Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, July 22, 2013

Kesi ya ugaidi makada wa Chadema ni leo


   Mahakama Kuu Kanda ya  Tabora leo  inatarajia kusikiliza kesi ya ugaidi dhidi ya makada watano wa Chadema  iliyotolewa uamuzi na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Tabora kuwa haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo . Mahakama hiyo inatarajia kutoa uamuzi dhidi ya hoja zilizowasilishwa na mawakili wa uapnde wa utetezi, Peter Kibatala pamoja na Profesa Abdallah Safari kuwa sheria  zilikiukwa katika kuwasilishwa kwa kesi hiyo. Washtakiwa ni Evodius Justunian, (30) mkazi wa Bukoba, Osca Kaijage mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Seif Magesa mkazi Nyasaka Mwanza, Rajabu Daniel  mkazi wa Dodoma na walikuwa wakishtakiwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Igunga kabla ya Henry Kilewo kuunganishwa katika kesi hiyo.

      Akizungumza  kwa njia ya simu,  wakili Kibatala alisema kuwa katika Mahakama Kuu watahakikisha wanashambulia mashtaka hayo kwa kufuata sheria ili kila kitu kisikilizwe upya. Alisema kuwa mashtaka hayo hayana mashiko ya kuitwa makosa ya kigaidi na kuongeza kuwa Mahakama Kuu wataiomba iyaangalie kwa mara ya pili kwa umakini zaidi.
Source: Kapalala M (July 2013).Kesi ya ugaidi makada wa Chadema ni leo. Retrieved from Mwananchi

No comments: