Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, September 16, 2013

CHADEMA yalaani matendo ya Balozi wa China, Dk. Lu

Balozi wa China, Dk. Lu Youqinq, nchini Tanzania akiwa kwenye jukwaa la CCM

Leo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake Ndugu Benson Kigaila na John Mrema,wametoa tamko kulaani kitendo cha Balozi wa China kujiingiza ktk siasa za chama tawala na kusimama majukwaani kuongelea sera na siasa za chama tawala CCM. Ndugu Kigaila amesema kitendo hicho ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za Umoja wa Mataifa za Mambo ya mahusiano ya kimataifa na diplomasia chini mkataba wa Vienna.

Chadema imesema inalaani kitendo hicho na itachukua hatua kwenda Umoja wa Mataifa na pia kupata maelezo toka Serikali ya China kama imemtuma balozi huyo kujihusisha na mambo ya siasa za ndani za vyama au kuiwakilisha nchi.

Akijibu tuhuma hizo Nape Nnauye amenukuliwa akisema,hakuna ukiukwaji wowote wa sheria wala mkataba wa Vienna,balozi huyo ni mwanachama wa chama cha kikomunisti cha nchini China,ambacho ni chama rafiki kwa CCM toka Uhuru,hivyo licha yakuwa ni balozi,lakini pia ni mshauri wa chama cha Mapinduzi ambacho ni rafiki wa CCP.

NAPE amenukuliwa akisema kuwa alichofanya balozi huyo ni kitendo cha kuungwa mkono,mana alikuwepo kwa nia ya kuangalia maeneo ya uwekezaji wa zao la Pamba ktk eneo la Shinyanga..ambapo amesema uwekezaji huo utasaidia kuondoa tatizo sugu la ajira,kupanda kwa bei ya zao la pamba ambacho kimekuwa kilio kikubwa cha wakulima pamoja na ujengwaji wa viwanda vya nguo na kuchuja mafuta.

Hivyo ni vema kumpongeza balozi huyo na kuunga juhudi za CCM za kuwatafuta wawekezaji wa nje badala ya kusingizia uvunjaji wa Mkataba wa Vienna ili kupata umaarufu wa kisiasa

NB: ITAKUMBUKWA KABLA YA KUONEKANA HUKO KISHAPU,BALOZI HUYU ALIKUWEPO PIA KTK MKUTANO WA NDANI.WA CCM HUKO IRINGA..WAKATI WA ZIARA YA KINANA NA NAPE KTK MKOA WA IRINGA NA NJOMBE..NA KTK KIKAO HICHO BALOZI HUYO ALITOA AHADI YA KUJENGA/KUKARABATI MAJENGO YA CHUO CHA MAFUNZO IHEFU(IHEMI?)MKOANI IRINGA ILI KUTOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA UKAKAMAVU KWA VIJANA NA MAKADA WA CCM..CHUO HICHO KILIANZISHWA WAKATI WA SIASA ZA CHAMA KIMOJA ILI KUANDAA MAKADA WA CCM KAMA ILIVYO KILE CHA KIVUKONI.

Barafu/Jamii Forums

No comments: