ZIARA YA KATIBU MKUU DKT. WILLIBROD SLAA
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt.
Willibrod Slaa ataanzaziara ya siku 20 katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma,Tabora na Singida kuanzia Desemba 4/23, mwaka huu. Lengo la ziara hiyo ambayo imetokana na maombi yamuda mrefu ya viongozi wa chama katika maeneohusika, ni kuimarisha na kukagua uhai wa chamakatika ngazi za chini hususan kata na majimbo mikoahiyo.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakutana nawananchi katika mikutano ya hadhara ambapoatazungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa na eneohusika, kisha atafanya vikao vya ndani vya kichama. Ziara hiyo itaanzia mkoani Shinyanga ambapo siku yaJumatano Desemba 4, mwaka huu, Katibu Mkuu Dkt.Slaa atakuwa Wilaya ya Kahama, siku inayofuataDesemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo laBuyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo laMuhambwe. Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwavyombo vya habari.
Imetolewa leo Jumanne, Desemba 3, 2013, Dar esSalaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA
No comments:
Post a Comment