Akiwa anaendelea na ziara yake nchini Marekani, siku ya ijumaa
katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dr. Wilibrod Slaa
alitembelea Chuo kikuu cha tiba cha Alabama ambako alilakiwa na viongozi wa juu
wa chuo hicho
Chuo kikuu cha Alabama ina wanafunzi 16,000 katika Kitengo cha
tiba. Hii ndio moja ya vyuo vikubwa nchini marekani katika maswala ya tiba, ikiwa
na vitengo karibia vyote vinavyotibu magonjwa mbali mbali. Chuo hicho pia
ufanya utafiti nchi nyingi duniani husasan afrika. Chuo hicho ushirikiana na
nchi kama Afrika kusini, Zambia, Malawi, na Aljeria katika mambo ya utafiti na
kutayarisha watafiti. Kadhalika imekuwa ikisaidia mataifa kama Saudi Arabia,
Uchina na Qatar kutayarisha madaktari bingwa
Ikiwa ni moja ya sera za chama cha demokrasia na maendeleo
CHADEMA kuweka mikakati ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya huduma bora za afya
kwa watanzania, Dr. Slaa Amekuwa akizunguka nchini marekani ili kujifunza mambo
mbali mbali hasa mafanikio ya vyuo kama hivi, na ni jinsi gani anaweza kupata
ushirikiano na vyuo hivi ili kutayarisha madaktari wengi wa tiba na mabingwa
ili kuiokoa taifa gharama kubwa ya kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi.
Kujibu ombi la Dr. Slaa, rais wa chuo cha tiba, ameahidi
kushirikiana na serikali ya Tanzania chini ya CHADEMA ili kujenga vyuo vya
utafiti na tiba nchini Tanzania. Viongozi hao wameweka bayana nia yao ya
kuisaidia Tanzania hasa ufisadi na urasimu uliopo utaondolewa. Naye kwa upande
wake, Dr. Slaa amemuahidi kwamba, ufisadi utakuwa ni historia katika serikali
ya CHADEMA.
Chuo hicho itakuwa tayari kuwatuma madaktari wake bingwa wa kila
aina nchini Tanzania kusaidia katika mambo mbali mbali ya tiba itakayoambata na
makubaliano na serikali ya CHADEMA ikiwemo kuwafundisha na kuwatayarisha
madaktari 4,000 katika kipindi cha miaka (accelerated program) miwili kama
walivyofanya nchini Bangladesh ili kupunguza uhaba wa madaktari. Hawa ni
madaktari wasaidizi ambao wanaujuza Fulani. Madaktari wengine watahitaji miaka
mitatu ili kuwa madaktari bingwa.
Dr. Slaa pamoja na viongozi wa Chuo cha Tiba
Dr. Slaa na Dean wakiwa kwenye maongezi ya kufanya kazi pamoja
Dr. Slaa akipewa maelekezo na rais wa chuo cha Tiba
Dr. Slaa akielekezwa kwenye chumba cha Mikutano na rais wa chuo cha tiba
Dr. Slaa akiongozwa na Professor ambaye pia ni dean msaidizi |
No comments:
Post a Comment