma ambako alikuwa anajiandaa kuelekea Kiteto mkoani Arusha
leo ambako kuna mapigano kati ya wakulima na wafugaji. Tangu aingie
madarakani Oktoba, 2005, Rais Kikwete amebadili Baraza lake la Mawaziri mara
tano, kutokana na kukaribia kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ni wazi kuwa uteuzi
atakaoufanya sasa utakuwa wa ustadi mkubwa.
Source: Butahe F. ( Jan. 2014).
Baraza la mawaziri koto nyuzi 100. Retrieved from Mwananchi
No comments:
Post a Comment