Hatimaye msajili wa vyama vya siasa Nchini John Tendwa ameibuka
na kusema sasa anaandaa kalamu yake kukifuta Chama kikuu cha upinzani nchini
CHADEMA.
Katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari muda mfupi uliopita
Tendwa amesema CHADEMA wanataka kuanzisha kikundi cha mgambo ambacho ni kinyume
na sheria,katiba ya nchi na sheria za usajili wa vyama.
Msajili huyo ambaye inadaiwa ni mwanachama mwaminifu wa CCM
amesema kwamba kama madai ya CHADEMA ni kuanzisha kikundi cha kujilinda dhidi
ya Green Guard wa CCM madai hayo hayana msingi wowote kwani kama CHADEMA wana
taarifa kwamba Green Guard wanahatarisha amani basi wanapaswa kuripoti suala
hilo polisi ili lifanyiwe kazi kwa mujibu wa sheria.
Tendwa amezidi kuonya kwamba uamuzi wake ni wa mwisho na
atakapoifuta CHADEMA maamuzi yake hayapingwi popote kisheria.
Tangu Kamati Kuu CHADEMA itoe tamko la kufundisha vijana wake
ukakamavu kukabiliana na ukatili na uharamia unaofanywa na kikundi cha Green
Guard ni kama Taifa limesimama na hiyo imekuwa ni habari kuu kila mahali. Dhihirisho
linaloonyesha kwamba CHADEMA ndicho chama kinachofuatiliwa habari zake zaidi
hapa nchini na pia kuwa na idadi kubwa zaidi ya watanzania wanaokiunga mkono.
Viongozi ambao wameshazungumzia Tamko hilo la CHADEMA ni Rais
Jakaya Kikwete, Jeshi la Polisi nchini,Viongozi wakuu wa CCM,Mwenyekiti wa NCCR
James Mbatia na sasa Msajili wa vyama John Tendwa.
Source: Molemo. (July 2013).Tendwa: Kwa hili la Red Brigade, Nitaifuta CHADEMA!. Retrieved from Jamii Forums
1 comment:
Tanzania haijawahi Kuwa na msajili wa vyama mpumbwvu kama John Tendwa!
Post a Comment