Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, December 16, 2013

Dk. Mengi:Waziri Muhongo amedanganya



Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, amesema madai yaliyotolewa dhidi yake na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, hayana ukweli wowote. 
Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na wahariri kufafanua kauli mbalimbali, ambazo zimekuwa zikitolewa na waziri huyo dhidi yake. Dk. Mengi alisema  Septemba, mwaka huu, Profesa Muhongo alinukuliwa akisema kwamba, Mengi hana uzawa, bali ana ubinafsi na anataka kufanya udalali wa vitalu vya rasilimali za Watanzania. “Profesa Muhongo alisema hivi namnukuu: “Mengi hana uzawa, bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu,” Alisema yeye siyo mbinafsi na pia hajawahi kuomba upendeleo wa kupewa kitalu cha gesi, bali anapigania Watanzania kwa jumla. Aidha, Dk. Mengi alisema Desemba 8, mwaka huu, alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Waziri Muhongo alitoa takwimu zinazomhusu, ambazo siyo sahihi.

        “Ukweli ni kwamba, mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita moja ya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema,” alisema Dk. Mengi. Aliongeza: “Naomba nisisitize kwamba, mimi binafsi nimeshapata nafasi kubwa ya kujiendeleza kibiashara. Ukweli ni kwamba, ninachopigania leo ni juhudi ya kupanua wigo ili Watanzania wengi waweze kushiriki kama ilivyo kwenye Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004, ambayo inatoa upendeleo maalumu kwa Watanzania katika rasilimali zao.” Alisema sekta binafsi itapata nafasi ya kipekee leo ya kuwa na mkutano, ambao mwenyekiti wake atakuwa Rais Jakaya Kikwete.  Alisema yeye binafsi atapata heshima ya kushiriki kama kiongozi wa sekta binafsi chini ya TPSF, hivyo aliona kuna haja ya kufafanua madai yaliyotolewa na Waziri Muhongo kumhusu ili asiende kwenye kikao cha leo zikiwapo fikra kwamba, mambo hayo ni ya kweli. “Nina matumaini makubwa kwamba, katika mkutano wa kesho (leo), ambao utatoa fursa kwa sekta binafsi kuzungumza na uongozi wa Taifa chini ya uenyekiti wa rais utatuwezesha kupata muafaka wa jinsi gani tutashirikiana katika juhudi za kuwawezesha Watanzania kwenye nyanja mbalimbali za uchumi wetu,” alisema Dk. Mengi.


Source: Ippmedia (Dec. 2013). Dk. Mengi:Waziri Muhongo amedanganya. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: