Kwenye barua ya
kujiuzuru mwenyekiti wa Singida amemtaja Tundu Lissu kuwa sehemu ya wavamizi
wanao iua CHADEMA haya ndio majibu ya TUNDU.
Soma majibu ya Tundu Lissu hapa;
Kwa vile
aliyejiuzulu ni Mwenyekiti wangu wa Mkoa, na kwa vile amenituhumu specifically
kuwa ni mmoja wa 'wavamizi' ndani ya CHADEMA ambao ndio 'vinara' wa migogoro
ndani ya chama chetu, nafikiri nitasemehewa nikiweka utetezi wangu hapa
jukwaani.
Wilfred Kitundu
is probably the longest serving regional chairman wa CHADEMA katika nchi hii.
Na ni kweli, Kama anavyosema, kwamba kwa muda wa karibu miaka ishirini ya
uenyekiti wake, sebule ya nyumba yake ilikuwa ndio Ofisi ya chama ya Mkoa.
Which is another way of saying, kwa miaka yote hiyo, chama hakikukua.
CHADEMA haikuwa
na Mwenyekiti wa kitongoji, wala wa kijiji, wala Diwani, achilia mbali Wabunge.
In fact, viongozi wetu wa kwanza wa kuchaguliwa - wenyeviti wa vitongoji na wa
vijiji - walichaguliwa mwaka 2009, mwaka mmoja baada ya mimi kuvamia na/au
kuhamia CHADEMA Singida. Mwaka 2010 tulipata, kwa Mara ya kwanza tangu mungu
aumbe mbingu na nchi, Wabunge na Madiwani wasiokuwa maCCM.
Sitaki
kujisemea sana katika hili, lakini nafikiri mchango wangu katika kuijenga
CHADEMA Singida ni mdogo. On the other hand, zaidi ya kutuwekea Ofisi ya Mkoa
sebuleni kwake, sidhani kama Mzee Kitundu ametoa mchango mwingine wowote katika
mafanikio haya. Zaidi ya kula pesa zetu za kampeni ya udiwani katika Kata ya
Urughu mwaka 2011 wakati wengine tukiwa kwenye mapambano ya uchaguzi mdogo wa
Igunga, sidhani kama nitakuwa namsingizia Mzee huyu nikisema kwamba hatujamwona
akishiriki kwa maana yoyote katika harakati za kisiasa za CHADEMA Singida. Mtu
aliyemwokoa kutokana na hasira ya wanachama baada ya kula hela za kampeni kata
ya Urughu ni ....... Jaza mwenyewe!!!
Mwaka huo huo
wa uchaguzi, kulikuwa na skandali ya mgombea ubunge wetu wa Singida mjini
kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi kwa maelekezo ya Mh. Zitto Kabwe.
Mtu aliyetumiwa kuweka pingamizi ili mgombea wetu aenguliwe alikuwa wakati
Mwenyekiti wa CHADEMA Singida mjini Wazaeli Nakamia. Tulipambana hadi
tukamrudisha mgombea wetu kwa kushinda rufaa kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mzee Kitundu hakuwahi kusema chochote, either way, kilichokuwa kinaendelea kwa
sababu Mhusika Mkuu wa skandali hiyo, kama alivyo Mhusika Mkuu aka MM wa
Mkakati wa Mapinduzi 2013, alikuwa mfadhili wake yaani Zitto Kabwe.
CHADEMA imekuwa
sana katika Mkoa wa Singida tangu 2010. Kwa kiasi kikubwa, pengine kuliko mtu
mwingine yeyote katika Mkoa wetu, ni mvamizi na mhamiaji Tundu Lissu. I can say
with a straight face kwamba Jimbo pekee ambalo sijawahi kufanya mikutano ya
hadhara ni Iramba Magharibi. Mengine yote nimefanya mikutano ya hadhara hata
kabla sijawa Mwenyekiti wa M4C Kanda ya Kati.
In brief,
naweza kusema, as a matter of fact, kwamba Mzee Kitundu amejiuzulu kwa sababu
mfadhili wake ameng'olewa madarakani na Kamati Kuu. I also can say with clear
conscience kwamba Mzee Kitundu ataondoka peke yake CHADEMA Singida. Hana
following yoyote Mkoa ule. Hata mkutano wa Mtaa hawezi kuitisha akapata watu.
Kuondoka kwake ni good riddance, at least inatupunguzia mizigo ambayo tumeibeba
kwa miaka mingi!
One final
point: kwa vile amemtaja marehemu Chacha Wangwe kama mmoja wa wasaliti
waliong'olewa CHADEMA siku za nyuma, ni vizuri wananchi wafahamu kwamba Mzee
Kitundu, kama Zitto Kabwe, alikuwa mmoja wa Wajumbe wa Kamati Kuu
'iliyowaaminisha' Watanzania kwamba Chacha Wangwe alikuwa msaliti mwaka 2007! Kama
anabisha mwuulizeni jamaa yake anayempigania sasa hivi!
Kama ilivyo
katika historia ya mapambano ya ukombozi ya zama zote, hakuna mapambano
yasiyokuwa na akina Yuda Iskariote wake, yaani wale wanaosaliti cause kwa
vipande thelathini vya fedha! Haijaanza jana wala juzi. Na haitaisha kesho.
Kitu muhimu zaidi ni kwamba wasaliti wa aina hii hawajawahi kuzuia jua la haki
kuchomoza na giza la ufisadi na uonevu kutoweka. Haitakuwa tofauti kwa CHADEMA.
We, too, shall overcome. Tutashinda. Kama anavyosema mwanafasihi Shaffi Adam
Shaffi katika kitabu chake Kuli: 'Yana mwisho haya'!
Tundu
Lissu
No comments:
Post a Comment