Katibu mkuu wa Chadema Dr. Willibrod Slaa katika ziara yake
nchini Marekani iliyoandaliwa na umoja wa vyuo vikubwa nchini humo ya kujifunza
mambo mbali mbali, imemfikisha leo katika jimbo la Alabama na kupokelewa na
wakuu wa jimbo hilo akiwemo Gavana pamoja na Waziri wa biashara.
Alabama ni moja ya majimbo yaliyokuwa nyuma sana kiuchumi na
kimaendeleo siku za nyuma. Uchumi wake ulitegemea kilimo kwa 90%. Miaka 25
iliyopita, viongozi wake walibuni mikakatati ya kulibadilisha. Leo, Jimbo la
Alabama ndio moja ya majimbo yenye viwanda vikubwa vya magari kama Honda,
Mercedes Benz, Airbus, Hyundai, Raytheon, Space station, Wallgreens na
mengineyo Uchumi wake unakua kwa kasi kubwa.
Kupitia kauli mbiu yake ya “Vision Tanzania” Dr. Slaa
alipata kukutana na viongozi wa jimbo hilo ili aweze kujifunza mbinu ambayo
ataweza kuwarudishia watanzania ili nao waondokane na umasikini. Licha ya yote,
Gavana wa jimbo hilo pamoja na mawaziri wake, wako tayari kushirikiana na
Tanzania kwenye mambo ya biashara hasa miundombinu ikiwemo bandari, ujenzi wa
madaraja na bandari. Dr. Slaa na mkewe Josephine walipokelewa na Gavana pamoja
na mawaziri wake
![]() |
Uongozi wa jimbo na Dr. Wakila chakula cha mchana iliyotayarishwa kwa ajili yake |
![]() |
Dr. Slaa akimshukuru mmoa wa askari waliokuwa wakiongoza msafara wake |
![]() |
Dr. Slaa, gavana na mawaziri wake wakiwa katika mjadala wa ushirikiano |
![]() |
Dr. Slaa akiwasili kwenye gavernor mansion baada ya kupokelewa na Waziri wa Biashara pamoja na Waziri wa mambo ya nje |
![]() |
Dr. Slaa Akimkabidhi Waziri wa Biashara Sera za Kiuchumi za Chadema |
![]() |
Dr. Slaa kwenye picha ya pamoja na gavana |
Kubwa ya yote alichojifunza Dr. Slaa ni kwamba, serikali inaweza
kuwa na ufanisi hata ikiwa na baraza dogo. Jimbo la Alabama lina Mawaziri sita
tu, huku CCM ikiwapa walipa kodi wa tanzania mawaziri 70 wasiokuwa na kazi.
Wengi wao wakiwa na matumizi makubwa huku wakina mama wakijifungua sakafuni,
walimu wakinyimwa haki zao, polisi na wanajeshi wakiishi hali duni na wanafunzi
wakisoma chini ya miembe. CCM ni janga kubwa lililowakumba watanzania
Chuo Kikuu Cha Kilimo Auburn
Kadhalika Dr. Slaa ametembelea chuo kikuu cha auburn ambayo ni
moja ya vyu vikuu vikubwa zaidi vya utafiti duniani. Auburn Inafanya shuguli
zake nchini Kenya, Uganda, Senegal na kwingineko barani Afrika. Nchini Kenya,
chuo cha auburn inawasaidia wakulima mbalimbali hasa wafugaji wa samaki na
technologia za kisasa inayowawezesha kusafirisha samaki wengi kwenda ulaya
Ulaya. Kati ya Kenya na Uganda, utafiti wao umetoa zaidi ya ajira 7000.
Walipoulizwa kwa nini walikwepa Tanzania, hawakuficha ukweli.
Walinena kwamba ni vigumu sana kufanya kazi Tanzania. Ufisadi uliwazuia ingawa
wangekuja na fedha zao kutoka benki ya dunia na shirika la kimarekani la USAID
ambayo inadhamini miradi yao sehemu nyingi barani Afrika ikiwemo Kenya na
Uganda. Viongozi wa chuo hicho wako tayari kurudi Tanzania ikiwa mazingira ya
kazi yatabadilika hasa kukiwepo na serikali mbadala, ambayo Mh. Slaa amewahakikishia
kwamba Chadema hiko tayari kufanya nao kazi.
Viongozi wa Auburn University wako tayari kusaidia vyuo vya
Tanzania kama Sokoine kwa kuwafundisha waalimu na pia kubadilishana nao
technolojia za kisasa za kilimo. Wako pia tayari kuwafundisha wakulima wa aina
zote na hata walaji mbali mbali mbali.
![]() |
Dr. Slaa akiwasili chuo kikuu cha Kilimo Cha Auburn. Nyuma yake ni walinzi kwenye msafara wake |
![]() |
Dr. Slaa akilakiwa na Dean wa Chuo cha Kilimo pamoja na viongozi wengine wa juu wa chuo hicho |
No comments:
Post a Comment