Selemani
Msindi (Afande Sele) Jumamosi hii, akihutubia mamia ya wananchi wa Kata ya
Kichangani, jimbo la Morogoro Mjini, aliwahakikishia wanachi, kama
watashikamana na kusiliza maneno ya busara yanayotolewa na viongozi wa CHADEMA,
basi lazima CHADEMA itachukua madiwani wengi na nafasi ya ubunge, Jimbo la
Morogoro Mjini. Alieleza sababu za wanamziki wenye upeo mkubwa kuingia katika
siasa, kwamba wanasiasa wameziba masikio na hawataki kusikiliza jumbe zao
kupitia muziki.
Kabla ya kupanda jukwaani alikanusha kabisa, kushiriki katika
kuikosoa kamati kuu ya CHADEMA na maamuzi yake, kwani yeye anaipenda CHADEMA,
Muundo wake, Katiba na vikao vyake, na hana muda wa kuzungumza mambo
yaliyowekwa katika mitandao, yakimhusisha na kauli zisizo za kweli, eti kwamba
analaani uamuzi wa kamati kuu. Alisema hizo ni njama zinazopangwa kumchonisha
na chama anachokipenda, na kamwe hazitafanikiwa. Kazi imeanza na sasa hakuna
kulala mpaka kieleweke. Angalia picha hapa chini.


No comments:
Post a Comment