-
Kuitisha mkutano wa wabunge, Baraza la Wawakilishi
MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Salim Ahmed Salim, ameonja joto ya jiwe ndani ya kikao cha Kamati Kuu (CC), ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakitaka atoe ufafanuzi wa namna walivyoleta tena hoja ya serikali tatu kwenye rasimu ya pili ya Katiba. Hali hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Zanzibar wakati wa kikao cha CC, kilichoitishwa pamoja na mambo mengine, kupitisha jina la mgombea ubunge katika Jimbo la Kiembesamaki, kuziba nafasi ya Mwakilishi wa jimbo hilo, Mansoor Yussuf Himid, aliyevuliwa uanachama mwaka jana. Salim ambaye amepata kuwa Waziri Mkuu, kwa sasa ni mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba yenye msimamo wa serikali tatu, lakini pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, ambayo ina sera na msimamo wa serikali mbili.Kutokana na nafasi hizo mbili, zenye misimamo tofauti kuhusu mabadiliko ya Katiba, mwanasiasa huyo mkongwe na mwenye historia nchini amejikuta kwenye wakati mgumu anapokuwa kwenye vikao vya CC yenye msimamo wa serikali mbili na anapokuwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, inayosimamia hoja ya serikali tatu. Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kuwa baadhi ya wajumbe wa CC walimshambulia Salim kwa madai kuwa anajua msimamo wa CCM kuhusu muundo wa serikali, lakini ameshindwa kuitetea hoja hiyo mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba iliyokuja na mapendekezo ya serikali tatu. Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kulikuwa na mnyukano mkali wa hoja za kisiasa kupinga mapendekezo ya rasimu ya pili ya mabadiliko ya Katiba.Kila mjumbe aliyesimama alizungumza kwa jazba na kumbebesha lawama Salim na Jaji Warioba, kwamba tume yao imependekeza hoja ambayo si sera ya CCM na ina lengo baya na chama. Habari zaidi zinasema kuwa CCM imepitisha azimio la kuitisha mkutano mkubwa wa wabunge wote wa CCM, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba watakaoteuliwa na Rais Kikwete ili kuweka msimamo kuhakikisha hoja ya serikali tatu inafia kwenye Bunge la Katiba. Kwa muundo wa Bunge la Katiba, CCM itakuwa na wajumbe wengi, hivyo uwezekano wa msimamo wa chama chao kupita ni mkubwa. Habari zaidi zinasema wakati wajumbe wa CC wakimshambulia Salim, hakusema wala kujibu chochote kutetea chama au kusimamia msimamo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisisitiza kuwa kamwe CCM haijabadili msimamo wake kutetea mfumo wa Muungano wa serikali mbili ulioasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na hayati Sheikh Abeid Amani Karume mwaka 1964. Nnauye alisema chama chao kinatambua kuwa Tume ya Jaji Warioba imependekeza mfumo wa serikali tatu na kusema pendekezo hilo si sera ya chama tawala na wanachama wake. Nape aliwaambia waandishi wa habari kuwa muundo wa serikali mbili utabaki kuwa msimamo wa CCM na hadi sasa hakuna kikao chochote cha kikatiba kilichokaa na kubadili msimamo huo hadi pale vikao vya kikatiba vitakapoamua.“Tutalisema kwa uwazi na hatutamuogopa mtu wala kumng’unya maneno kwa manufaa ya wananchi na taifa letu,” alisema Nape. Tangu Jaji Warioba kutangaza rasimu ya pili ya Katiba kumejitokeza tofauti za kimsimamo kati ya vyama vya CCM na CUF, huku CCM wakitaka mfumo wa serikali mbili uendelee na CUF wakiunga mkono mapendekezo hayo. Kamati Kuu ya CCM imempitisha Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa jimbo hilo la Kiembesamaki kuziba nafasi ya Mansoor Yussuf Himid, aliyevuliwa uanachama mwaka jana. Tayari mgombea huyo ameshachukua fomu katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar na uchaguzi mdogo unatarajiwa kufanyika Februari mwaka huu visiwani hapaSource: Ame H. (Jan. 2014). Salim ailiza CCM. Retrieved from Tanzania Daima
Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com ------Nguvu Ya Umma-----On Twitter @ChademaDiaspora
Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------
Thursday, January 16, 2014
Salim ailiza CCM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment