Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, September 13, 2013

Moto waendelea kuwaka UVCCM


 
          Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)  Wilaya ya Rorya, mkoani Mara, umetishia kuendesha kampeni nchini kote kuwaondoa madarakani viongozi wake wa makao makuu wanaoendekeza migogoro kwa madai kwamba, inatishia kukisambaratisha chama hicho. Tamko hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Rorya, Sango Kasera, baada ya kuhitimisha ziara ya siku 15 katika kata 14 za wilaya hiyo kwa lengo la kuhamasisha vijana kuunga mkono serikali mbili, na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2005-2010. Alisema wanasikitishwa na mgogoro uliopo ndani ya UVCCM makao makuu na kusema iwapo utaendelea, watawasilisha mapendekezo kwenye Baraza Kuu la Umoja huo Taifa kuwaondoa madarakani vinara wote wa mgogoro.
 
      “Tutachukua fomu kisha tutazunguka nchi nzima kuwapa wenyeviti wa jumuiya wa wilaya washinikize wajumbe wa Baraza Kuu wawavue uongozi,” alisema Kasera.  Alisema anawashangaa viongozi hao kwani badala ya kukaa na kujenga chama, wao wamekuwa wakiendekeza migogoro. Kasera alisema wanapinga mgogoro kwa kuwa mara zote unapoibuka na kushamiri wao ndiyo wanaoumia, hivyo akaonya kuwa: “wasipoangalia wataondoka kwa aibu.”. Aliwataka vinara wa mgogoro katika UVCCM makao makuu kuiga uongozi mzuri wa Mwenyekiti mstaafu wa Umoja huo, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi. “Dk. Nchimbi katuachia assets (mali) kubwa. Kajenga jengo la UVCCM, ambalo linaweza kuwalipa wafanyakazi mishahara. Na alistaafu, huku akiwa amewaunganisha vijana nchi nzima, aliijenga jumuiya akaiacha ikiwa na umoja na mshikamano. 

      Siyo kama ilivyoparaganyika hivi sasa,” alisema Kasera. Katika hatua nyingine, Kasera aliwataka vijana kutowaunga mkono baadhi ya wanachama walioanza kujipitishapitisha majimboni wakifanya kampeni za chini chini kutaka kugombea ubunge mwaka 2015. “Vijana wawahoji watu hao walichowafanyia miaka iliyopita. Tuwahukumu kwa rekodi zao,” alisema Kasera.


Source: Said M. (Sept. 2013).Moto waendelea kuwaka UVCCM. Retrieved from 

No comments: