Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, September 13, 2013

JK azidi kubanwa


    
      KAMATI Maalum ya Katiba inayoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, imemta Rais Jakaya Kikwete kutazama mapungufu yaliyomo katika muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba kabla ya kuisaini. Pamoja na nia njema aliyokuwa nayo Rais katika mchakato huo ili kupata Katiba yenye muafaka wa kitaifa kwa sasa mchakato huo umetekwa na wanasiasa. Akizungumza na waandishi wa habari jana, mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Khoti Kamanga, alisema kuwa mswaada huo umeingiliwa na wanasiasa kwa maslai yao binafsi. “Namuomba Rais Kikwete kutoweka saini kwa sababu nashangaa kuona wanasiasa leo ndio wanakuwa wenye sauti kwenye huu mswaada. Kamati hii ilitoa ushauri wa kitaalamu kuwa kazi ya kutengeneza Katiba si ya wabunge bali wananchi kwa ujumla wao lakini inakuwaje sasa?

       Dk. Kamanga pia alieleza kushangazwa na muswada huo kutowashirikisha watu wa Zanzibar kwani huko ni kuwatenga wakati wana haki katika muswada huu. ‘‘Hoja aliyoitoa Lissu (Tundu) ina mashiko, inabidi iungwe mkono na wabunge wote kwa sababu Wanzanzibari hawakushirikisihwa, kwa hiyo kitendo hicho ni kuwatenga wakati nao wana haki katika Katiba hii. “Lakini kutokana na Naibu Spika, Job Ndugai, kuendesha Bunge kwa kushinikizwa, aliidharau hoja ya Lisu,’’ alisema. Akizungumzia vipengele vya muswada huo wa marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013, Kamanga alisema kuwa havifai kwani vitasababisha kupatikana Katiba mbovu yenye kuwanufaisha wanasiasa. “Ukitazama sheria ilivyo katika kifungu cha 22(1) kuhusu wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, idadi ya wabumge (wanasiasa) itakuwa ni zaidi ya asilimia 72.


       “Wananchi wengine kutoka makundi ya kijamii wamepewa nafasi 166 tu ambayo ni sawa na asilimia 27, hii ni kasoro pia,’’ alisema. Naye mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Jasiah Kabira cha mjini Bukoba, Kagera, Dk. Azaveli Lwaitama, alitahadharisha kuwa nchi inaweza kuingia kwenye machafuko kama wanasiasa wakiachiwa wao waamue Katiba mpya. “Hii ni hatari inaweza kutokea endapo wanasiasa wakituandalia Katiba. “Wanasiasa hususan wabunge wa CCM ndio wanaumia sana kuona Katiba mpya inapatikana kwa sababu kuna vipengele ambavyo wanavipenda,” alisema.

      Alivitaja baadhi ya vipengele hivyo kuwa ni kile cha wabunge kutokuwa mawaziri akisema kuwa hawavitaki kwa sababu wananufaika na nyadhifa hizo. Alimwomba Rais Kikwete kuutupilia mbali muswada huo akidai kuwa upo kwa ajili ya wanasiasa na kwamba endapo akiusaini utamshushia hadhi yake kwa wananchi. Kamati hiyo iliwapongeza wabunge wa upinzani kwa kuonyesha umoja na mshikamano kupinga muswada huo kwa kile walichodai umejaa kasoro nyingi na haufai kutumika. “Watu wengi wanajadili jinsi ngumi zilivyopiganwa bungeni, wameacha kile kilichofanya fujo hizo kutokea. “Sisi tunawapongeza kwa hatua ya kugundua mapungufu katika maswala ya wananchi,” alisema Lwaitama.

Source: Vinsent k. (Sept. 2013). JK azidi kubanwa. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: