Pamoja na kwamba kumekuwa na mijadala mingi kuhusu
kipindi kilichooneshwa Juzi Jumamosi Stat TV, bado naomba na mimi nichukue
nafasi hii kuendeleza mjadala huu, kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo:
1. Hoja kwamba mitafaruku na migongano mingi hutokea bungeni na
sio katika kamati. Ndugai alijenga hoja kwamba hii ni kwa sababu kuna Kamera
bungeni wakati katika kamati hakuna kamera. hoja yake ni kuwa wapinzani, hasa
CHADEMA, wanatumia nafasi hiyo ya kuonekana kwenye kamera, kufanya
"vituko". Jibu la Mnyika: Kamati siyo chombo cha maamuzi ya mwisho.
chombo cha maamuzi ya mwisho ni bunge. kwa mantiki hiyo, lazima kuwe na
mtifuano katika hatua ya bunge kwa kuwa hapo ndipo muhimu zaidi. na kwa hiyo
hata kama kusingekuwa na kamera, mtifuano ungetokea. kwa mawazo yangu, Hoja ya
mnyika ni logical and sensible, hasa ukizingatia kwamba kuna maamuzi mengi
ambayo inaonekana yanatetewa na wabunge wa CCM kufuta "pressure"
kutoka CCM, na ambayo yanapingana na maslahi ya taifa kwa ujumla. mfano dhahiri
ni huo muswada wa mabadiliko ya sheria ya katiba mpya ulioleta mzozo hivi
karibuni.
2. Hoja kwamba inakuwaje mitafaruku mingi na vurugu hutokea
anapokuwepo Mh. Ndugai. Hoja ya Ndugai hapa ilikuwa pengine watu wanamuona kuwa
yeye nidhaifu, ndio maana wanafanya vurugu. Jibu la Mnyika: hapa Mnyika
alishangilia kwa furaha kwamba hatimaye amepata jibu la swali ambalo
limemsumbua siku nyingi. kumbe Mh. Ndugai ana tatizo la INFERIORITY COMPLEX!
Hapo Ndugai alikuja juu sana na kufoka kwamba Mnyika amemtukana kumwambia
kwamba ana INFERIORITY COMLPLEX!! Kwa maoni yangu, Ndugai hawezi kumlaumu
Mnyika kwa kujenga hoja hii, kwa sababu "opening" aliitoa mwenyewe,
Mnyika akapenyeza ngumi ikatua usoni. ngumi hiyo ni halali kabisa.
3. Hoja ya umri. Ndugai alirejea hoja hii mara kadhaa. katika
taharuki yake pale Mnyika alipomwambia kwamba kwa kuwa amekiri kwamba ni
dhaifu, basi ana INFERIORITY COMPLEX (inaleta maana hasa ukizingatia kwamba
mara nyingi katika midahalo Ndugai hupandwa hasira. rejea kipindi cha ITV cha
Kipima joto, Ndugai Vs Lissu), Ndugai alitoa kigezo kimoja cha umri, kwamba
Mnyika anatakiwa kumheshimu Ndugai kwa kuwa amemzidi umri. na kuna wakati
alikuwa anamjadili nadhani Mbowe, akasema kwamba ni mtu mzima wana rika moja.
Mnyika hakutoa jibu la hoja hii moja kwa moja, lakini nitachangia. kwa kawaida
hoja ya mantiki inatakiwa ijibiwe kwa hoja ya mantiki. tayari Ndugai
alishafanya kosa la kuzungumzia uwezekano wa yeye kuonekana dhaifu. inawezekana
subconscious yake ilikuwa ina-struggle kusema tu ukweli wake unaomsumbua muda
mrefu. alipotapika ukweli huo mbele ya dogo Mnyika, na mbele ya hadhara ya
ulimwengu mzima uliokuwa unamtazama, hapo hapakuwa na njia tena. hapo alitakiwa
aoneshe umahiri wake wa kupindisha mwelekeo wa mjadala, kitu kigumu lakini
inawezekana. kutumia kigezo cha umri ni hoja dhaifu sana katika mazingira yale,
inaonesha kushindwa hoja.
4. Hoja ya Ndugai vs. Mbowe. kuhusu hili, hoja kubwa ya Ndugai
ilikuwa kwamba kwa kuwa Mbowe aliposimama, Naibu Spika pia alisimama,
kumwashiria Mbowe aketi, Mbowe alikiuka kanuni kwa kuendelea kusimama. Hii ni
hoja nzito, imejikita kwenye kanuni. lakini najiuliza hivi: kanuni zimewekwa
ili kuwezesha bunge lifanye kazi zake vizuri, kwa njia bora na inayohakikisha
matokeo bora kwa maslahi ya taifa. Kanuni zinaweza kutumiwa kufunika au
kukwamisha yale ambayo zimeundwa kuyalinda. kwa uzito wa mjadala ule, na kwa
uzito wa Mh. Mbowe, Mh. Naibu Spika angeweza kabisa kuamua kumpa nafasi Mbowe
azungumze. yeye aliamua kutompa nafasi hiyo. Ni nani analinda maslahi ya taifa
hapo? Mantiki inatuelekeza kwamba katika suala la Katiba, kinachohitajika ni
maridhiano zaidi kuliko ushindi wa walio wengi, busara na hekima zaidi kuliko
kutimiza kanuni au kutumia fimbo ya kanuni. inaonekana hapa Ndugai ametumia
fimbo ya kanuni kukidhi mahitaji ya kundi fulani katika jamii.
Hatima:
Kwa ujumla, Mnyika alijitokeza kama mpambanaji wa hali ya juu,
anayetumia akili, na hekima zaidi kuliko umri wake, na hivyo kumzidi Ndugai
ambaye alitaka kujenga hoja kwamba akili na hekima zikipungua, ongezea na idadi
ya miaka ili uwe na akili na hekima nyingi zaidi!!
Mnyika, kwa wale ambao walikuwa wanasikitika kwamba LISSU
hayupo, basi Ndugai leo anaserereka tu - wapi! dogo kamkomalia mpaka povu
likamtoka Ndugai wa watu jamani! huruma?
No comments:
Post a Comment