Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, July 15, 2013

Ufisadi wa ardhi Kigilagila wamuumbua ofisa Ilala


Mkazi wa Kiluvya “A” katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, akichangia mada kwenye mkutano wa wananchi na Maofisa Ardhi kutoka wilayani kuhusu mradi wa kupanga, kupima na kuuendeleza Mji wa Kisarawe na kata zake. Katikati ni Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye ambaye ni Mkazi wa Kiluvya. Picha na Venance Nestory
     
       Ofisa Tarafa wa Ukonga, Jeremiah Makolele alijikuta katika wakati mgumu mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi baada ya kushutumiwa na wananchi kuwa amegawa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya huduma za kijamii. Ofisa huyo ambaye ni Katibu wa Kamati ya Ugawaji Viwanja vya wakazi wa Kigilagila anatuhumiwa kugawa viwanja halali kwa watu ambao si wakazi wa maeneo hayo katika eneo la Zavala Manispaa ya Ilala. Waliolalamikia suala hilo ni wale waliohamishiwa katika eneo la Zavala ili kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere huku wakidai maeneo yao yameuzwa na kupewa watu wasiohusika wakiwamo maofisa Ardhi wa Manispaa ya Ilala.
    Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi hao walisema wameshangazwa na kamati hiyo kwa kuwanyima viwanja vyao na kuwapa watu wengine huku wakipelekwa eneo lililotengwa kwa ajili ya huduma za jamii ambalo ni la kuzika. Mkazi Salehe Iddi alisema, kiwanja cha awali alichopewa na Serikali kilikuwa Kiwanja L chenye  namba 186 na alibadilishiwa na kamati hiyo ambapo alipewa kiwanja kilichopo eneo la huduma za jamii ambalo ni eneo la makaburini kiwanja namba T269/32. Alisema mkazi mwingine Lucy Juma kiwanja chake cha awali ni L  chenye namba 183 na kupewa kiwanja cha huduma za jamii eneo la makaburini chenye namba T269/32 na mwingine Ponziane Maliwa kiwanja chake cha awali kilikuwa L chenye namba 180 na kupewa eneo la makaburini T269/32.
    Iddi alisema baada ya kupeleka malalamiko hayo kwenye kamati hiyo , walielezwa kuwa viwanja vilivyopo ni hivyo kama hawataki  wangepokonywa na kupewa watu wengine. “Nilifuatilia kiwanja changu chenye namba 186 kauziwa mtu ambaye hahusiki kabisa na si mkazi wa Kigilagila lakini baada ya kufuatilia bila ya mafanikio niliambiwa na Katibu Tarafa ambaye ni Katibu wa kamati hiyo kuwa kama sitaki kukipokea kiwanja walichonipa cha eneo la makaburi atapewa mtu mwingine,”alisema Idd. Naye Mwenyekiti wa Mtaa huo, Mohamed Ramadhani alisema ni kweli hayo maeneo yalitengwa kwa ajili ya huduma ya jamii ikiwamo makaburi wamepewa na wakazi hao na kamati hiyo kwa ajili ya ujenzi.
     “Pia nimeletewa malalamiko na wakazi wa eneo hilo kuwa eneo lililotengwa kwa ajili ya shule limekatwa nusu na kuuziwa mtu mmoja ambaye hajulikani na ameanza kupanda miti eneo hilo,”alisema Ramadhani. Ofisa Tarafa huyo, Jeremiah Makolele alikana na kusema hilo eneo la huduma ya jamii lipo hajaligawa kwa wakazi hao na litaendelea kuwapo.Mkuu wa Wilaya hiyo,Raymond  Mushi alisema suala hilo limemfikia hivyo atawaita ofisini waliopatwa na mkasa huo pamoja na  kamati hiyo ili kujua tatizo  lipo wapi.
Source: Chilongola P. (July 2013).Ufisadi wa ardhi Kigilagila wamuumbua ofisa Ilala. Dar. Retrieved from Mwananchi

No comments: