Ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa kiafrika kupewa mapokezi
makubwa ambayo Dr. Slaa ameyapokea katika ufunguzi wa mchezo wa mpira maarufu
kama football. Dr. Slaa alialikwa na Chancellor pamoja na Rais wa chuo kikuu cha
Alabama kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo baina ya Alabama na Georgia State.
Kiongozi huyo wa Chadema alipokewa na viongozi wa ngazi mbali mbali wa kitaifa
na wa jimbo la Alabama. Akimkaribisha Dr. Slaa katika chakula cha asubuhi iliyoandaliwa
kwa ajili yake, Chancellor wa chuo hicho, amemfananisha Dr. Slaa na Nelson
Mandela kutokana na juhudi zake za kupambana ufisadi nchini Tanzania. “Tunajua jinsi polisi wanavyowaua raia na kuwakamata wapinzani”
alisema kiongozi huyo. Kadhalika kiongozi huyo amemsifu Dr. Slaa kutokana na
msimamo wake, sera zake za kulikomboa Tanzania kutoka katika umasikini licha ya
chama chake kutungiwa kesi za ughaidi.
Kwa upande wake, wakiwa kama moja ya vyuo vikuu nchini marekani,
wako tayari kufanya kazi kwa ukaribu na Dr. Slaa hasa katika sekta ya elimu.
Wamemuomba ajisikie nyumbani na kufurahia mchezo wa American football. Kwa unyenyekevu Dr. Slaa aliwashukuru governor, na viongozi
wengine kwa kuwa wakarimu sana kwake na mkewe na watu wa Tanzania.
Amefurahishwa jinsi wamarekani wanavyokuwa na hamasa na kuipa kipaumbele
michezo. Nimejifunza kwamba michezo ni moja ya mbinu ya kuiunganisha
taifa hasa tunapokuwa na changamoto nyingi kama za kwetu alisema Dr. Slaa.
Kadhalika amesema kwamba, chama chake cha Chadema ina sera ya kukuza vipaji
kupitia taasisi za michezo nchini Tanzania na siyo kuwaleta Makocha wa kigeni,
mmoja baada ya mwingine na kuwapeleka Ikulu kula pilau na kupiga picha. Nilichojifunza ni kwamba, lazima nirudi na ujumbe kwa watanzania
kuweka mifumo endelevu ya michezo kuanzia shule za misingi hadi vyuoni.
Nilichoona hapa ni mfano wa kuigwa alimalizia Dr. Slaa.
|
Msafara wa Dr. Slaa ukiwasili uwanjani |
|
Dr. Slaa na Senator Shelby wakibadilishana mawazo wakielekea uwanjani |
|
Watu wa kila aina mashuhuri walifika kumsalimia Dr. Slaa |
|
Dr. Slaa na Mkewe wakilakiwa na Rais wa Chuo |
|
Watoto nao walijitokeza kumsalimia na kupiga picha na mgeni mashuhuri Dr. Slaa |
|
Dr. Slaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi ya Masenators walioalikwa kujumuika naye |
|
Moja ya Viongozi wa Juu Nchini Marekani |
|
Moja wa mamea mashuhuri marekani akimsalimia Dr. Slaa |
|
Dr. Slaa akikaribishwa Ukumbuni kwenye Chakula cha Asubuhi iliyoandaliwa kwa ajili yake |
|
Watu wengi mashuhuri walioalikwa walimiminika kusalimiana na Dr. Slaa |
|
Uwanja ulijaa hasa. Watu zaidi ya laki moja walihudhuria |
|
wakiwa katika chumba cha watu mashuhuri. Baadhi ya watu mahuhuri kama yeye hawakujizuia kwenda kumsalimia. Akifungua mchezo wa leo, Dr. Slaa alirushwa moja kwa moja na moja ya luninga kubwa zaidi nchini marekani |
|
Dr. Slaa na Gavana |
|
Viongozi Mashuhuri wakiwa uwanjani kabla ya mchezo kuanza. Dr. Slaa ndiye mgeni Rasmi. Hapa ni chumba maalum cha rais kwa ajili ya wageni mashuhuri |
|
Mshindi wa Nobel Peace Price na Dr. Slaa ndani ya Chumba cha watu mashuhuri wakijadili neno |
|
Dr. Slaa akisalimiwa na mmoja wa US congressmen waliohudhuria mchezo |
No comments:
Post a Comment