Dr. Slaa anaendelea na safari yake ya kujifunza inayoitwa “Vision
Tanzania” ambayo leo imemfikisha moja ya bandari kubwa nchini marekani.
Bandari ya Mobile Alabama ambako alipokelewa na mkurugenzi wa Shirika la
Alabama Ports Authority
Shirika la Alabama Ports Authority inapitisha makontena 100 kwa
lisaa limoja na mizigo inayozidi tani million 30 kwa mwaka na kuipa shirika
hilo linalojitegemea kiasi cha dola za kimarekani million 152 kwa mwaka ambazo
ni faida. Shirika hilo lina wafanya kazi 600 tu, lakini imeweza kutoa ajira
ambazo siyo za moja kwa moja 280,000.
Bandari ya Alabama inajitegemea kiuendeshaji; haliingiliwi na
uongozi wa jimbo. Utekelezaji wa bandari hii ni wa kipekee kwa sababu mizigo
uondoka bandarini punde tu zinapowasili au chini ya siku tatu. Alichojifunza
Dr. Slaa katika ziara hii ni kwamba, mashirika ya umma yanaweza kufanya kazi
kwa ufaninisi mkubwa pasipo uingiliaji wa kisiasa.
Dr. Slaa pia amejifunza kwamba, kama jimbo dogo kama Alabama
inaweza kupitisha tani million 30 kwa mwaka, basi Tanzania inaweza kupitisha
tani million 100 kwa mwaka kutokana na jiographia yake. Dr. Slaa anaamini
kwamba Bandari ya Tanzania inaweza kuajiri vijana 350,000 chini ya utawala wa
Chadema.
Dr. Slaa anaamini kwamba, mashirika ya umma kama bandari hayana
ufanisi kwa sababu waendeshaji wake wanateuliwa kiurafiki na kindugu bila ya
kuzingatia uwezo wa mtu. China ya utawala wa Chadema haya yote yatafikia kikomo
kwa manufaa ya watanzania wanaoumia na umasikini
 |
Dr. Slaa Akipokelewa na Mkurugenzi wa Mkuu wa Bandari ya Mobile Alabama |
 |
Mashine nzito bandarini ikishusha mizigo |
 |
Mkuregenzi mkuu wa Bandari akitoa maelezeo kwa Dr. Slaa |
 |
Mashine (crane) zinazotumika kunyanyua kontena |
 |
Sehemu maalum ya kushusha kontena |
Alabama
Business Council.
Dr. Slaa amekutana na viongozi wa
juu wawili wa “Alabama Business Council” Katika chakula cha jioni
kilichoandaliwa kwa ajili yake na taasisi hiyo. Mwenyekiti wa Alabama Business
council ameahidi kuhamasisha makampuni makubwa kwenye jimbo la Alabama
kumsaidia Dr. Slaa na Chadema kunyunyua uchumi wa Tanzania kwa kuwekeza kwenye
sekta mbali mbali za uchumi wa Tanzania kama Kilimo, elimu, viwanda,
miundombinu nishati nk.
 |
Chakula cha jioni iliyotayarishwa kwa ajili ya Dr. Slaa |
 |
Dr. Slaa akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa rafiki yake |
 |
Dr. Slaa na Msaidizi wa zamani wa Rais Bush wakiwa katika majadiliano |
 |
Dr. Slaa akipokelewa na kiongozi wa Alabama Business Council ambaye pia alikuwa msaidizi wa Rais Bush Snr. kwenye maswala ya kiuchumi |
No comments:
Post a Comment