Dr. Slaa anaendelea na safari yake ya kujifunza inayoitwa “Vision
Tanzania” ambayo leo imemfikisha katika kituo kikubwa cha Umeme kinachoitwa
Alabama Power Company ambayo inatenegenza umeme wake kutokana na jua, gesi
asilia, makaa ya mawe, upepo, jua, takataka, (biomass) pamoja na nuklia Akielezea baadhi ya shuguli za Alabama Power company, mkurugenzi
wa shirika hilo linalojitegemea, ameeleza kwamba shirika hilo linawahudumia
wateja million nne tu, huku ikizalisha kiasi cha megawati 48,000 (4.8GW) Tangu
kuanzishwa kwa shirika hilo, hakujawahi kutokea mgao wa umeme au umeme kuzimwa
hata kwa dakika 5. Panapotokea dharura, kuna kuwepo njia mbadala ya kukabiliana
nayo,
|
Dr. Slaa na ulinzi wake wakiwasili katika ofisi za Shirika la Alabama Power Company |
|
Mkurugenzi mkuu akimpokea Dr. Slaa na Mkewe |
Kwa upande wake, Dr. Slaa amejifunza na kugundua kitu kimoja
kwamba, watanzania wanaumia kutokana na wachache kuligeuza Tanesco kuwa mradi
wao. Dr. Slaa anaamini kwamba mgao tulionao Tanzania, ukosefu wa umeme tulionao
ni matunda ya ufisadi wa CCM. Kiongozi huyo anaamini kwamba tatizo ni ccm na
desturi yao ya kulindana. ilahali tunatengeneza 600MW huku Waziri Muhongo
akidai mwakani tutauza umeme nje ya nchi. Umeme gani wa kuuza nje ya nchi
wakati 80% ya watanzania hawana umeme? Huyu mtu yuko katika sayari gani? Miaka
52 ya ufisadi, kugawana vyeo kindugu, umasikini na magonjwa sasa tuseme basi.
CCM hawawezi kujidai kwamba watatatua matatizo ya watanzania Viongozi wakuu Wizarani na Tanesco wanawazuia na kuwadhalilisha
wawekezaji kwa manufaa yao binafsi na makampuni yasiyokuwa na huruma na
mwananchi wa kawaida. Njia pekee ya kumuokoa mtanzania, ni mtanzania mwenyewe
kuamka, na kumng’oa adui CCM kupitia njia ya kura. Mtanzania asifanye kosa tena
2015. Lazima amn’goe CCM ili apate umeme na kuweza kuboresha maisha yake
Akitembelea mitambo inayopewa ulinzi wa kipekee, Dr. Slaa
amejionea jinsi kampuni hiyo inavyofanya shuguli zake pamoja na kuwa na mitambo
ya kisasa inayo monita njia zote za umeme kusini mwa marekani yaani, Georgia,
Florida, Alabama, Mississini na South Carolina. Mkurugenzi wa shirika hilo, amemuahidi Dr. Slaa kwamba wako
tayari kuja Tanzania na kuisadia nchi hiyo kuboresha uzalishaji, usambazaji
pamoja na uendeshaji ikiwa serikali itawahitaji, kwani wameisadia nchi za
Philippines na Kuwait ambazo hadi sasa wanazo umeme wa uhakika.
|
Mkurugenzi wa shirika akimpa maelezo Dr. Slaa jinsi shirika hilo linavyofanya kazi |
|
Sehemu maalum yenye ulinzi mkali ambako gridi inakuwa monitored |
|
Dr. Slaa akitizama kwa umakini mitambo hiyo ya kusisimua inayoongoza gridi kusini mwa marekani.Hata mashine moja ikiharibika watagundua maramoja na kuweza kutafuta njia mbadala |
|
Dr. Slaa akikabidhiwa kitabu na mwanasheria mkuu wa shirika hilo |
No comments:
Post a Comment