Tangu kumalizika kwa vikao vya
Kamati Kuu ya CHADEMA, iliyoketi kwa siku mbili mfululizo Novemba 20-21, mwaka
huu, kisha maazimio yake kutolewa kwa wanachama na umma wa Watanzania siku ya
jana, kumeanza kuibuliwa propaganda nyingi zenye makusudi maalum.
Ni wazi kuwa hatuwezi kukimbizana
na wapika propanda (rumourville is back?), kwa kujibizana nao kwa kila
wanachokisema. Itakuwa ni kufanya kazi wanazotaka wao tufanye badala ya
kuendelea kutekeleza majukumu ya kuimarisha taasisi na mifumo, hasa katika
wakati huu ambapo CHADEMA inaendelea kutimiza wajibu mkubwa kwa wanachama wake
na Watanzania wote kwa ujumla.
Pamoja na kwamba propaganda hizo
nyingi zinapuuzwa, si kila upuuzi unaweza kupuuzwa. Mathalani zimeenezwa habari
za uongo kuwa Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse amekuwa Makamu
Mwenyekiti Bara, Mbunge wa Iringa Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu, Peter Msigwa
ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara na Prof. Mwesiga Baregu, amejiuzulu
nafasi yake ya ujumbe wa Kamati Kuu.
Kwa mtu makini, ukisikia na
kuzisoma propaganda hizo katikati ya maneno kama si mistari, mara moja
unang'amua zinalenga kitu gani. Kwa sasa si lazima kuingia undani wa malengo
hayo, lakini ni vyema ikajulikana kuwa yanajulikana tayari. Hazitafuzu.
Tunatambua kuwepo kwa watu wa CCM,
wakiwemo viongozi wa juu kabisa wa chama hicho, wanaoonekana eti 'wanaipenda'
CHADEMA leo ghafla, wanahusika katika kueneza uongo na propaganda hizo. Bila
shaka ni dalili ya kushindwa kushughulika na mambo yao (ufisadi, kujivua gamba,
kukataliwa na wananchi, n.k), kiasi wanapata muda wa 'kujali' ya wengine.
Tunajua wanatishika na namna
ambavyo CHADEMA inaendelea kujiimarisha (huku wao wakizidi kukataliwa), kupitia
CHADEMA ni msingi na Operesheni ya M4C, kupitia kanda za chama na kazi nyingine
zinazeondelea yakiwemo mafunzo kwa viongozi.
Wanachama makini wa CHADEMA na
Watanzania kwa ujumla wanaoamini kwa dhati katika mapambano ya mabadiliko
ambayo chama hiki kimeyasimamia consistently, bila kuyumba, kikionesha kila
sifa ya kuwa mbadala wa status quo ya CCM, wataendelea kusikiliza chama chao
kinasema nini (hasa kupitia maamuzi ya vikao), kuhakikisha nguvu ya mshikamano
wa pamoja inaendelea kuwa ndiyo nguzo imara ya mafanikio kwa ajili ya haki nha
matumaini ya Watanzania.
Propaganda za hivi sasa, kama
ambavyo zimeshindwa zote zingine, hazitawaondoa katika mstari wanachama na
Watanzania wenye matumaini makubwa na CHADEMA kuwa ni chama mbadala chenye
kujenga uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganaizesehni tahibiti,
mijini na vijijini kwa ajili ya kutoa utumishi bora kwa wananchi.
Tumaini Makene
Afisa Habari CHADEMA
0752 691569
No comments:
Post a Comment