Kamanda Zellothe Stephen akionesha CD za mafunzo ya kijeshi zilizokuwa zinatumiwa na kundi hilo. |
POLISI
mkoani Mtwara inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kupata mafunzo ya kijeshi
msituni kwa kutumia CDs za al-Shabaab. Tukio
hilo la aina yake limetokea katika mlima Makolionga wilaya ya Nanyumbu mkoani
hapa ambapo pia CDs zenye mafunzo mbalimbali ya kijeshi 25 zimekamatwa. Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen ameuambia “mtandao wa Kusini Leo”
kuwa watuhumiwa hao walikamatwa
wiki moja iliyopita baada ya jeshi lake kupata taarifa kutoka kwa wasamaria
wema: “CD hizo zilikuwa zinatoa mafunzo ya Al-Shabaab ya kuchinja watu,
Mauaji wa Osama Bin Laden, Zindukeni Zanzibar, Kuandaa Majeshi, Mauaji wa Idd
Amin na Mogadishu Sniper,” alisema Stephen.
Alisema
watuhumiwa wote ni wakazi wa wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa na kwamba walikuwa
wakiongoza na Mohamed Makande 39, mkazi wa kijiji cha Sengenya ambaye pia
anashikiliwa na jeshi hilo. Aliwataja
wengine waliokamatwa kuwani Hassan Omary (39) mkazi wa kijiji cha Nanyulu,
Rashid Ismail (27). Abdallah Y. Hamisi (32), Salum Wadi (38), Fadhili Rajabu
(20), Abbas Muhidini (32), Ismail Chande (18), Said Mawazo, Issa Abeid (21), na
Ramadhani Issa (26) wote wakazi wa kijiji cha Likokona.
Kuhusu
vitu watuhumiwa walivyokamatwa navyo, Kamanda Zelothe alisema, “Tumekamata
mapanga mawili, Deki ya DVD, Solar, Visu, Tochi, Betri, Simu za kiganjani 5,
Vyombo mbalimbali vya kulia chakula, Baiskeli tatu, Vitabu mbalimbali wa dini
ya Kiislam, Unga wa mahindi kilo 50, Mahidi kilo 150 na virago vya kulalia.
Vingine ni mfuko wa kijani unaosadikiwa ni wa kijeshi wenye nembo ya nanga ya
meli yenye mistari kulia na kushoto na nyoka katikati.” Alisema
jeshi lake licha ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani, linaendelea na uchunguzi
wa kina kwa kushirikiana na Polisi Makao Makuu kwa lengo la kufanikisha kuunasa
mtandao mzima.
No comments:
Post a Comment