TAFADHARI FUATA LINK MWISHO KUWEKA SAINI KWENYE WITO HUU
Why
this is important
Sisi
wananchi wa Tanzania:
•
Tukiwa ni wapiga kura wa majimbo mbalimbali nchini Tanzania, tumechukua jukumu
leo kutoa wito kwa wabunge na serikali kufuta tozo/kodi mpya ya laini za simu
iliyoanza kutumika baada ya sheria kupitishwa na Bunge Juni 2013.
•
Hii ni sehemu muhimu ya wajibu wetu kama raia waaminifu, wenye nia njema
ya kuchangia mawazo bora yatakayotuletea maendeleo endelevu nchini kwetu.
•
Bila mjadala mpana na mawazo chanya yaliyochambua masuala kwa undani kama
msingi wa maamuzi, nchi itafanya maamuzi dhaifu yasiyosimama kwenye misingi ya
hoja na ukweli wa mambo.
•
Kukaa kimya kwenye jambo ambalo tunaliona linakandamiza wananchi na huenda
likaturudisha nyuma kimaendeleo, ni kushindwa kuwajibika kama wananchi.
Tunapinga
kodi ya laini za simu:
KWA
SABABU:- Sisi wananchi hatujashirikishwa kupitia mjadala wa Bunge kuhusu kodi
hii kwani Waziri wa fedha hakusoma hiki kipengele wakati wa hotuba yake na
tulikosa taarifa mpaka baada ya kupitishwa kwa sheria ya kodi hii.
KWA
SABABU:- Kodi hii inamkandamiza mtanzania wa hali ya kawaida na wa hali ya
chini ambao ni 67% ya wananchi wanaoishi chini ya kipato cha dola 1.25 (shs
2,000) kwa siku. Takwimu zinaonyesha kuwa kati wa wamiliki wa laini za simu
milioni 22, milioni 8 wanatumia chini ya shilingi 1,000 kwa mwezi. Kuwaongezea mzigo
wananchi hawa kwa kiwango ambacho tayari wanashindwa kumudu ni kuwanyima kabisa
fursa ya kutumia huduma hii muhimu.
KWA
SABABU:- Kodi hii haifuati misingi ya kulipa kwa kadri ya matumizi na ni kodi
kandamizi inayowatoza wamiliki wa laini ya simu wote kiasi kimoja bila
kuzingatia kiwango cha matumizi. Hii inamkandamiza mwananchi wa hali ya chini
kwa kumlazimisha kulipa kiwango kikubwa cha kodi kulingana na mapato yake.
Tukichukulia mfano wa mtu anayetumia shilingi laki tano kwa mwezi kama muda wa
maongezi na yule anayetumia shilingi elfu tano - na tukilinganisha uwiano wa
malipo haya na matumizi yao – basi yule anayetumia shilingi laki tano analipa
0.2% ya matumizi yake, ila yule anayetumia shilingi elfu tano anatozwa 20% ya
matumizi yake.
KWA
SABABU:- Kodi hii ni juu ya ongezeko la kodi mbalimbali katika huduma za simu
za mkononi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ushuru kutoka 12% kwenda 14.5% na
pia kodi hii kutozwa kwa huduma zote ingawa awali ilitozwa kwa huduma ya
matumizi ya kuongea. Hivi sasa utumiaji wa internet, kutuma na kupokea pesa kwa
njia ya simu za mkononi unatozwa kodi. Ongezeko hili pekee limeshafanya huduma
za simu za mkononi kupanda gharama kwa kiasi kikubwa. Ongezeko hili la shs
1,000 litazidi kuwaumiza wananchi.
KWA
SABABU: - Kodi hii pekee inampunguzia mtumiaji muda wa maongezi na huduma
zingine za simu za mkononi ikiwa ataendelea na matumizi yake ya mwezi kama
kawaida. Kwa mfano mtumiaji akitumia kifurushi cha bei ya shs 475 inayompa
dakika 20 za maongezi, 50 MB za data, na sms 100 kwa masaa 24, kwa kodi ya shs
1,000 kwa mwezi ni sawa na serikali kuchukua siku mbili za kifurushi hiki kila
mwezi au ni sawa na kuchukua dakika 40 za maongezi, 100MB za data na sms 200
kila mwezi.
KWA
SABABU:- Huduma ya simu za mkononi siyo anasa na ni sehemu muhimu ya
mawasiliano na kiungo kinachochangia kurahisisha harakati za maendeleo. Kwa
mfano wakulima hutumia huduma hizi katika kuuza mazao yao na kupokea fedha;
akina mama wajawazito hupelekewa taarifa muhimu kuhusu afya zao; wanafunzi
kupitia internet wanaweza kupata habari muhimu zinazohusiana na masomo yao nk.
Kodi hii itawanyima fursa ya kutumia huduma hizi muhimu.
KWA
SABABU:- Serikali inaweza punguza matumizi yake mengineyo (safari, posho,
semina, manunuzi ya magari na kudhibiti ufisadi) hivyo kufidia pengo
litakalosababishwa na kusitisha tozo/kodi ya laini ya simu.
KWA
SABABU:- Pia, utafiti uliofanywa na Interfaith Standing Committee on Economic
Justice and the Integrity of Creation mwaka jana uligundua kuwa kwa wastani Tanzania
hupoteza dollar billion moja (takriban shs trilioni 1. kila mwaka kutokana
na ukwepaji kodi, uhamishaji harama wa fedha na misamaha ya kodi. Tunaitaka
Serikali yetu iongeze ufanisi wa kukusanya kodi kutoka vyanzo vilivyopo tayari
na kuondoa misamaha kwa hivyo itaziba pengo la shs billioni 264 kutoka kwa kodi
ya laini ya simu za mkononi.
Saini petition hapa WITO WA KUSITISHA TOZO/KODI YA LAINI YA SIMU KILA MWEZI
No comments:
Post a Comment